Uzi maalum: Visa vilivyowahi kukutokea ukipata tiba kwa mganga wa kienyeji

Niliwahi kuchaniwa begi na wanafunzi wenzangu hostel,wakaniibia tsh 30000 na saa flan ya mkononi nilinunuaga elf 2 tu kariakoo....sasa kila ninae muuliza anakataa hajachukua..na hostel tunakaa wanne tu...lakin katika hao wanne mmoja wapo hakuenda chuo siku nzima...hivo hostel tulimuacha yeye...

Na wakati nagundua huo wizi yeye hakuwepo hostel na siku hiyo alichelewa san kurudi..sijui ndio alienda club...alvorudi tukamvamia na kumbananisha sana lakini akagoma

Basi tukashauriana kwenda kwa mganga asubuh...tukatoka nje tukatafuta ya mabango yao na kuchukua namba.akapokea mganga akatuelekeza ofis yake ilipo...tukamfwata...ilikuwa mitaa ya ubungo maziwa huko ndani ndani..
Kufika kule akatuambia tuandike majina yetu,tukaandka akaanza makalatee yake..amejufunika gubgubi anaongea ongea kichina sijui kile...baadaye akasema haya..chukua hii dawa ya kwanza nenda kaweke kwenye lile begi ambalo pesa zimepotea...asubuh mwizi wako jina lake litatokea kwenye hii karatasi..nikasema poa..
Hii ya pili ndio muhimu..hiyo asubuh utaenda kuoga nayo, yaan changanya kwenye maji ya kuoga kisha urudi hapa peke ako na hilo karatasi la majina ili uchague sasa tumuadhibu au arudishe mali yako,lakini leo inatakiwa ya mizimu tsh 25000.Nikasema poa.. Nikampa
Wakati tunatoka akasema kesho utavokuja uje elfu 30...kwa ajili ya kumaliza dawa nahakikisha unajuja peke yako...saa 4 asbuh...na sasa hiv msizungumze chochote mpka mfike njia panda.

Nikasema poa..sasa wakat tunaondoka kimoyoni nikawaza nimeibiwa 30000 na saa tu..lakini hapa kwa mganga itatumika kama 55000 hiv tena na nauli wote nilikuwa nalipa mm...
Dah nilijiona boya kweli...nikaitupa ile dawa na kalatasi mitaa ile ile nikasema kama majin yakimaind poa tu...skuenda tena..wala hiyo asubuh hmna lolote lilitokea...na hakuna alimuuliza mwenzake mpka leo...waganga ni nouma
 
Kuna miaka miaka ya 1997, niliibiwa baadhi ya vitu vyangu room,

Nikasikia Kuna mganga mmoja yeye huwa Kuna dawa anakupa unakunywa,then wezi wako unawaona kwenye kitu mfano Kama wa TV ya asili,

Basi bwana nikaenda kwa huyo mzee, kufika nikamkuta huyo babu wa kizigua,
Nikamuelezea, "akasema sawa shida yako imeisha mwanangu, akaniambia mwizi wako utamuona dhahiri hapa, lipia elfu nane, nikalipia, kipindi kile ilikuwa ni nyingi kiasi chake, maana sukari nakumbuka kilo moja ilikuwa inauzwa Tsh 200/= mkate mkubwa 100/= chai kikombe 20/=

Basi Kuna dawa ipo Kama ya mti imesagwa,akanipa nikainywa, then akanielekeza Kuna kachumba Kama kilinge niingie nikae ntashuhudia,
Basi bwana baada yakunywa hile dawa, muda kidogo nikaanza kuona Kama maruerue si marue, mbele Giza si Giza, ukutani naona Kama watu wanapita wanazomea,Wengine sijui wapo uchi, kichwa kikawa kinauma , nikawa Kama sizielewi elewi

Mzee akaniuliza vipi umeuona mwizi wako babu, haraka nikamjibu ndio nimemuona, 'nimemjibu hivyo hili tu nitoke kwenye hile dhahama, kwakweli ilikuwa Ni balaa hali niliyokuwa najisikia,Babu akaniuliza vip umemfahamu vizuri, nikamjibu haswaa, akaniambia Sasa nenda kamkabili umwambie akurudishie vitu vyako, akikaidi Rudi tumtie adabu, walahi sikurudi Tena kwa yule mzee,

Nakumbuka niliibiwa redio yangu ya mtumba model ya Haiwa ya CD moja, nilinunuaga Zanzibar kipindi hiko, na baadhi ya vitu
 
Kuna waarabu walitoka Oman wakiwa na na ramani ya kahama! Wakanitafuta niwap3l3ke kahama kwa mganga fulani ambaye sasa ni marehemu.

Safari ilianza na balaa sababu tulipata seat zile za mwisho kabisa, bus najimunisa, kama mnakumbuka kuna kipande cha dodoma kilikuwa na vumbi tena kipande kirefu, basi tulipofika gairo wanauliza bado? Nikawaambia kahama tunafika kesho na tunatembea usiku na mchana wakachoka..kipindi hicho kahama mnaingia asubuhi, chombo ikifika nzega inalala.

Kufika kahama

Kahama pale tulifikia kwa mwenyeji wetu ambaye alikuwa ana hostel kabisa, yaan kama ana shule, kuna paka weusi zaidi ya 100 wateja si chini ya 50 wanakaa hapo hapo wanahudumiwa mpaka wakipata nafuu na pia ana hostel zingine nje ya mji, kifupi jamaa alijipanga

Aisee nilipapenda kwa yule jamaa maana asubui anachinja kuku20, utakunywa supu, kuku rost, kuku ya kuchoma na za kukaanga, sasa sijajua ilikuwa ni nili ya wale waarabu ama laa,

Tiba ikaanza wakawa asubuhi wanatibiwa na jioni, ila kuoga wanatakiwa wakaogee mlimani kule kuna viwanda vya pamba kule juu, ikawa hivyo , hapo mm nafanya utalii wa ndani tu maana nishavuta fungu langu tangu nikiwa dar, nakumbuka walinipatia laki 9 .2007 laki 9 si haba..kila kitu juu yao kwenye safari.

Sasa kuna siku yule mwarabu ( alikuwa ni meneja kwenye visima vya mafuta huko kwao sasa kilichomleta huku ni kwamba kuna mzungu kaletwa kuziba nafasi yake, yaani yeye anashushwa cheo anakuwa chini ya mzungu, mwarabu hilo jambo hakutaka hata kulisikia akafikia uamuzi wa kuja Africa kuroga, kaja na location kabisa anataka apelekwe kahama kwa (fulani)

Sasa wakati ameshatoka kuoga kule juu ya mlima ( hiyo siku alitakiwa aoge saa 4 asubui ) tunarudi kwa mtaalam kwa bahati mbaya sijui ama bahati nzuri mi sielewi lakini yule mjuba aligusa upupu ule uko kama ukwaju hivi, basi ulimuwasha sana mpaka ngozi ikawa nyekundu, akaniuliza hii ni nini? Nikamwambia huu ni upupu! Upupu ndio nini nikamwambia upupu ni upupu tu na kazi yake ni kama hiyo unayoiona. Ajabu akasema tafuta watu wanichumie hii kitu, itanifaa na dawa basi siogi tena na kama tunaweza kupata ndege inayoenda dar leo hii fanya taratibu tuondoke leo hii hii hii upupu itanifaa sana.

Badi tukarudi mpaka kwa mtaalam tukamwelekeza, jamaa ana connection vibaya mno, wakafanya booking, ya ndege ya kesho yake hawakutaka tena bus maana walifika kahama na vidonda mikononi.

Mimi sikuwa na mzuka na ndege, nikawaambia ppesa yangu ya tiketi nipeni mm nitarudi na bus, tukaachana hivyo,

Yule mwarabu sasa baada ya kufika huko kwao alichokifanya anakijua mwenyewe, kwa maelezo yake, likizo ilipoisha maaana alikuwa na likizo ya wiki2, aliwahi ofisini mapema sana akausambaza ule upupu ofisi nzima asema na mwingine akaweka kwenye AC! Akasepa akaenda kufanya mishe zingine,

Mzungu alipoingia ofisini, akawasha Ac akawa anakung'uta mafile mara kagusa huku mara kule, kilichomkuta yule mzungu anajua mwenyewe. Anasema alianza kuwashwa alipiga kelele akawa kama ana kichaa na kule ni jangwani, ikabidi ifanyike jitihada ya kumfunga kamba kumtia ndani ya ndege ya kumpeleka mjini, na hata alipofikishwa hospital na kupata matibabu alikataa kufanya kazi Oman kabisa, ikabidi mwarabu arudishwe kwenye ofisi yake..

Upupu ndio uliomsaidia na si tiba ya yule gagula.
Huko kahama niliskia hata mimi kuna jamaa alikuwa anajiita Shetani, huyo jamaa naskia ni balaa.

Alikuwa anasema kabisa najua nikifa naenda kuchomwa moto ila kwa hapa duniani lazima niwe kiboko.

Jamaa kama unashida yoyote alikuwa anaweza kutibu.
 
Me jamaa yangu ndo aliniadisia alipewa dawa ila sharti lilikuwa rahisi kwa akili za kibinadamu kwamba ahakikishe hakojoi ikiwa mfukoni japo unatakiwa kila uendapo iwe mfukoni, Yaani ukihisi haja make sure unaitoa kwanza pembeni ndipo ujisaidie, Jamaa ndani ya week tuu akachana mkeka.
 
Kuna miaka miaka ya 1997, niliibiwa baadhi ya vitu vyangu room,

Nikasikia Kuna mganga mmoja yeye huwa Kuna dawa anakupa unakunywa,then wezi wako unawaona kwenye kitu mfano Kama wa TV ya asili,

Basi bwana nikaenda kwa huyo mzee, kufika nikamkuta huyo babu wa kizigua,
Nikamuelezea, "akasema sawa shida yako imeisha mwanangu, akaniambia mwizi wako utamuona dhahiri hapa, lipia elfu nane, nikalipia, kipindi kile ilikuwa ni nyingi kiasi chake, maana sukari nakumbuka kilo moja ilikuwa inauzwa Tsh 200/= mkate mkubwa 100/= chai kikombe 20/=

Basi Kuna dawa ipo Kama ya mti imesagwa,akanipa nikainywa, then akanielekeza Kuna kachumba Kama kilinge niingie nikae ntashuhudia,
Basi bwana baada yakunywa hile dawa, muda kidogo nikaanza kuona Kama maruerue si marue, mbele Giza si Giza, ukutani naona Kama watu wanapita wanazomea,Wengine sijui wapo uchi, kichwa kikawa kinauma , nikawa Kama sizielewi elewi

Mzee akaniuliza vipi umeuona mwizi wako babu, haraka nikamjibu ndio nimemuona, 'nimemjibu hivyo hili tu nitoke kwenye hile dhahama, kwakweli ilikuwa Ni balaa hali niliyokuwa najisikia,Babu akaniuliza vip umemfahamu vizuri, nikamjibu haswaa, akaniambia Sasa nenda kamkabili umwambie akurudishie vitu vyako, akikaidi Rudi tumtie adabu, walahi sikurudi Tena kwa yule mzee,

Nakumbuka niliibiwa redio yangu ya mtumba model ya Haiwa ya CD moja, nilinunuaga Zanzibar kipindi hiko, na baadhi ya vitu
Huyo wa kuona Mbaya wako kwenye kitu kama TV hata Magomeni huku alikuwepo.
 
Back
Top Bottom