Uzi maalum jinsi ya kupata kazi miradi mikubwa kama Bwawa la Nyerere, Bomba la mafuta, Standard Gauge n.k

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari zenu wanabodi!

Hebu tujadili leo jinsi gani unaweza ukapata kazi kwenye miradi mikubwa niliyoitaja hapo juu na mengineyo.

Kwanza tumuombe Mungu aujalie uzi huu uwe na wachangiaji ambao sio wabinafsi, ambao watashare experience zao mbinu gani wanazotumia au walizotumia kupata kazi kwenye miradi mikubwa.

Binafsi nimejifunza mengi katika harakati za kusaka ajira na kugundua kwamba pindi unaposikia sehemu kuna mradi mkubwa sio swala la kukurupuka na kwenda kichwa kichwa kwa matarajio ya kupata kazi maana kama una familia unaweza ukaitesa kwa njaa .

Hebu tupeane mbinu sasa. Mtu anawezaje kuchomoka na kupata ajira kwenye miradi mikubwa, wapi anaanzia mpaka kutoboa ukizingatia wengine wanakuwa hawana pakufikia wala connection. Je, anapataje connection?
 
Ni changamoto mkuu kupata kazi kwenye miradi hii mikubwa kama huna kimoja wapo ni ngum sana.
1. pesa
2.mtu unae juana nae kwenye site

#bila hivyo vitu viwili ni ngum sana kupata kazi kwenye miradi.

Kuna wakati hata PESA yenyewe haina maana unakuwa na pesa yako ila kupata kazi hupati cha msingi nikutafuta REFA yani mtu atake kushika mkono .
Binafsi nimekata tamaa nauli nilizo tumia kwenda mwanza kwenye daraja la busisi nikakosa nikaenda musoma kwenye mradi wa maji nikaona napo hapaeleweki nikaenda kisaki kwenye hilo bwawa kucheki ramani nikashindwa hapa nipo nasubili neema ya YAP MERKEZ MWANZA kama napo nitabahatika. nimesha sota vya kutosha.

Naomba kama kuna mtu aliye bahatika kupata kazi kwenye hiyo miradi basi aje atoe ushahidi yeye alipataje.
 
Inamaana hata saidia fundi yaani kibarua nayo ni ngumu kupata mpaka uwe na refa au mkwanja??

Kwani taratibu zao za kupokea wafanyakazi pale site zipoje?
 
Inamaana hata saidia fundi yaani kibarua nayo ni ngumu kupata mpaka uwe na refa au mkwanja??

Kwani taratibu zao za kupokea wafanyakazi pale site zipoje?
Mkuu nimezunguka cha muhimu ni kuwa na mtu alafu uwe na chochote mkononi alafu vyeti ndio vinafata kwenye hii miradi hasa kazi za kawaida vyeti vinakuwa vya mwisho nimehangaika sana mkuu
 
Mkuu nimezunguka cha muhimu ni kuwa na mtu halafu uwe na chochote mkononi alafu vyeti ndio vinafata kwenye hii miradi hasa kazi za kawaida vyeti vinakuwa vya mwisho nimehangaika sana mkuu.
kweli waswahili waliposema mkono mtupu haulambwi hawakukosea..
Je unatakiwa uwe na mlungula kiasi gani sasa?
 
Bwawa la Rufiji nilienda mpaka ofisini kwao pale Makumbusho DERM PLAZA FLOOR YA 12 nikafukuzwa na walinzi. Sisi tusio na wakutushika mkono tunapata tabu sana nchi hii
 
Back
Top Bottom