Uzi maalum wa kujuzana namna ya kufanya chochote

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,107
Unataka kujua/ kufahamu namna ya kufanya jambo fulani? Au unafahamu namna ya kufanya jambo fulani? Karibu tushirikiane, tupeane ma-tricks na solutions kwaajili ya kurahisisha maisha. Na mimi naanza kama ifuatavyo:

NAMNA YA KUTUMIA BARUA PEPE (eMail) MOJA KWA AKAUNTI NYINGI ZA TWITTER.
Kama ni mmiliki wa biashara, kuna uwezekano mkubwa unahitaji kuwa na akaunti mbili za Twitter. Lakini kuwa na barua pepe inayojitegemea kwaajili ya kila akaunti ni heka heka. Na kama umejaribu kutumia akaunti mbili kwa barua pepe moja, tayari unafahamu kuwa Twitter hawaruhusu hicho kitu, na utaletewa ujumbe wa “Email has already been taken”.

Hata hivyo, iko namna rahisi kabisa ya kucheza na hii changamoto. Sharti ni moja tu - uwe ni mtumiaji wa Gmail. Kwenye Gmail, unaweza kuongeza dot (.) popote kwenye username na email zote zitaingia kwenye inbox moja bila shida. Yaani kwa mfano, kama email address yako original ni; computervirus@gmail.com, basi email yoyote inayotumwa kwenda computer.virus@gmail.com au com.puter.virus@gmail.com itaingia kwenye mailbox yako original - kwasababu Gmail daima huwa ina-ignore hizo dots katika username.

Hivyo ndivyo unavyoweza kufanya ili kuwa-trick Twitter. Wao Twitter (Walivyokuwa wajinga) watachukulia computervirus@gmail.com na com.puter.virus@gmail.com kuwa ni email mbili tofauti na zilizo halali ingawa zina-point kwenye inbox moja. Kama unafikiri nafanya mazingaombwe, basi jaribu sasa hivi wewe mwenyewe.

Trick ya pili: Wakati unapofungua akaunti mpya ya Gmail, automatically unapata email address nyingine ambayo inatumia domain ya googlemail.com. Kwahiyo, kama una akaunti mbili tu, unaweza kutumia ile ya gmail.com kwa akaunti ya kwanza na googlemail.com kwa akaunti ya pili.

Najua ulikuwa hujui, na sasa unajua... vipi tuendelee?
#virus
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom