Uzi maalum kwa watu wanaohitaji kuagiza magari, ama wenye malengo ya kuagiza magari

Prodigy Oligarchy

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
571
643
Habari Jf,

Uzi huu, utakua ni uzi maalum kwa watu wanaohitaji kuagiza magari, ama wenye malengo ya kuagiza magari bila kujali sasa au baadae.

Hapa, ninakaribisha maswali yatakayo husika na

(i). Gharama za uagizaji (manunuzi) ya gari

(ii). Gharama za ushuru (Tra) bandarini, n.k

Kwa kifupi mchanganuo mzima wa gharama zote utakazo takiwa gharamia mpaka gari lako kuwa mikononi mwako.

Nimeweka huu uzi, baada ya kuona threads ni nyingi zenye maudhui ya maswali yanayohusiana na ushuru n.k.

Nawasilisha.

Kazi iendelee
 
Gari mpya kabisa aina ya vitz itagharim kiasi gani? Na gharama za vx v8 ni kiasi gani toka kununua hadiinifikie.
 
Gharama zipoje kwa Toyota vanguard na Rav>2014(Disel engine)
Ahsante.
 
Hello,

Hizi buses, taratibu zake ni tofauti kidogo, maana ni units ambazo hua zinaundwa kwa order.

Lakini bei yake ni 390mil hii ni mpaka mikononi, ila bima inakua hakuna.
Nashukuru mkuu,nilidhani uko na bei nafuu kidogo kumbe hakuna tofauti
 
Nashukuru mkuu,nilidhani uko na bei nafuu kidogo kumbe hakuna tofauti
Anytime kaka,

Ila ningependa kukukumbusha kwamba, hapa sipo kwaajili ya kuuza, ila kusaidia kutoa michanganuo

(rejea lengo na ufafanuzi wa uzi huu)
 
Kuna hii gari nimeipenda nataka kuagiza nimekuja kwenu nataka kujua je ni kiasi gani kinahitajika mpka gari kunifikia ukijumisha Kodi na gharama nyngne.
Bei yake ni $19200
 
Kuna jamaa yangu anatamfuta mtu amuuzie ist,ameiagiza from japan imefika bandarini pesa ya kugombolea ni kama 6m,yeye ameiagiza kwa kama 5m!
Anatafuta mtu amrudishie hiyo 5m then yeye achukue hiyo ist mpya
Namba zake ni 0736770052
 
Kuna hii gari nimeipenda nataka kuagiza nimekuja kwenu nataka kujua je ni kiasi gani kinahitajika mpka gari kunifikia ukijumisha Kodi na gharama nyngne.
Bei yake ni $19200
Please , ingekua vizuri kama utatupatia details kamili za gari tuweze kukupatia mchanganuo mzima.

Aina ya gari (Make & Model)
Mwaka
Ukubwa wa engine n.k
 
Habari Jf,

Uzi huu, utakua ni uzi maalum kwa watu wanaohitaji kuagiza magari, ama wenye malengo ya kuagiza magari bila kujali sasa au baadae.

Hapa, ninakaribisha maswali yatakayo husika na

(i). Gharama za uagizaji (manunuzi) ya gari

(ii). Gharama za ushuru (Tra) bandarini, n.k

Kwa kifupi mchanganuo mzima wa gharama zote utakazo takiwa gharamia mpaka gari lako kuwa mikononi mwako.

Nimeweka huu uzi, baada ya kuona threads ni nyingi zenye maudhui ya maswali yanayohusiana na ushuru n.k.

Nawasilisha.

Kazi iendelee
Hello ndugu, nakushukuru kwa kuja na uzi huu mana kuna wengi tunataman kuagiza gar toka nje lakin utaratibu na hasa zaid mchanganuo wa gharama had gar inakufkia imekuwa changamoto xanaaa..... Pia ningetaman kujua kwann gharama za TRA huwa kubwa kias cha sawa au zaid ya bei ya gari uliloagiza?!?

Sasa kwa upande wng nataman kuagiza gari aina ya Noah old model SR40.... Kwaajil ya familia.....naomba maelekezo na mchanganui kwa ujumla.......

Asante ndugu.... Nawasilisha kwako.....
 
Ahsante kushukuru.

kuhusiana na kwanini TRA hua wanatoza kiasi ambacho huonekana kama ni sawa ama zaidi na bei ya kununulia gari yenyewe. Kwa majibu ya kina kabisa, nadhani wao (TRA) Ndio wanaweza kuyatoa na kwa ufafanuzi mkubwa zaidi.

Kuhusiana na Noah,

naomba nikupe mfano halisi wenye michanganuo.

(kwenye link hiyo hapo juu, ni toyota Noah SR40 )

Bei ya manunuzi hadi kuifikisha bandari ya Dar es salaam ni $4,4497 (TZS 10,792,800 )

Ushuru wake ni TZS 6,553,000/=

(https://gateway.tra.go.tz/umvvs/Umvvc_result)

Ambapo itakuja jumla ya TZS 17,345,800/=

Unapaswa kuwa na TZS 800,000/=

ambayo ita-cover

- Port Charges
  • Shipping Line
  • : Walfage
  • Agent Fee (gharama za agant wako atakae kutolea gari lako bandarini)
n.k

ambapo jumla itakua 18,145,800/=

usisahau kuhusiana na bima utahitajika gari yako kuikatia bima.

comprehensive watakutoza TZS 750,000/=

Jumla kuu TZS 18,895,800/= Hadi barabarani /mikononi mwako

bei sawa na ALPHARD
 
Back
Top Bottom