Moja kati ya manufaa makubwa ya kuwa na ratiba ni kuweza kutumia muda vyema. Unapokuwa na ratiba ni vigumu kupata muda ambao haujapangiwa jukumu au kazi kwenye ratiba.
Unapokuwa na ratiba muda wako wote utatumika vizuri tena kwa shughuli yenye tija iliyopangwa. Hivyo ni vyema kuhakikisha unajiwekea ratiba na unaifuata ipasavyo.
Kuweka ratiba ni mbinu mojawapo ya kuweka vipaumbele. Unapoweka ratiba ni lazima utaondoa mambo yasiyo ya msingi ili ratiba yako ikae vyema na itekelezeke.
Ni vigumu sana kusahau jambo ambalo lipo kwenye ratiba yako. Hii ni kutokana na sababu kuwa unafanya kazi kwa kufuata ratiba, kila mara utakuwa unatazama ratiba yako inataka ufanye nini na kwa muda gani.
Unaposahau mambo unayotakiwa kuyafanya, unapaswa kurejea kwenye ratiba yako na kutazama inataka ufanye nini.
Watu wengi wanakosa muda wa kupumzika kwa sababu wanafanya hiki mara kile bila mpangilio maalumu. Hili huwafanya kuhangaika siku nzima bila hata kujua wamekamilisha nini.
Utamsikia mtu akisema “leo nimechoka sana hata sijui nimefanya nini” “leo nahangaika tu hata hamna nilichofanya”. Hii inaonyesha kuwa mtu huyu amechoka bila hata kukamilisha kazi zake.
Kwa kujiwekea ratiba utaweza kupanga muda wa kazi na muda utakaoutumia kwa ajili ya kupumzika.
Mbinu mojawapo nzuri ya kuacha tabia mbaya ni kujipangia ratiba ngumu na kuifuata. Kama kuna muda ambao unautumia kufanya matendo kamavile ulevi, matumizi ya madawa ya kulevya, uzinzi, umbea, n.k. Basi upangie muda huo majukumu mengi kwenye ratiba yako.
Kwa kuzingatia hili hutopata muda wa kupoteza kufanya matendo au tabia ambazo kimsingi siyo nzuri
Ikiwa umeajiriwa unaweza kukosana na mwajiri wako kwa kuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yako vyema. Jambo hili linaweza kukunyima utulivu wa kiakili.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.