Uzi Maalum kwa wanachama, wapenzi na makamanda CHADEMA

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
IMG_20171127_101305.JPG




Tusipopaza sauti sasa, tutabaki na wabunge 2 mwaka 2020,kulialia tumechoka tuchukue hatua.

Hapana shaka kabisa kuwa CHADEMA ni chama kilichojengwa katika misingi ya umoja, nidhamu na mshikamano wa hali ya juu baina ya viongozi,wanachama na wapenzi wa chama na wakijiita makamanda na hivyo kuakisi misingi imara ya chama iliyojengwa mithili ya jeshi imara lisiloteteleka.

Kwa upande mwingine hii imekuwa ndio ngao thabiti ya chama kuweza kuhimili mikikimikiki ya wapinzani wetu kisiasa CCM, ambao wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali za siri na bayana kutaka kukiua chama.

Pamoja na uimara wa chama,lakini kutokana na mabadiliko ya mbinu za CCM katika jitihada zake za kukifuta CHADEMA katika siasa za Tanzania, hatuna budi sasa kuchukua hatua za makusudi kubadilisha mwelekeo ili kumchanganya mpinzani wetu ambae kwa sasa ameamua kukiteketeza chama kwa kutumia mihimili na nguvu za dola bila aibu.

Hatua zifuatazo ni chungu lakini ni lazima zichukuliwe.

Nidhamu:
Sina shaka na uwepo wa nidhamu na utii wa hali ya juu miongoni mwa makamanda wote kuanzia juu hadi chini, lakini wakati umefika sasa tofauti na huko nyuma ambapo makamanda huku chini tulikuwa tukipokea maelekezo na maamuzi toka juu na kazi yetu kutetea na kutekeleza lakini sasa viongozi wetu lazima wakubali ushauri toka chini.

Mwelekeo: Kumekuwa na juhudi kubwa za kutaka kubadiri mwelekeo wa siasa za kimkakati na uanahalakati kuja kwenye siasa za mlengo wa kati wa maridhiano,hili ndio kosa letu kubwa na ndio litakuwa kaburi letu, siasa za uanaharakati ndio siri ya CDM kupendwa na kundi kubwa la vijana na kuchukiwa kwa mpinzani wetu,kwa kawaida uanaharakati hujengwa katika hoja na ndio siri ya kukubarika kwa CDM.

Kwa kinachoonekana kutokana na vitisho toka upande wa pili uwanaharakati mmemwachia Lisu na ndio maana ameshambuliwa binafsi na sio chama kwa kuamini kuwa akiondoka yeye kazi itakuwa imeisha kwa kuwa mliobaki mmesoftishwa, ukiacha Lema anajitahidi, wako wapi wanaharakati wetu Mwalimu, Mnyika, Halima na wengine wote mbona kimya?

Kimya chenu ni kujijengea mazingira ya kuondoshwa! mfano uchaguzi wa madiwani kata 43 iwe kama rejea, tayari kuna watu wanaamini wanaweza kuwafanyia lolote na hamna la kufanya, na huku chini tunazidi kukata tamaa,matarajio yenu ni nini?

Wanaowaonea wanapandishwa vyeo mbele yenu hamjui kuwa hii ni mbinu ya kuvunja mori kwa wafuasi wenu,na pia kuhamasisha watendaji wavunje sheria bila kujari kila palipo na masilahi ya CDM na huku wakitarajia zawadi! kama hamtachukua hatua hamtabaki mmezingirwa kama kuna kipindi kinahitaji uanaharakati ni sasa.

Sheria; Huenda mnaogopa mahakama haitawasikiliza,sio kweli pelekeni kero wazikatae taifa litanena kwa niaba yetu,mwanaume hufia vitani,sio ufie ndani harafu udai hata kama ningeenda vitani ningeuwawa,ipo tofauti aliefia vitani kapunguza adui.

Tafadharini pelekeni kesi zetu zote mahakamani zinazohusu uvunjaji wa katiba na sheria,miiko ya viongozi, siku hizi mpaka makatibu wakuu wanapewa kadi za chama cha siasa mko kimya? Wakurugenzi wa halimashari makada napo mko kimya,kama mtaingilia uteuzi wa raisi basi pelekeni mswada haraka bungeni ipeni tume uwezo kuajiri watumishi wake!

Watu ambao watakuwa wanawajibika kwa tume sio raisi,kuna kesi ya wananchi Mtikila alituachia ushindi MGOMBEA BINAFSI mbona hamfuatilii sheria irekebishwe au na nyinyi mna mawazo kama ya CCM kuwa itadhoofisha chama? Kama ndio hivyo mmekosea sana. Haraka sana badirisheni utaratibu wa kumpata mgombea urais,tengenezeni utaratibu makini ambapo maoni ya wananchi na wanachama yatazingatiwa, sio lazima utaratibu ufanane na wa CCM Ila maoni yetu ni muhimu tusirudie tena kuteua mgombea.

Vyombo vya habari, Kwa kipindi chote Bunge na vyomba vya habari binafsi ndio vilikuwa nyenzo ya CDM kujieneza,hakuna asiye jua vitisho vimeshafanya kazi yake,uenezi uko matatani mpinzani wenu hataki msikike jibu ys hili anzisheni vyombo vya chama Magazeti na Radio tv mtandao kwa kuanzia, utakapofika uchaguzi vitisho vitazidi hakuna chombo binafsi kitakuwa na uthubutu kwani ukiijua tabia ya adui jiandae kumkabiri.

Kama hamtachukua hatua sasa Wabunge,Madiwani mliopo sasa jiandaeni kuondoka 2020 maana hamtakuwa na wakuwasaidia, amkeni sasa ili tuwasaidie wakati ni huu hamjachelewa sana.

Uchaguzi wa jana uwe fundisho kwenu,huu ni ushauri wangu ni matarajio yangu kuwa na wengine watatoa ushauri kwa ajiri ya kujenga na sio kubomoa karibuni.
This is the right time let us push for the right changes.

Thanks
 
Makamanda hapa kuna haja ya kujitoa kafara.

Ingieni barabarani andamaneni.

Mkikaa kimya maCCM wanawaona nyie maboya ndo mana wanaendelea. ACHENI UOGA.

Ingieni barabarani MPIGWE RISASI na mapolisi mfe kama 1,500 hivi. na wengine wapelekwe ICC.

Baada ya hapo mtaenda sawa na CCM.

Otherwise endeleeni kusubiria embe chini ya m'buyu.
 
Makamanda hapa kuna haja ya kujitoa kafara.

Ingieni barabarani andamaneni.

Mkikaa kimya maCCM wanawaona nyie maboya ndo mana wanaendelea. ACHENI UOGA.

Ingieni barabarani MPIGWE RISASI na mapolisi mfe kama 1,500 hivi. na wengine wapelekwe ICC.

Baada ya hapo mtaenda sawa na CCM.

Otherwise endeleeni kusubiria embe chini ya m'buyu.
Mku haya nayaona Mpinzani kuapishiwa nchi jirani na huku nyumbani hayo yakaendelea kwani mambo yanakoelekea siko kabisa ni Mungu atunusuru na mabaya
 
Makamanda hapa kuna haja ya kujitoa kafara.

Ingieni barabarani andamaneni.

Mkikaa kimya maCCM wanawaona nyie maboya ndo mana wanaendelea. ACHENI UOGA.

Ingieni barabarani MPIGWE RISASI na mapolisi mfe kama 1,500 hivi. na wengine wapelekwe ICC.

Baada ya hapo mtaenda sawa na CCM.

Otherwise endeleeni kusubiria embe chini ya m'buyu.
Aliekuambia suala hili linamalizwa kwa maandamano nani?
 
Njia pekee iliyosalia ni kutoshiriki uchaguzi wowote. Ikitokea uchaguzi ukasusiwa na upinzani ukawa ni wa ccm pekee hapo ndiyo mchakato wa time guru na katiba mpya utawezekana lkn hii habari ya kulalamika harafu tunarudi ulingoni ni ujinga 2020 tukijitahidi tutakuwa na wabunge 2 tu.
 
Back
Top Bottom