Bhikalamba
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 1,698
- 2,346
Kwanza kabisa napenda nikupongeze kwa juhudi zako za kutatua migogoro ya ardhi nchini.
Pamoja na pongezi hizo, naomba utilie mkazo suala la upimaji ardhi kwa nchi nzima, na udhibiti wa makazi holela. Niseme tu wazi kuwa ujenzi holela na mpangilio mbovu wa makazi katika miji yote nchini ni uzembe, kutopewa kipaumbele na utendaji ulio zorota wa idara ya Ardhi.
Katika halimashauri nyingi nilizotembelea, suala la upimaji ardhi, liko chini; ukiuliza wanasema hakuna fedha za kulipa fidia wananchi ili halimashauri ipate kumiliki eneo, kupima viwanja na kuviuza. Na hapo ndipo naliona tatizo lilipo; kimsingi hapo ndipo tulipokwamia.
Hakika tukienda kwa mkitadha huu itakuwa vigumu sana kupata fedha za kutosha kulipa wananchi fidia ya ardhi , kisha halimashauri au mamlaka za miji kuyachukua maeneo husika na kuyapima ili wauze viwanja.
Ushauri wangu, idara za ardhi kila wilaya au halimashauri waje na master plan, wapime ardhi na watoe title deeds kwa wenye maeneo husika. Ikiwa MTU akitaka kujenga tayari mipaka inakuwepo wazi kuonyesha eneo la barabara, na mipaka ya kiwanja chake. Pia akitaka kuuza, mnunuzi atanunua eneo lililokwisha pimwa na process ya kubadilisha title deed inafanyika.
Kuna halimashauri zingine idara ya ardhi wapo tu kwa ajili ya kuripoti kazini asubuhi na kurudi nyumbani jioni, hakuna kazi pale ofisini. Hakuna upimaji ardhi, ukienda ofisi ya ardhi unataka kununua kiwanja, wanakwambia hawana labda ukanunue kwa watu binafsi, lakini pia huko hupati viwanja vilivyo pimwa au kuwa na hati. Mwenye eneo atakupigia hatua kadhaa kulingana na makubaliano, mtaandikishana kwa mtendaji tu kazi imeisha. Matokeo yake ni ujenzi holela.
Rafiki yangu alinunua ardhi Mbulu mjini, baada ya kujenga MTU mwingine akaja kunua pembeni yake, wengine wakafuata kumzunguka. Sasa ikawa ni shida namna ya kuingia na gari nyumbani kwake baada ya hao majirani zake kujenga. Na huo ni mfano mmoja tu kwa kadhia hii inayotokea katika miji karibu yote inayoendelea kusitawi nchini.
Hainiingii akilini pale idara ya ardhi wanapokaa tu ofisini, huku wakipokea mishahara kila mwezi halafu kupima ardhi inasubiriwa eti fungu kutoka serikalini. Kwani, ni lazima halimashauri ipime na kujimilikisha? Kwanini wasipime tu na kutoa hati kwa wenye maeneo, wao wakabaki kukusanya maduhuri yatokanayo na kodi ya ardhi? Na hii itaongeza mapato kwa halimashauri na serikali kwa ujumla.
Ikiwa halimashauri inao maafisa na watendaji wa ardhi wanaolipwa mshahara kila mwezi, si haya ndo majukumu yao!!? Je, suala la kupima ardhi linahitaji tena fungu lingine kutoka serikalini? Nadhani hii mentality inatakiwa kuondolewa, na watu wawe wabunifu na wachapa kazi.
Zaidi, naona msisitizo wa upimaji ardhi na mpango wa makazi rasmi umewekwa zaidi mijini lakini tuelewe pia baadhi ya vijiji ndo miji ya kesho. Kwahiyo hili lifanyike kote mijini na vijijini nchi nzima, ardhi ipimwe na makazi yapangwe vizuri.
Hii itasaidia kuondoa foleni na mafuriko katika baadhi ya miji yetu mikubwa. Badala ya kutumia gharama kubwa kujenga flyovers, tungeweza kupanga vyema makazi, tukawa na barabara nyingi za mitaa kila kona, tungepunguza traffic jams kwenye highways.