Asante mwalimu wa mavumbini, ila kila siku asubuhi upite kumwaga shikamoo kama shukurani ya kukuokota jalalani na kukuweka mahali hapa
_" Mhemiwa JamiiForum sikutegemea heshima hii toka kwako, mimi ni nani? Nimezaliwa kijiji cha vumbi, nimeishi maisha ya ufukara na baada ya kustaafu sikutegemea nitakuwa hapa lakini wewe na Mungu wako mnajua kwanini mmenitoa jalalani na nikawepo humu kwenye hii forum na kunifikisha hapa"
 
Asante mwalimu wa mavumbini, ila kila siku asubuhi upite kumwaga shikamoo kama shukurani ya kukuokota jalalani na kukuweka mahali hapa

Dr Benson Bagonza (Bishop)

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi wa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
 
Naanza kuamini mtu akizeeka anazeeka na akiri yake adi wewe mwandishi
naijatwittersavages-20190610-0002.jpeg
 
915 Reactions
Reply
Back
Top Bottom