Uzi maalum nchi ya kijani (CCM): tuangalie mafanikio yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana bila kuwepo kwa wapinzani

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Hapa tutaangalia mafanikio yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana bila kuwepo kwa wapinzani.

Sasa hivi serikali za vijiji na mitaa ni CCM vipi hapo ulipo nini kimeongezeka? Je, hakuna dhuluma na ufisadi? Vipi miundombinu kama ulaya au ulaya inakaribia (wapinzani walituchelewesha)

Halmashauri zote ni CCM, ufisadi si hakuna kabisa, ukusanyaji kodi, ujenzi wa miundo mbinu, hospitali, maji kila mtaa, majengo ya shule, ukienda huko sasa hivi asikwambie mtu maisha kama ulaya, CAG bwana anasema maniapaa ya Kinondoni ufisadi wa kutosha, nadhani hii manispaa ni Chadema na CUF. Hivi bado kuna Halmashauri ya CCM inapata hati chafu (wapinzani walituchelewesha sana)

Bungeni nako ni kijani, sasa hivi mashirika ya umma, huko wizarani ni kusafi, wabunge wanasimamia serikali kikamilifu, miradi inasonga mbele kama ulaya. Hakuna ufisadi, wabunge wa CCM wanafichua mafisadi huko bungeni na kuwaajibisha viongozi wa serikali.

Sasa hivi matumizi ya serikali na usimamizi wake hakuna mashaka, ila CAG anatuonea sisi nchi ya kijani (wapinzani walituchelewesha)

Vipi hapo ulipo nchi ya kijani vipi wapinzani waliwachelewesha eneo gani? Na sasa mko sawa au pametatuliwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom