Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siku hizi watu hufikiria kunywa mvinyo, lakini nchini Ufaransa ambako kulikuwa na kilimo cha mizabibu karne ya 5, mvinyo upande wa afya ulikuwa muhimu jambo ambalo bado lipo katika fikra za wengi hadi karne ya 21.
 
Kujifunza zaidi kuhusu uhusiano kati ya mvinyo na tiba, mwanahabari wa BBC alitembelea hifadhi ya divai katika hospitali moja ya Strasbourg, mashariki mwa Ufaransa.
 
Strasbourg, ni mji wa kisasa wenye historia ya miaka 2,000, ambao unafahamika kama kitovu cha divai na pia umetambuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kama urithi wa dunia mwaka 1988
 
Tangu mwaka 1395, hospitali ya Strasbourg imekuwa na uhisiano wa karibu na eneo la hifadhi ya divai: na kwa hali ya kawaida ni kwamba mtu hangeweza kuishi bila divai.
 
Kwa karibu miaka ya 600, wagonjwa wengi hospitalini walilipa gharama zao za hospitali kwa mashamba ya mizabibu - mizabibu ambayo ingepandwa kwa kipande hicho cha ardhi, ingetengenezwa mvinyo na kupelekwa katika hifadhi ya mizabibu.
 
Hili lilikuwa jambo la kawaida Ufaransa kwasababu mizabibu ilikuwa njia moja ya kuletea hospitali pesa.

Watu kutoka maeneo mbalimbali ya Ufaransa walitembelea hospitali hizo kupokea tiba ya divai ambayo ilikuwa ni kama chupa mbili za mvinyo kwa siku kutibu magonjwa mbalimbali.
 
Thibaut Baldinger, msimamizi wa hifadhi ya divai amesema kwamba ameona uthibitisho wa kuwa divai ilitumika kama tiba tangu 1960 - na tiba hiyo iliendelea hadi ilipositishwa 1990.

Kwa mfano, chupa moja ya divai aina ya Châteauneuf-du-Pape, ingependekezwa kwa mtu aliyevimbiwa huku chupa ya mvinyo aina ya Côtes de Provence rosé, ilitumiwa kutibu uzito kupita kiasi.
 
Kiwango kikubwa cha kolesteroli ilikuwa ni glasi mbili tu za Bergerac.

Kwa ugonjwa wa malengelenge, wagonjwa wangeombwa kuoga kwa mvinyo wa Muscat de Frontignan.
 
Glasi sita za mvinyo aina ya Saint-Amour ilikuwa tiba tosha na pia divai hiyo hiyo ilisemekana kwamba inatibu magonjwa kadhaa ya wanawake.
 
Ingawa tiba ya kutumia mvinyo ilisitishwa miongo kadhaa iliyopita, bado eneo la hifadhi ya mvinyo ni muhimu sana katika historia ya utengenezaji divai Ufaransa kwa kuendeleza kuonesha baadhi ya mvinyo wa kale huku eneo hilo likiendelea kuingizia hospitali kipato.
 
Zaidi ya karne 20, hospitali hiyo iliuza mashamba ya mizabibu kufadhili miradi kadhaa ya hospitali ambayo ilihitaji angalizo la haraka.

Lakini hifadhi hiyo ililazimika kuachana na pipa lake kubwa la mwaloni la kukoleza divai baada ua Ufaransa kubadilisha sheria mwaka 1991.

Sheria hiyo ilikuwa inalenga kuzuia unywaji wa pombe.
 
Hata hivyo mtangulizi wa Baldinger, Philippe Junger, alikuwa mtetezi mkuu wa hifadhi hiyo ya divai kwa kuunda shirika la kilimo ambalo limekuwa mtetezi wake na kushawishi wabunge umuhimu wa kuacha eneo hilo wazi kama njia moja ya kuendeleza urithi wa eneo.
 
Leo hii hifadhi hiyo inatengeneza chupa 140,000 za mvinyo wa Gewürztraminer, Klevener de Heiligenstein, Sylvaner na Riesling kwa mwaka kwa kutumia mizabibu iliyopandwa na washirika mbalimbali 26.

Mivinyo hiyo huwa ndani ya mapipa ya mwaloni ya kukoleza divai kwa miezi 6 hadi 10 kabla ya kufungashwa kwenye chupa na kuuzwa kwa umma.
 
Kuna baadhi ya mvinyo kwenye hifadhi ambayo haiuzwi. Mfano ni mvinyo wa kale uliobadilika rangi kwa sababu ya kutu unaofanana na damu iliyokauka ambao ulitengenezwa mwaka 1472.
 
Msimamizi wa hifadhi ya eneo la divai Baldinger, anasema mvinyo huu umeonjwa mara tatu tu: Mwaka 1576, mwaka 1718 wakati hospitali inajengwa tena baada ya kutokea kwa janga la moto na mwaka 1944 wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, hifadhi hiyo ikiwa chini ya udhibiti wa Wanazi.

Ni wazi kwamba watu hawaruhusiwi hata kukaribia sana mvinyo huo zaidi ya msimamizi ambaye aliusongelea na kusemea:
 
Ni wazi kwamba watu hawaruhusiwi hata kukaribia sana mvinyo huo zaidi ya msimamizi ambaye aliusongelea na kusemea:

"Unanukia vizuri,". "Pengine mtu anaweza kuuonja kidogo tu"
 
Msimamizi Baldinger alitingisha kichwa chake na kusema kiwango cha pH cha mvinyo huo ni 2.28 - ishara kwamba una asidi sana kiasi cha kuweza kusababishisa matatizo ya tumbo.

Sio kwamba mvinyo wote kwenye mapipa ulitengenezwa mwaka 1472.
 
Huwa tunaongeza mvinyo kila wakati unapoisha," Baldinger amesema. "Mara nne kwa mwaka, kati ya lita 4 hadi 6 huongezwa kwa mvinyo halisi wa lita 400. Tulichagua mvinyo wa Riesling au wa Sylvander ambao umekuwa kwenye hifadhi kwa miaka mingi."

"Mizabibu ya kwanza halisi iliyotumika kutengeneza divai hiyo kwa bahati mbaya haijulikani," Baldiner amesema. "Kumekuwa na mabadiliko mengi katika kipindi cha miaka mingi tu, pamoja na kuchanganywa kwa mizabibu mingine shambani wakati wa ukuzaji."
 
Lakini maneno hayo, hayangemzuia mwanahabari wa BBC kuonja mvinyo huo wa asili hata kama ingemaanisha kumsababishia matatizo ya tumbo na isitisho si kuna mvinyo ambao unasemekana kutibu tatizo kama hilo?

Hata hivyo kulikuwa na mivinyo mingine mingi kama vile wa Gewürztraminer ambao hadi mwaka 1990, glasi mbili tu zilisemekana kutumiwa kutibu maambukizi.

Na wakati wa kuondoka ulipowadia, mwanahabari wa BBC alijinunulia mvinyo aina ya Alsatian 'ambao ni tiba' kama zawadi kwa familia yake.
 
Hakikisha unajifunza kuishi na watu vizuri kuna muda heshima na nidhamu inaweza kukupeleka sehemu ambayo bidii haiwezi kukufikisha.” -
 
Back
Top Bottom