Uzi Maalum kwa ajili ya BANK TELLERS/CASHIERS!

Uchunjuba Punjubi

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
799
619
Huu ni Uzi maalumu kwa ajili ya watu waliowahi au wanaofanya kazi kama Bank Teller au Cashiers katika mabenki mbali mbali. Tuweze kupeana vituko, uzoefu au changamoto ...n.k katika kazi hii ambayo inataka umakini sana, pia tuutumie Uzi huu kwa ajili ya kuwaelimisha watu wanaotulaumu kwamba sisi ni wezi (japo wapo baadhi) wakati kuna tupo ambao ni waaminifu 100%. Binafsi nina uzoefu wa miaka mitatu (3) katika kazi hii na nimeajiriwa na Bank fulani kongwe hapa nchini.
CHANGAMOTO
Changamoto zipo nyingi katika kazi hii lakini kwa upande wangu ni hizi
-Mwanzo wakati unajifunza kazi unashindwa kupangilia pesa vizuri, hazikai sawa kabisa
-Kuingiza loss kwa kumzidishia mteja
-Mteja anaiamini mashine ya kuhesabu pesa ikiwa utamwambia pesa yake imezidi lakini mashine hiyo hiyo mkihesabu na ukamwambia pesa imepungua anaona unamdanganya

VITUKO
Pia kuna vituko vingi lakini kwa upande wangu ni pale mtu anakuja kazificha pesa zake ndani ndani huko kisha akizitoa ili umhesabie zinakuwa mbichi mbichi hivi
Pia kuna wale wateja ambao wameizoea bank kwahiyo akija hata kama kuna foleni vipi ye anataka ahudumiwe na kuondoka. ...n.k

Karibuni Tellers wenzangu tushee ujuzi na changamoto katika kazi yetu hii ngumu, pia tujibu maswali ya wateja wanao tutuhumu vibaya(japo kiukweli wapo Tellers wenye tabia mbovu) Karibuni.
 
Kuna Tellers mwenzako Mwanamke alishawahi nizishia pesa mara mbili mara ya Kwanza nilirudisha mara ya pili siku nyengine nikaona uboya nikazila hv kesi hizo inakuwaje au ndo mnakatwa mshahara
 
Kuna amount ndogo huwekwa kwa ajili hiyo ikizidi hapo inakuwa juu yako
 
Sina hamu, nilienda kuchukua hela nilizotumiwa kwa njia ya western union kwenye tawi moja wapo la benki ya posta. Siku hiyo kazini nilikuwa nimebanwa hatari na hizo pesa zinahitajika siku hiyo nikirudi nyumbani.

Nikajiiba walau dakika 20 niende nikachukue daah nilitamani kulia, cashier yuko slow hatari. Nikavumilia ilipofika zamu yangu ndo nikachoka kabisa, nilikuwa nachukua milioni tatu na ushee, alizihesabu na mashine kisha akarudi tena kama ziko sawa. Alirudia kuhesabu kwa mashine mara tatu na akahesabu kwa mkono mara 2.

Aliponipa akaniambia karibu tena hata sikumjibu maana nilikuwa na haraka na nikajisemea sitarudi tena hata nikiwa sina haraka. Japo uhakiki wa pesa ni muhimu ila sio kuhakiki kule.

Otherwise poleni kwa kazi ngumu pesa ina mambo mengi, bado hamjaletewa pesa feki....
 
Nilifanya muda mfupi wakati wa mafunzo, orientation (kitaaluma ni mhasibu, ) sio kama teller kwenye kibanda pale mbele bali kwenye bulk cash, wale wateja wanaoleta pesa kwenye vigunia. Kilichonishinda ni kung'amua noti ambazo ni bandia, hata nikioneshwa hiyo sababu inayofanya iitwe ni bandia, sikuweza kuiona. Kilichoniuma zaidi ni kukatwa kwenye mshahara wako kiasi ulichopokea na kurekodi kumbe ni noti bandia.
 
Back
Top Bottom