Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
FB_IMG_1561075080844.jpeg
 
Mtoto mdogo wa chini ya miaka mitano alipatikana akilia kwa hofu ndani ya nyumba akisema, "Sitaki kufa ".
Wazazi wake waolikua wameshawishiwa kuwa chanjo ya polio ni salama walijaribu kummtoa nje ashuhudie ndugu zake wakiwekewa matone ya chanjo hiyo mdomoni.
Lakini mtoto huyo aliendelea kulia kwa uwoga. Wahudumu wa afya ya jamii wanaotoa chanjo hiyo walikua wamekatazwa kuendesha kampeini hiyo katika moja ya vijiji nchini Pakistan hadi waliposaidiwa na Dr Uzma Hayat Khan, mshauri wa afya ya umma.
 
Khan, ambaye ni mshirikishi wa kampeini ya chanjo ya polio nchini anauzoefu wa kuwzungumza na watu wanaokataa watoto wao wapewe chanjo hiyo.
Lakini alikuwa na hofu alipofika katika boma hilo kwa sababu alikutana na kundi la wanaume ambao walimkataza ingie nadi ya nyumba.
Purukushani hilo lilimalizika baada ya jamaa mwingine wa familia hiyo ambaye ni daktari kutokea na kuwasaidia.
 
Wahudumu wa afya walifanikiwa kwapatia chanjo watoto wote katika boma hilo isipokua yule aliyekuwa akilia kwa uwoga.
Watu wengi nchini Pakistan wanahofia sana kupewa chanjo ya polio licha ya kuwa inaokoa maisha
Lakini hali ni mbaya zaidi katika mji wa Rawalpindi ambako vurugu zinazotokana na wakaazi ambao hawataki watoto wao wapewe chanjo ya polio ni ni za kiwango cha juu.
 
Ziara ya siku ya kwanza kabla ya uzinduzi wa kampeini ya chanjo katika shule moja ya vijijini iliopo viungani mwa mji wa Peshawar iliishia kuwa vurugu huku watu wengine wakiishia kuchomeana nyumba.
Mwalimu mkuu wa shule ya Mashokhel aliwahi kukataa watoto wapewe chanjo ya polio lakini mara hii alishurutishwa na serikali aruhusu shughuli hiyo.
Lakini muda mfupi baada ya wao kuanza kazi aliwapigia simu wazazi na kuwafahamisha kkuwa watoto wao walikuwa wanapoteza fahamu na kutapika.
 
Makumi ya watoto kutoka shule hiyo walipelekwa hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na hawakupatikana na tatizo lolote.
Lakini tulikua tumechelewa sana kukabiliana na hofu hiyo kwasababu hofu ya wanavijiji ilikuwa imesambazwa katika kitandao ya kijamii.
Wazazi waliokua na hasira walikusanyika nje ya kituo cha afya cha katika kijiji hicho na kuanza kuvunja lango lake kwa kutumia magongo na nyundo na walipofanikiwa kuingia ndani waiichoma moto.
Tukio lote hilo lilioneshwa kwa Televisheni hatua ambayo ilizua ghadhabu zaidi kote mjini Peshawar.
 
Kwa ujumla karibu watoto 30,000 kutoka shule tofauti katika mji huo walipelekwa hospitali, kwa mujibu wa serikali.
Katika taarifa waziri wa afya katika mkoa huo alisema hali hiyo ya wasiwasi ilichangiwa na viongozi wa kidini katika misikiti ya eneo hilo waliokuwa wakitoa tahadhari kwa wazazi kuwapeleka watoto wao waliopewa chanjo hospitalil. Lakini watoto hao walikua hawana neno. aliongeza
Lakini visa hivyo vinatishia kuvuruga kampeini ya polio nchini humo.
Kampeini hiyo iliyochukua siku tatu katika mwezi wa Aprili ilisababisha vifo vya wahudumu wawili wa afya na maafisa wawili wa usalama waliokuwa wameungana nao kuwapa ulinzi.
 
Watu wanatuzomea njiani na wenye maduka vijijini walitufukuza, mmoja wao walisema, ''Mko hapa kuwapa sumu watoto wetu!''.
Serikali ililazimika kusitisha kwa muda kampeini ya kitaifa ya ya chanjo hiyo kwa wiki kadhaa hadi hali itulia.
Lakini wafanyikazi wa afya wanauhakika chanjo hiyo ni muhimu .
 
Ni kinga dhidi ya magonjwa hahatari ya utotoni ambayo yanashambulia mfumo wa neva na huenda ikasababisha mtoto kupooza.
Mtu mmoja kati ya 200 hupooza kati ya visa 200.
Polio inaweza kusababisha maafa saa kadha baada ya kingo kama mapafu kushindw kufanya kazi. Polio Haina tiba.
 
Lakini chanjo dhidi ya kupooza imesaidia sana katika harkati ya kutokomeza ugonjwa huo duniani.
Ni mataifa matatu tu ambayo bado yanakabiliwa na janga la kupoza ikiwa ni pamoja na - Pakistan, Afghanistan na Nigeria.
Nigeria haijawahi kuripoti kisa chochote cha ugonjwa huotangu mwezi Augosti mwaka 2016, na inatarajiwa kutangazwa kuwa huru dhidio ya polio miezi michache ijayo.
 
Pakistan ilikuwa inaelekea kutangazwa kuwa huru dhidi ya ugonjwa huo lakini ilirudi nyuma kutokana na sababu ambazo hazingeweza kuepukika.
Ilikuwa imepunguza viwango vya maambukizi kutoka visa 22,000 mwaka 1994 hadi visa 100 kutoka mwaka 2015 kuendelea mbele..
Lakini mwaka huu umetajwa kuwa mbaya zaidi katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo.
Serikali ya Pakistani imeripoti visa 21 vya aina ya polio inayofahami- Wild Polio Virus ama WPV1 - kuanzia Juni ikilinganishwa na mwezi wa Agosti mwaka 2017.
 
Back
Top Bottom