Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1570706204430.jpeg
 
Hakika bro, elimu kwa njia ya vitendo ni bora sana tena sana sana
Bro. Nimejifunza haya mambo kwa vitendo kama mwalimu wa kujitolea katika shule za watoto wenye vipaji huko kwa Trump kwa miaka zaidi ya minne. Naingia darasani. Nawasaidia walimu. Najifunza wanavyofundisha. Naangalia mitaala yao ilivyo. Shule zao zimegawanywa katika michepuo tangu watoto wakiwa Middle School. Wanaotaka kuwa madaktari. Manesi. Wafamasia. Wahandisi. Wataalamu wa kompyuta, ufundi wa vitu mbalimbali (magari, ndege, umeme, Radiology technician, dentist assistant...)...Kama ni mchepuo wa udaktari, kwa mfano wanafundishwa kwa vitendo. ABC za kuwa daktari. Wanatembelea mahospitali. Wanaangalia madaktari wanavyofanya kazi. Madaktari wanaalikwa kuja shuleni na kufanya upasuaji mdogo mdogo. Wanajifunza kwa vitendo...Watoto wanahamasika sana.

Hili limekuja baada ya Marekani kujikuta inaachwa nyuma na nchi zingine hasa katika sayansi na tekinolojia; na wanahaha sana kubadili hiyo hali. Nao wamekumbwa pia na hatari ya kuzalisha wahitimu ambao hawana uzoefu kivitendo. Na mkazo sasa unaelekezwa huko. Mtu awe akimaliza high school awe na kitu tangible cha kufanya na siyo kukariri fomyula tu za Algebra na upuuzi mwingine.

Nimekuwa nikiandika andika mapendekezo yangu kuhusu jambo hili kwa muda mrefu na sasa nina kakitabu kabisa na mapendekezo kibao. Nataka nimpelekee waziri na naamini kwamba baadhi ya mapendekezo yatasaidia sana kwa sababu wala hayahitaji pesa nyingi. Japo najua yatatupwa tu huko lakini ni lazima tubadilishe mfumo wetu wa elimu vinginevyo huko tuendako hatutafika...

Asante bro ...
 
Back
Top Bottom