Uzi Maalum Wa Kujadili Shule Mbali Mbali

Imefika wakati shule zetu ziweze ku inject technology facilities kwenye systems zetu za shule. Kila kitu ni teknolojia sikuizi ni wakati wa walimu kua na kompyuta kama kitendea kazi, shule lazima ziwe na computer rooms kwa wanafunzi kujifunza ni wakati wa walimu kutumia projectors (kwa madarasa yenye wanafunzi wengi) mambo ni mengi kwa kweli ila my worry ni kuhusu teknolojia zaidi mana tusipofanya sasa wenzetu huko duniani watatuacha mbali!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sisomeshi sina uchambuzi wa moja kwa moja. Ila nitaongelea elimu kwa ujumla wake.

Tanzania elimu yetu haiko sawa.

Tangu tupate Uhuru hatujawahi kua na sera ya elimu ambayo ilidumu, kuanzia Nyerere na UPE mpaka sasa Magufuli na Elimu Bure.
Ukifuatilia kila Rais alikuja na lake ilipokuja swala la elimu, kuanzia mitaala, vitabu vya kiada, walimu wa kufundisha, sasa hivi hadi muda wa kufunga na kufungua shule Rais anadictate.

Surprisingly hakuna sera ambayo iliridhisha kiasi atakayefuatia aone ngoja niendelee na hii. Kila anayekuja anafanya majaribio yake.

Watu wanaojipendekeza, waoga, wanaokaa kusubiri elimu iwakomboe ni matokeo ya hayo majaribio. Ni matokeo ya mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika lakini anafaulu kwenda kidato cha kwanza.

Kuna mwaka niliona kitabu cha kiada cha shule ya msingi inaonyesha sehemu za mwili na kazi zake. Kile kitabu kilionyesha kichwa halafu kazi yake ilikua ni kubeba mizigo.

Huyu mtoto tunataka aweje?
hahahahahah yani hapo mtoto anasomea kuwa kuli moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rebecca,

Kuwaza kwamba elimu ni lugha, hiyo desperation tu ni tatizo.

Kati ya tatizo letu kubwa ni kushindwa kuamua lugha ya kutumia kufundishia, hata kwenye sera ya elimu ya mwaka 2014 bado wameweka lugha zote mbili kama lugha za kufundishia, it doesn't make sense kwakweli.

Objectives za elimu (mtu kwenda shule) zipo 3
1. Astaarabike (5%)
2. Aongezeke ubunifu (80%)
3. elimu yenyewe ( 2+2=4) (15%)

Kumbuka mtu hutumia lugha kufikiria, ndo maana kila aina ya watu wanakosea grammar ya lugha nyingine, wanajaribu kuiweka kama ile ya lugha yao (direct translation ) yote ni kwa sababu walichotaka kusema/kuandika walikuwa wanakiwaza kwa lugha wanayoielewa zaidi ndo wanatafsiri kwenye hatua za mwisho.

Wengi wetu tunaelewa zaidi kiswahili, ila unafundishwa poultry kwa kiinglish mwisho wa siku wengi hawaelewi wanakariri, mwisho wa siku kwenye ubunifu hatu gain kitu chochote, aliyemaliza form6 na darasa la saba tofuati yao ni kuwa moja anajua log mwingine hajui, hawana tofauti kwenye kutatua changamoto zinazowazunguka.

Sina hakika na utafiti wake, lakini nina hakika zaidi ya 80% ya watanzania ni wasomi kwa ajili ya matumizi ya ndani, yani walimu, manesi, wakulima, mafundi, wafugaji. Je si muhimu kuongeza ubunifu kwenye hili kundi kubwa? wachache wanatoka nje au kufanyia kazi makampuni ya nje.

PIA, usifikiri ilikuwa kazi rahisi sana kufanya kiswahili kizungumzwe nchi nzima. Kubadilisha inawezekana, ila ujue ni mfumo wa maisha, lazima hiyo lugha nyingine izungumzwe kuanzia nyumbani hadi shuleni accross the country ndo tutaleta maana. Sasa tuko tayari kwa hilo?

Kama hatuko tayar kupoteza kiswahili chetu, basi tufundishwe kwa kiswahili tu, halafu Kiingereza kifundishwe kama lugha ya pili.

Itaendelea
mnhhh.hata hizo nchi nyingi sasa hivi wanatafuta walimu wa English,

watoto wakifundishwa kwa kingereza madarasa yote,nursery,primary,secondary na chuoni sidhani kama itakua tatizo…..

kisha kwenye ajira mtu kama kasomea vitu kwa Kiswahili,inam limit huyu mtu afanye kazi katika nchi zinazoongea Kiswahili tu...au makampuni ya Kiswahili tu...ila kwa Kingereza inapanua wigo,unaweza uka explore hata kazi nje ya nchi...as English ni standard language...

Mambo ya culture yaache Adrian,hata tufundishwe ki china,kiswahili hakiwezi kufutika...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza na kwa kuzingatia JF ni uwanja mpana unaojumlisha wazazi, wamiliki wa shule, maofisa wa elimu wenye wadhifa tofauti na pia kwa vile waalimu wamo humu basi tukutane kujadili uwanja mzima wa Shule za Nursery, Primary na Secondary Tanzania.

Tutakosoa mifumo mbali mbali ya elimu, ada ambazo wazazi wanahisi ni uonevu kwa vile hazikuwepo mwanzoni.... kudorora kwa elimu ama performance ya shule.... nidhamu za wanafunzi na hata waalimu wao... na kadhalika.

Karibuni wana JF....

Cc Mshana Jr Madame S Khantwe snowhite Mentor Asprin Daby cute b Relief Mirzska farkhina Dreka BAK Watu8 Castr Nyani Ngabu BAFA
chaliifrancisco espy Hornet Zamazamani
Rebeca 83 Lizzy afrodenzi Sky Eclat
kwahiyo hao ulio wa_tag ndio unaohisi ndio wadau pekee wa elimu au ndio unao hisi ni wasomi pekee humu ndani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wehu washaharibu mada wanafanya personal chats. Pathetic

Sent using my Nokia Torch
 
.
Screenshot_20190221-160008.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dahh!
Picha halisi ya shule nyingi za serikali na wananchi
Nijadili PAMBALU shule ya msingi,

shule yetu iko very smart, Iko MKOA WA MWANZA, SENGEREMA jirani na wilaya ya NYAMAGANA na MISUNGWI ambako stand maarufu ya NYEGEZI inapatikana.

inawanafunzi 3500 na usheheeee.

kila darasa wanakaa wanafunzi 180 na wote wanakaa kwenye dawati!! Dawati la watu wa tatu wao hukaa watano kama kwenye hice!

Shule inawaalimu 150 wanao fundisha vizuri kwa lugha ya kiswahili na kiingereza wakiwa na vitabu vya kutosha kwa masomo yote.


Shule yetu hii ina matundu ya vyoo 24 hali inayo sababisha wanafunzi wote 3500 na ushehe kujisaidia vizuri sana na vyoo kubaki visafi kiasi unaweza lia pilau ndani ya vyoo vile.

Hatuna swiming lessons, ila tuna mpira wa sembo (chandimu) kombolela na hata kadome

Hatuna school bus tuna magari yetu yaasili TZ11 (miguu yetu)

Watoto wetu ni wasafi sana, maana wana nguo pea moja wanayo vaa january mpaka disemba.

wengi huja na daftari mkononi, kidumu cha maji na fagio la chelewa la mkono!!

Shule yetu ina toa huduma ya maji ya bomba ambayo nisafi na salama kwa watoto wetu kunywa kipindi cha mapumziko.

Karibuni PAMBALU,

Nishule bora sana ambayo watoto wamefundishwa ABCD EFG HIJK ELOMENOPNQU,

Hawa ndio taifa bora la kesho,


karibuni sana PAMBALU

Kengele yetu ni chuma chakavu,

sisi watoto wetu huingia shuleni kuanzia saa moja mpaka saa nne za asubuhi na huondoka pale wanapo hisi njaa au wamechoka,

hii inathibitisha uhuru wa uhakika kwa wanafunzi wa pambalu!!


Si lazima mwanafunzi awe na proper uniform, huku pambalu hatakama una ndala suruali ya home, sketi ha kanisani unakaribishwa sana



Shule yetu ina wakuu wa shule 10, hawa ni :-

waziri wa elimu, mbunge wa jimbo, diwani wa kata, afisa mtendaji, mwenye kiti wa bodi, mkurugenzi wa halmashauri, mkuu wa mkoa, rasi mkoa, na wengineo.

hawa wote ni wakuu wa shule maana muda wowote wanatoa maamuzi kuhusiana na shule yetu popote walipo!!


PAMBALU wanafunzi wote HUFAULU, Na wooooooote hufaulu kwenda PAMBALU SECONDARY SCHOOL, ambako huko hufika wakiwa ni wataaalamu wa kuongea kiingereza na kusoma.

hivyo wote hufaulu kwa kiwango cha dv zero!!!

Wazazi wako komited sana, wakishaleta watoto january huonekana january ingine kuwaleta wengine kama wapo!!

Wazazi wahuku ni wazalendo sana, kwani watoto wao wanapo kaachini wakiambiwa kutafuta kiti cha mtoto wake, wao husema serikali itawaletea viti.

Inapendeza kwa kweli!!

Waalimu wetu huku hufundisha wajiskiavyo, ivyo wapo huru kwa kuwa wanamishahara mizuri na minono na ya kutosha kiasi cha wao kufungua biashara zingine waweze kukuza kipato!!



KARIBUNI PAMBALU SHULE BORA TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
me sitaki kuwa specific na shule moja, lakini ningependa kuwa general kwa shule zote za kata. Kulingana ma maana halisi ya elimu na kipimo cha kutahini watahiniwa kuwa ni mitihani, na kwa vile elimu yetu imekuwa ikapambanuliwa kwa mfumo wa serikali na shule binafsi huku pia serikali kukiwa na shule za mkoa, wilaya na shule za kata. Lakini pia hapohapo serikali inajipambanua kuwa na shule zake kongwe na shule za vipaji huku treatments na ruzuku zikitofautiana kati ya madaraja ya shule hizo. Basi ninapendekeza mitihani itungwe kulingana na nature ya mazingira na uhalisia wa maisha ya elimu inayotolewa kwa wanafunzi hao, haiwezekani mwanafunzi asiye na walimu wa kutosha, asiye na vitabu unampima sawa na mwanafunzi wa Marian, Mzumbe, St thomas feza n.k. Maon; mitihani itofautishwe kati ya shule za kata na shule zingize ili kuweza kuacess kile mwanafunzi amejifunza.
inaonekana ni shule nzuri. Ada zao zikoje?
 
Back
Top Bottom