Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Tangu nihitimu nimekuwa mtu wa kujitolea pasipo kupewa hata sumuni ila Mungu kanishika mkono na sasa nimeanzisha mradi wangu wa kuuza dagaa wabichi kutoka bukoba.

Ni mwezi mmoja tangu nianze kazi hii ila ugeni katika biashara siwezi sema ni biashara mbaya kimasilahi ila inalipa, Nipo Arusha kwa yeyote atakayetaka dagaa nitamletea popote ndani ya Jiji la Arusha na maeneo jirani.....Dagaa ni wazuri sana Hawana mchanga......


Kwa biashara nitafute kwa namba hii....0692405717.....

Tusisubiri ajira..... Kidogo huleta kikubwa
c5150c1e2120f42a7db80011edf01bd0.jpg
32ce772bb33ee4c64023c0dc30d0f08a.jpg
0b3015822a336c61dd5602a236859e23.jpg
Usife moyo
 
Heshima kwenu viongozi

Nimeona ni vyema na sisi wenye lengo la kuacha kazi tukawa na uzi wetu kama wenye agenda nyingine walivyoanzisha uwanja wao.

Lengo la nyuzi hii ni kupeana mawazo, moyo na uzoefu wa mbinu bora tunazotumia katika maandalizi yetu ya kuachana na aina Mpya ya utumwa, yaani KUAJIRIWA.

Lengo lingine la uzi huu ni kuonesha sababu ya uamuzi wa kutaka kuacha kazi ili kila mtu apime kama sababu yake ni sababu tosha ya kufanya hivyo ama la, lakini hii pia inatoa fursa kwa wachangiaji wengine kufanya assessment ya maamuzi hayo.

Kuacha kazi na kujiajiri na pengine baadae kufikia hatua ya kuajiri ni uamuzi wa kuyatoa maisha yako mikononi mwa mtu mwingine (muajiri) na kuyakabidhi mikononi mwako mwenyewe. Ni kujitoa katika kutawaliwa na kuamua kujitawala mwenyewe. Ni vyema pia tukajulishana gharama za maamuzi hayo mazito ya kutoka Misri kuelekea Kanani. NI WAZI HAITAKUWA SAFARI NYEPESI.

Tushauriane time scale, mfano mimi ninakimbizana na miaka Mitatu kabla sijatoka kwenye hii Jela. Baada ya hapo ntarudi uraiani, nyumbani kuishi maisha yangu ya uhuru.

Tunaotaka tutoke hii Jela Tushauriane humu, je tukusanye mtaji sasa bila kufanya ujasiriamali na tutakapoacha tu kazi ndio tuanze rasmi ujasiriamali? Ama tuanze sasa hivi kufanya kazi na ujasiriamali ili tu-taste ladha ya ujasiriamali kabla hatujaacha kazi? (Ila hata mambo yakiwa magumu kwenye ujasiriamali kipindi tupo kazini na tunafanya ujasiriamali, kuendelea na kazi sio option). Kubaki Jela haiwezi kuwa option kisa kuna dona na maharage ya bure, bora kuwa uraiani ule mlo mmoja wa maharage na ugali kwa mwaka mmoja ili uje kula asali na maziwa kwa miaka mingi ijayo.

Kila mtu anaweza kuwa na sababu yake ya kuacha kazi. Wengine watakwambia kazini kipato kidogo, lakini amini nakwambia hata ukiajiri na kutoweka mwili, moyo na roho yako kwenye hiyo kazi, unaweza kupata kipato kidogo kuliko hata kile cha kazini. Katika swala la kipato, tofauti ya kipato cha kuajiriwa na kujiajiri ni kipato kimoja Anapanga mtu akulipe kiasi gani, na Kingine Unapanga wewe uingize kiasi gani.

Wengine watakwambia, wanataka waache kazi sababu ya Mateso kazini,ubabe wa mwajiri, kutojali kwa mwajiri. Yote hayo yanakupa HASIRA, geuza hasira zako kuwa DRIVES, zigeuze kuwa USONGO.

Kwanini nataka niache kazi, nataka kuwa huru, nataka kusafiri huku na kule bila kujali bosi atahesabu siku tatu sipo kazini anifute kazi. Sitaki kumpigia mtu mmoja Magoti (bosi) ili kipato changu kiendelea kutiririka. Bora nipigie magoti watu wengi (wateja) ili kipato kiingie, kwani mteja mmoja akiamua kunifukuza kazi ntakuwa na option kwa mteja mwingine.

Uzi wetu TUNAOPANGA KUACHA KAZI, the clock is clicking....LET'S DO IT, LET'S GO.... Tunapenda pia kuchota busara za wale walioacha kazi na wapo wanaendelea kupambana.
 
BUSARA ZANGU,

Mtaani kugumu...... Haya ndio Majibu ya walio wengi kwenye ushauri wa kuacha kazi, Kama unataka kuacha acha usiombe ushauri, Nakuomba ufanye kautafiti. Tafuta watu kama kumi ambao wako mtaani na unawaamini, waombe ushauri.

Kama wakitokea wawili wakakubaliana na wazo lako njoo nidai vocha ya 500(joke)

Kimsingi haya maamuzi yanategemea tu utashi wako, Unapokua na Biashara huku bado uko kwenye ajira watumishi huwa wanakupiga sana, mwisho wa siku biashara inakufa na ndoto yako ya kuacha kazi inakufa

Mimi nakushauri anagalia mfuko wako na uwe na uhakika wa biashara ambayo unataka kufanya, Kumbuka challenges hazipo maofisini peke yake hata kwenye biashara pia kuna challenges.

Biashara ambayo unaweza kuanza nayo kama bado hujabuni biashara jaribu kuangalia Mazao, Mazao hayana hasara jaribu ku avoid perishable things kama viazi na mboga mboga.

Mazao kama mahindi yakiharibika utauzia wanaotengeneza byakula vya kuku.

suala kubwa ni mfuko wako na utayari wako wa kuishi kigumu.
 
Great, nilishaacha kazi ya Ualimu mara mbili, nikarudi kwa kazi nyingine ila pia roho yangu inaniambia kuwa ni Lazima niache kazi ili niwe na kitu ambacho ni lasting.... kazi zina muda, kazi za watu zinazeesha, zinaleta magonjwa ya stress na kukuminya sana kufikiria nje ya box. Nashukuru kwamba nakarinia kuvuka daraja hili, sitarudi nyuma this time MUNGU anisaidie. Kuna kitabu nakisoma kipo kwenye Playstore kinaitwa THINK AND GROW RICH aaaghhhh kinanitia nguvu sana, I encourage you guys mkisome pia.

Hivi vitabu vipo vingi na vya bure
Lazima tubadilike, lazima tubadilishe our Life style, inawezakana lakini ni lazima tujikane kwanza, lazima tujishushe, lazima tuwe commited.

Thank you
 
dedication kwenu;
retire young, retire rich by R.Kiyosaki...
ni miongoni mwa maamuzi magumu ambayo ni sahihi.
ni kosa kuacha kazi ujiajiri akilini mwako ukiwa na wazo mambo yakigoma nitarudi kuajiliwa.
unaweza kuja kuaibika. Hiyo mission ni kama movie ya The Hardway The only way, makomando wanatua na ndege iliyowaleta inalipuliwa kuwadhihirishia hawana option zaidi ya kushinda pambano msituni maana hakuna usafiri wa kuwarudisha.

ukifanya maamuzi hayo mapema, utapata faida ya Muda mrefu ila lazima upitie bonde la uvuli wa mauti ili kukuandaa kukabiliana na kupata na kukosa maishani. bonde hilo huwarudisha wengi kwenye ajira wakiogopa gharama ya kujiajiri.
 
Back
Top Bottom