Uchaguzi 2020 Uzi maalum kwa watia nia ubunge unaowahisi jimboni kwako

CCM MKAMBARANI

JF-Expert Member
Mar 15, 2017
1,339
933
Ndugu wana jukwaa Kama ilivyoada nawasalimu. Kwa salamu ya wajamaa watanzania sisi.Uzi huu utakuwa maalumu kwa ajili ya kuwatambua watu ambao wameanza kupitapita majimboni mwetu kwa ajili ya kuelekea 2020.

Uzi huu utakuwa hai hadi itakapofika 2020 na tutafanya tathmini kubaini kuwa je,ni kweli hisia zetu zilikuwa vizuri,kwa sababu hili ni jukwaa la watu wenye fikra kubwa napenda kuanza na hawa wafuatao ambao mimi binafsi kwa majimbo niliyotembelea kuwasalimu ndugu zangu niliona na kufanya utafiti kidogo.

1. Morogoro kusini Mashariki- Fabian Peter (chama bado lkn anaonekana ni mwana-ccm)-Mbunge wa sasa ni Omary Mgumba.-CCM .Kupitia CHADEMA ni David Lugakingira

2. Shinyanga Mjini- Patrobas Katambi _CCM.Mbunge wa sasa ni Mh.Masele

3. Nyamagana CHADEMA (HEZEKIA WENJE) ccm ni Mbunge aliyepo sasa Anjelina Mabula

4. Musoma Mjini CCM (diwani wa kata ya kamunyonge) na (Dr.Eliud Esecko) kw upande wa upinzani ni Vincent Nyerere

5........................................................

6.............................................................

Kwa nadharia ya Mwanazuoni Vilfredo Pareto (The Circulation theory of elites) ni kwamba wakati ukifika waweka nia hawa tunaowahisi muda ukifika watatangaza na ikitokea wakashinda kwa kura za uungwaji mkono na wengi itakuwa vizuri na waungwe mkono.

Wanajukwaa karibuni Tujadili viongozi wetu wa kesho je watatufaa au wanatafuta pa kutuibia kama wengine?.


MJADALA UMEFUNGULIWA.
 
Said Mgumba ni was Morogoro kusini. Morogoro kusini Mashariki Prosper Joseph Mbena. Masahihisho tu
 
Back
Top Bottom