Uzi maalum: Growth Hacking

Kuanzisha na kukuza biashara ni ndoto na malengo ya kila mjasiriamali, lakini mara nyingine ni vigumu sana kupata mawazo ya namna ya kutoka ngazi moja kwenda nyingine. Biashara nyingi ndogo ndogo huwa zinaanzishwa lakini zinakwama, hazikui na pengine zinakufa kabisa. Ndiposa nimefikiri ni vyema tukawa na uzi ambao tunapeana taarifa na maarifa ya namna ya kukuza biashara zetu kwa mfumo wa 'growth hacking' hususani katika zama hizi za mapinduzi ya kiteknolojia. Tusiachwe nyuma, angalau siku moja tuwe na startup kutoka Tanzania ambayo inaingia katika orodha ya 'Unicorns' duniani.

GROWTH HACKING NI NINI?
Ni kipengele kipya katika tasnia ya masoko ambacho kinalenga zaidi katika ukuaji (Growth). Growth hacking ilianza kutumiwa na startups ambazo zilikuwa zinahitaji kukua haraka ndani ya muda mfupi, na kwa kutumia gharama ndogo kadiri inavyowezekana. Hivi sasa Growth hacking inatumiwa na makampuni ya saizi zote - madogo na makubwa. Make no mistake, inatumia zaidi DATA na TEKNOLOJIA.

Kuanzisha mjadala na ku-inspire watu nimekusanya taarifa zenye maarifa na baadhi ya mifano halisi ya biashara ambazo zilifanikiwa kutumia mbinu zenye gharama ndogo kupata mafanikio makubwa (Incredible growth). Inafahamika, biashara hazifanani - kwahiyo hii mifano na mawazo yanayotolewa humu yakusaidie kubuni mbinu zitakazokufaa wewe, mwisho wa siku lengo ni kuongeza wateja na mapato. Kumbuka, narudia tena, growth hacking inahusisha zaidi DATA na TEKNOLOJIA. Na tuanze kudukua mafanikio kama ifuatavyo:

MBINU YA 1: 'TENGENEZA UHABA' ILI KUONGEZA MAUZO.
Uhaba unaongeza mauzo kwasababu watu huwa wana-experience hofu ya kukosa. Inaitwa FOMO (Fear Of Missing Out.) Katika matangazo yako tumia maneno kama:
  • Ofa ya muda mfupi.
  • Bidhaa zinakaribia kuisha.
  • Promosheni inaelekea ukingoni.
  • Kwa leo tu.
  • Nunua kabla hazijaisha.
Hata kama stock yako bado imejaa, tangaza kuwa bidhaa ndio zinaelekea ukingoni ili kuongeza mauzo kwa kipindi fulani. Kama una e-commerce platform, weka matangazo kama;
  • Ofa hii ni kwa watu X PEKEE!
  • Zimebaki nafasi za watu X.
  • Jisajili kabla nafasi hazijajaa.
  • Usajili unafungwa tarehe X.
MBINU YA 2: TAFUTA DISTRIBUTION CHANNEL YA KUDUKUA.
Unapoanzisha biashara yoyote, unahitaji kutafuta 'distribution channel' ya kudukua. Utauliza, distribution channel ni nini? Ni eneo ambalo wateja unaowalenga tayari wanaenda kutafuta bidhaa wanazohitaji.

Kwa mfano; wakati Airbnb ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza walikuja na mbinu ya kuitumia Craiglist kwa maslahi yao. Craiglist kwa wakati huo ilikuwa ndio tovuti inayoongoza kwa watu kuitumia kutafuta makazi ya muda mfupi. Walichokifanya Airbnb waliwahimiza watumiaji wapya ku-post nyumba zao katika tovuti ya Craiglist - post ambazo zilikuwa na link inayorudi kwenye ukurasa wao wa Airbnb.

Wakafanikiwa kwa mambo mawili muhimu. Kwanza, kama startup mpya hawakuwa na idadi kubwa ya watu wanaotembelea tovuti yao kutafuta makazi ya muda. Wangeweza kulipa pesa nyingi ili kutengeneza na kusambaza matangazo , badala yake wakajipatia 'free traffic' kwa kuwaruhusu watumiaji wa Airbnb kuweza ku-post Facebook kirahisi kupitia Airbnb app. Ofcourse iliwagharimu muda wa kutengeneza teknolojia hii, lakini ilipokamilika iliwapa traffic ya kutosha kuelekea kwenye tovuti yao. Wakapata wateja wengi zaidi pasipo kutumia hata thumni ya matangazo. Pili, walitatua changamoto ya kutafuta wamiliki wa nyumba kwasababu sasa waliweza kuwatafuta kupitia Craiglist na kuwashawishi wahamie Airbnb!.

Waliajiri watu ambao kazi yao ilikuwa kuwashawishi watumiaji wa Craiglist wahamie Airbnb. Kazi nzuri kabisa ilifanywa na growth hackers wa Airbnb na hatimaye kampuni ikakua kwa kasi ya roketi na leo hii imekuwa maarufu duniani.

MBINU YA 3: LEVERAGE DISTRIBUTION CHANNEL AMBAYO TAYARI UNAYO.
Ukishaanza kupata wateja kiasi, anza ku-leverage distribution channel yako mwenyewe . Kwanza, mteja akija dukani/ ofisini/ kwenye tovuti yako muombe akawaambie na marafiki zake, in return utampa motisha fulani.

Kwa mfano: Dropbox iliongeza idadi ya watumiaji wake kwa 60% pale ambapo walianza kutoa 500Mb za ziada bure, pale ambapo mtu uliyemtambulisha kuhusu Dropbox anapo-sign up.
Hata yule uliyem-refer naye anapata storage ya zaida bure. Hii iliwafanya Dropbox waweze kufuatilia ni wapi watumiaji wao wanatoka. Wakaongeza motisha nyingine tena; ukishare Dropbox katika ukurasa wako wa FB unapata storage ya Mb kadhaa bure!

MBINU YA 4: TUMIA MITANDAO YA KIJAMII IPASAVYO.
Kwa mfano wewe unauza simu. Cha kufanya unaingia Twitter, una-search neno "Natafuta simu" au " Nahitaji simu"... kitakachotokea itakuja list ya wote walioandika maneno hayo... kazi inabaki kuwa kwako kuchambua yupi anahitaji simu. Una-reply kwenye post yake kwa kumpa ofa yako (Aina ya simu unayotaka kumuuzia, sifa zake na bei). Vivyo hivyo Facebook, Instagram n.k.

Au unaenda kwenye page ya mshindani wako, unawa-follow followers wake wote. Halafu unaenda hatua moja mbele, unaanza kujibu comments za watu wanaouliza vitu kwa mshindani wako na yeye hawajibu. Cha kufanya unatumia mwanya huo kuitangaza biashara yako.

Usisahau ku-search humu JF, kuna watu wengi humu wanahitaji huduma na hawajapata replies zinazokidhi mahitaji yao. Changamkia fursa hiyo - usiseme sikukwambia.

UPDATE:
Kama mmiliki wa biashara, kuikuza biashara yako ni moja ya vipaumbele. Lakini kwa sisi waanzilishi wa biashara ndogo, tunajua changamoto inayojitokeza: Tunakosa bajeti kwaajili ya kugharamia kampeni kubwa za marketing kama ambavyo biashara kubwa zinavyofanya - na wakati huo kuna vipaumbele vingine vya kushughulika navyo. Kwahiyo, ukiwa kama 'founder', unawezaje kuongeza mauzo na kukuza biashara yako?

Jibu ni growth-hacking. Growth hacking ina maana ya kufanya majaribio tofauti tofauti katika eneo la 'marketing', 'product development', 'sales segments' na maeneo mengine ili kuweza kujua ni kwa namna gani unaweza kuikuza biashara yako.

Kwa mara nyingine nimekuletea mifano rahisi ya growth hacks ikupe mwanga wa namna ya kufanya ili kuikuza biashara yako, kwa gharama ndogo na kwa muda mfupi. Karibu...

MBINU YA 5: FOCUS KATIKA KUTENGENEZA NA KUTANGAZA MAUDHUI.
Weka blogu kwenye website yako - blogu ambayo ina maudhui yaliyoshiba na yanayovutia ambayo yanaendana na aina ya biashara unayofanya. Weka maudhui ambayo yatawafanya wasomaji wako wakuone wewe ni bonge la mtaalamu katika eneo hilo na kwa njia hiyo itakuwa rahisi zaidi kwao kukuamini na kufuata huduma zako.

Lakini kwa jinsi teknolojia ilivyo, si lazima utumie blogu - unaweza kutumia mitandao ya kijamii tu. Kama unafikiri natania kawaulize wafuasi wa Ontario watakusimulia kinachowavutia kwake ni nini. Au mtafute mtu anaitwa Dan Lok (Instagram) au Dr Strive Masiyiwa (Facebook) halafu jifunze toka kwao. Ila za kupewa kumbuka kuchanganya na zako.

MBINU YA 6: UZA FAIDA, USIUZE SIFA
Ninachomaanisha ni kwamba; Sell BENEFITS not FEATURES.
Lakini, unajua utofauti wa hizi terms mbili? Kama hujui acha nikujuze;

Wakati iPod inaingia sokoni ilikuwa na sifa kwamba ina 1GB storage na ni ndogo sana kwa umbo. Hiyo ni sifa, sasa faida ya iPod ni kuwa inakuwezesha kutembea na nyimbo 1000 mfukoni!!!! Sijui kuna mtu kanielewa?

Wewe unamwambia mteja,"Gari hili lina turbo." Ni kweli lina turbo - lakini hiyo turbo inatatua changamoto gani? Ina faida gani? Au unamwambia mteja,"Nauza magauni kutoka Uturuki" Sawa tumekusikia, yanatoka Uturuki - lakini, kwani nitapungukiwa na nini nikiachana na gauni lako la Uturuki nikaenda kununua mtumba Mchikichini?

Wateja siku zote wanatafuta bidhaa itakayotatua changamoto fulani katika maisha yao au inayotimiza matamanio waliyonayo. Kwahiyo, endapo ukimhakikishia mteja kuwa bidhaa yako inaweza kumtatulia jambo lake au inakidhi matamanio yake - aha!

MBINU YA 7: CHEZA NA SAIKOLOJIA ZA WATU - Acha masihara!
Kwa mfano unauza Laptop; Fikiria mifano hii miwili halafu niambie wewe ungekuwa mteja trick ipi ingetumika usingeruka.

A. Muuzaji anakwambia; Nunua Laptop kwa TZS 400,000/= nikupunguzie begi - ntakuuzia kwa TZS 30,000/= badala ya TZS 45,000/= na external HDD 1TB ntakuuzia kwa TZS 120,000/= badala ya TZS 150,000/=

B. Muuzaji anakwambia: Lipia Laptop TZS 590,000/= - ntakupa begi na external HDD bure!!

Utafiti umeonesha trick B ina uwezekano mkubwa wa kumfanya mteja afanye maamuzi kwa wepesi zaidi kuliko A. Kwahiyo - kazi kwako mzee.

MBINU YA 8: TUMIA 'DECOY PRICING'
Hii ni mbinu inayomlazimisha mteja achague bidhaa fulani. Kwa mfano tuseme unauza chipsi na unataka kuongeza wateja wanaonunua chipsi kuku. Kwa kutumia mbinu ya decoy pricing unaweza kufanya hivi:

A. Chipsi kavu - TZS 2,000/=
B. Chipsi + Mayai - TZS 5,000/=
C. Chipsi + kuku - TZS 6,000/=

Sasa tuseme unataka kuongeza wateja wanaonunua chipsi mayai - unafanya hivi;

A. Chipsi kavu - TZS 2,000/=
B. Chipsi + Mayai - TZS 3,000/=
C. Chipsi + Kuku - TZS 6,000/=

Unaweza kuniambia 'decoy' ni zipi hapo? Na umeelewa jinsi hii mbinu inavyofanya kazi? Kwa taarifa yako hii mbinu inatumiwa na makampuni makubwa duniani. Naweka mic pembeni... sitaki kukuhadithia - shuhudia mwenyewe;

View attachment 1477813

View attachment 1477814

View attachment 1477815

***UPDATE II - July 1,MMXX
USHAURI: Chukua kabisa kinywaji ukipendacho kikusindikize wakati unasoma, maana naongelea mbinu moja tu ila naiongelea sana kama nahubiri vile!

Ivi - umeshawahi 'kufilisika' kwasababu ya kodi? I mean - ushawahi kufikiria kufunga biashara kwasababu TRA wamekukalia kooni? Kama bado - jiandae. Juzi tu nimeona mtandaoni kada mmoja wa kile chama ambae alikuwa kwenye 'system' iliyopita na sasa yuko benchi - alijitahidi akafungua nursery school. Sasa dhahama lililomkuta ni kwamba TRA wamemshukia kama mwewe!!! Kwanza alipigwa kodi ya milioni kama 250 ivi, akakata rufaa - wakamwongezea, akakata rufaa tena - wakaongeza tena, mara ya mwisho nimeona ameomba msaada wa waziri.

Siku nyingine nilibahatika kuiona post ya ndugu yetu wa damu kabisa aitwae Isaya Yunge - alitoa ya moyoni juu ya nini kiliifelisha 'startup' yake ya 'Soma Technologies'. Japo ilikuwa ni post ya maandishi lakini niliweza kumsikia 'anavyolalama' na kuufokea 'mfumo' wa nchi yetu. Kwa jinsi alivyoufokea mfumo mpaka yeye mwenyewe alijishtukia akafuta ile post haraka sana kabla wapwa hatuja-sceenshot.

Haya mambo ni kawaida sana hapa nchini na pengine afrika kwa ujumla. 'MIFUMO' yetu sio mizuri kwa ujasiriamali. Kuanzia sera, sheria, kanuni, mitazamo ya jamii, uongozi na mazingira kwa ujumla wake... vyote vimekaa mkao wa kumfelisha mjasiriamali yeyote anaejaribu kupiga hatua kubwa tangu siku ya kwanza. Whether ni makusudi au la - mimi sijui, ila naamini tunakubaliana kuwa mifumo si rafiki.

Kama unafikiri natania; Nenda Njombe, ukifika muulizie mzee anaitwa Mzee Pwagu... sikiliza simulizi yake. Kisha nenda Mbeya, muulizie yule fundi gereji aliyetengeneza helikopta, ukimpata - sikiliza simulizi yake. Kama huko ni mbali, ingia Instagram - muulize Wema sepetu au Alberto Msando au Freeman Mbowe - wote wana kitu kimoja kinachofanana; kuna wakati biashara zao ziliingia matatizoni kwasababu moja tu - walikuwa nje ya 'system'. Ivi sijui mnanielewa?

Sasa waneni husema; "Mwenzako akinyolewa, zako tia maji." Kizazi kipya tunasema;"Jifunze kutokana na makosa - ya wengine."(Sio lazima yakukute wewe ndio ujifunze.) Unapoona kila mjasiriamali anaulalamikia 'mfumo, au anailalamikia serikali, au anailalamikia TRA, au anazilalamikia sheria, sera, kanuni au anamlalamikia Mungu, au pengine anamlalamikia mke wake, watoto wake, blah blah blah.... wewe unafanyaje ili kukwepa hayo yanayowaumiza wenzako?!?!?

Twende taratibu... ni vizuri kuwadanganya wengine lakini usijaribu kujidanganya kuwa hayatakukuta, kwasababu hata Marehemu Kapteni John Komba alipokuwa anaimba ile 'Mbele kwa mbele' nashawishika kuamini kuwa hakuwahi kufikiria kuwa ipo siku 'mfumo' utamgeuka. Vivyo hivyo mzee wa 'goli la mkono' na 'Bunge recorded and edited' - sidhani kama wakati anafanikisha kupatikana kwa goli la mkono aliwaza kuwa ipo siku 'mfumo' utamgeuka. Umeanza kunielewa elewa eeh?

Basi hebu vaa kofia ya ujasiriamali, darasa huru na liendelee;

MBINU YA 9: USIUPIGE MFUMO, PIGANA NDANI YA MFUMO. (DON'T FIGHT THE SYSTEM - FIGHT IN THE SYSTEM.)
Hakuna wa kukuonea huruma hapa, kwahiyo usitie huruma. Kuna wengine kule nyuma hawajasikia.... nimesema hivi... NOBODY GIVES A F*** what you are going through bro, you either compete or die.

Pia lawama siku zote hazijengi, kwahiyo usijaribu kumlaumu yeyote; yaani hata wewe mwenyewe usijilaumu - futa kabisa neno lawama kwenye kamusi yako. Kulalamika pia ni rahisi sana, kila mtu anaweza kulalamika - na ndo mwisho wa siku tunajikuta tumekuwa nchi ya walalamikaji; Mwananchi anamlalamikia kiongozi wake, kiongozi anailalamikia mamlaka iliyo juu, mamlaka iliyo juu inamlalamikia Mungu, Mungu tu ndo sijawahi sikia amelalamika hata siku moja. Swali la kijinga unaloweza kuniuliza ni kwamba - kwahiyo tufanyaje? Ntakujibu - pambana ndani ya mfumo.

Sikia, wakati UBER inaanzishwa ilikutana na upinzani mkali toka kwa madereva taksi za kawaida na mamlaka za kiserikali. Madereva taksi walikuwa wanalalamika kuwa madereva wa UBER wanapiga hela ndefu wakati hawana leseni za biashara za 'udereva taksi' ambazo ni gharama. Mamlaka za kiserikali zilikuwa zinaibana UBER iwatambue madereva wake kama wafanyakazi rasmi na sio 'wakandarasi'. Pia mamlaka zilikuwa zinashindwa kuamua UBER iwekwe kundi gani; Taxi company au Technology company?. Kwa ambae haelewi - UBER haiajiri madereva, inatoa mikataba ya muda mfupi. Kwamba umejisajili UBER haimaanishi umeajiriwa na UBER. Kwahiyo, kwasababu haiwaajiri madereva imeepuka kuwa responsible kama mwajiri. Wengi wetu tunafahamu - waajiri wana mambo mengi ambayo wanapaswa kuyatimiza kwa wafanyakazi wao - UBER walikwepa hiyo since day 1. *Hiyo ndo inaitwa DISRUPTION / Challenging the status quo.

Sasa, kufika hapa walipo leo, UBER wamefanya mambo mengi sana nyuma ya pazia ambayo wengi hawajapata fursa ya kuyasikia. Siwezi kuelezea yote maana ni mengi, lakini nitakupa mbinu moja ambayo UBER waliitumia 'kupigana ndani ya mfumo'. Ilikuwa hivi;

UBER ilipata upinzani mkubwa pindi walipoanza ku-scale (Yaani kuipanua bishara yao katika nchi tofauti duniani). Serikali nyingi zilikuwa zinawanyima vibali kwasababu tofauti tofauti. UBER wakatumia mbinu moja.... wakaanza kujipenyeza kimya kimya bila ya serikali za nchi husika kujua. Lengo lao lilikuwa moja... kuhakikisha wanapata wateja wengi (Traction) kwa namna ambayo watakaopenda kuomba kibali serikalini, serikali ishindwe kuwazuia kwasababu ya wingi wa watu ambao tayari wanaitumia UBER (Too good to resist). Kuna mtu hajaelewa, ngoja nijaribu hivi;

Fikiria unataka kuanzisha biashara ya kutoa huduma jijini Dar ambayo unajua fika ukienda kuomba kibali utanyimwa. Cha kufanya, wewe anza kuitoa hiyo huduma kimya kimya, mdogo mdogo - bila matangazo, bila mbwembwe, unapata wateja through word of mouth - acha wateja wasimuliane wenyewe. Unaifanya hiyo biashara kwa muda fulani na hatimaye unapata wateja kama Milioni 2 hivi wanaotumia huduma yako. Ndiposa unatoka na takwimu zako hizo zilizoshiba, unaenda kuomba kibali. Kwamba mimi XYZ nina biashara ABC ambayo ina mpaka sasa ina watumiaji wa moja kwa moja Milioni 2. Watakunyima?

Weee acha ubwege - ndio, wanaweza kukunyima na unaweza kujikuta unapewa kesi ya uhujumu uchumi kwa kufanya biashara kinyume na sheria. Na ndio maana ili uweze kupigana ndani ya mfumo wowote, ni LAZIMA uhakikishe kwanza unazielewa vizuri SHERIA ZOTE ZA MCHEZO kisha unaanza kuzivunja like nobody's business. {Ssssh sogea nikunong'oneze.... si unamfahamu Chenge mzee wa vijisenti? Ivi unakumbuka kila dili kubwa na yeye yumo lakini hajawahi kupatikana na hatia popote? Sasa yule bwana ndo mfano halisi wa hii kanuni ya kuelewa kwanza siri ya mchezo kabla hujaanza kucheza rafu za kukata na shoka. Lakini ibaki siri yetu, usimwambie mtu, umesikia!?!?!?}

Well, kiuhalisia ni vigumu kuzielewa sheria za mchezo kwa muda mfupi, kama wewe hujasomea sheria; mbaya zaidi kuna waliosomea sheria lakini bado ni mtihani kwao kuzielewa sheria za michezo vizuri. Na ndio maana wapo wataalamu, wanaogopwa wakiwa mbele ya pilato; akina Kibatala, Lissu, Msando na wengine a.k.a Mawakili Wasomi. Pointi ni kuwa hakikisha unasema na watu wa kada hii vizuri kabla hujaanza kuucheza huu mchezo ili ujue wapi unaweza ku-take advantage ya udhaifu wa sheria. Kama huna rafiki hata mmoja ambae ni wakili msomi - anza kum-find ASAP.

Kuna wakati UBER walitengeneza version ya UBER app ambayo ilikuwa mahsusi kwaajili ya watu wa vyombo vya ulinzi na usalama tu. Yaani ilikuwa hivi; Kama wewe ni polisi, au FBI, au CIA basi ujue app ya UBER utakayo-download sio ile halisi. Ukiitisha gari linakuja lakini dakika chache kabla ya kukufikia dereva ana-cancel. Polisi wa huko mbele mbele washatembea sana kwa miguu na wakati UBER zilikuwepo za kumwaga. Sasa usiniulize waliwezaje kuwatambua hao wanausalama, ila ninachojua ni kuwa teknolojia inakua kwa kasi ya ajabu. You have to be ahead of the game.

Najua, wengi huwa wana-opt kutumia siasa. Yaani unachukua kadi ya chama, unaweka bendera ya chama katika maeneo yako yote ya biashara, na pengine unagombea uongozi kwa lengo moja; kujihami dhidi ya mfumo. Tatizo ni kwamba, siasa ni si-hasa na ni mchezo wa hovyo sana; wakati na saa usioijua siasa inakutema na kukuacha unapambana na mfumo bila huruma. Kawaulize vibopa wa enzi za Kikwete wako wapi siku hizi, kisha kawatafute wote walioshikamanisha biashara zao na siasa... wako wapi? Ukishikamanisha biashara zako na siasa manaake wewe umechagua kuishi maisha ya ujanja ujanja. Sasa siku ukitoka kwenye siasa au chama lako likitoka kwenye siasa ndo utaelewa ninachoongea.

Bado hujaelewa namna ya kupambana kwenye mfumo? Well sikia hii; Makampuni mengi makubwa duniani, na hata hapa kwetu huwa yanakwepa kodi. Lakini hayawezi kushtakiwa, unajua kwanini? Yanacheza na sheria. Unakumbuka wakati taasisi za kidini zinapata msamaha wa kodi - ikazuka kawaida ya watu kuagiza bidhaa nje ya nchi kwa jina la taasisi fulani ya kidini ili kutolipa kodi! Ile sheria ya msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini ilikuwa ni fursa kwa wajasiriamali wajanja.

Wengine wanatumia mfumo wa Holding company - yaani unakuwa na kampuni mama ambayo haijasajiliwa hapa nchini. Hiyo kampuni mama unaenda kuisajili katika nchi ambayo ina unafuu mkubwa wa kodi na mazingira yake ya kibiashara yako vizuri (Kuna utulivu wa kisiasa na sheria imara). Kisha unakuja unafungua kampuni dada (Subsidiary) hapa nchini. Kisha unahakikisha assets zote zinamilikiwa na ile kampuni mama, then kampuni dada inafanya kuazima au kukodisha.

Baada ya hapo mapato yote na faida unahakikisha zinahifadhiwa katika akaunti za kampuni mama za huko huko ughaibuni. Na unahakikisha pia kampuni dada inalipa gharama za kukodisha assets n.k. Unacheza na namba kwa namna ambayo kampuni dada mwisho wa siku inaweza kuonekana haizalishi faida yoyote. Na ukishapiga shekeli za kutosha, unairipoti kampuni dada kama imefilisika - na auditors wakicheki vitabu vyako wanakuta kweli mzee mapato yako yote yalikuwa yanalipa madeni kwa kampuni mama. Uzuri ukifilisika, umefilisika... unaondoka taratiiibu huku ukitabasamu kimoyo moyo - usitabasamu usoni bro maana utafungwa... ohooo!!!

BOTTOM LINE:
Sahau vyote nilivyosema katika mbinu hii ya 9 ila kumbuka kitu kimoja - siku zote tafuta mbinu za kucheza kwa kutumia sheria zilizopo. Usikatishwe tamaa na mfumo, tafuta namna ya kucheza ndani ya mfumo pasipo kukanyaga waya. Na zaidi ya yote, changamoto ni fursa kwa mjasiriamali; kwahiyo kama kuna changamoto nyingi maanake kuna fursa nyingi.

Tatizo nini bro?.. rushwa? - buni njia ya kuondoa rushwa, utapiga mamilioni. Hakuna ajira? - Fungua kampuni yako ili ujiajiri. Tatizo nini, mtaji? Kama huwezi kutumia TZS 10,000/= kuanzisha biashara basi hata ukipewa TZS 10m utafeli tu - huna DNA za ujasiriamali. Hata kama huna hata mia, bado sio sababu ya kufeli; watu wana pesa - unachotakiwa ni kutafuta namna ya kuwafanya watoe hizo pesa kukupa wewe.

Well, mimi sio motivational speaker - kwahiyo sisemi kuwa hizi changamoto ni ndogo, la hasha. Lakini najua maisha ni kuchagua - kwa kila kinachotokea una options za kuchagua. Na unapochagua kimoja unapoteza kingine... that's a fact! Na ukisema huchagui chochote, nature itakuchagulia by default.

Chagua kuacha kulalamika, chagua kuacha kuwalaumu watu wengine, chagua kuacha visingizio, chagua marafiki wazuri wenye faida, chagua aina ya ushauri unaosikiliza, chagua kupambana mpaka kieleweke, chagua kufurahi siku zote, chagua kula vizuri, chagua kuwajali wengine, chagua kutazama fursa kila mahali, chagua kuona nyota zinazong'aa badala ya giza, chagua kutokuogopa kukosea kwa kuwa ni fursa ya kujifunza, chagua kutokimbia matatizo, chagua, chagua, chagua... chagua kupambana ndani ya mifumo hii hii tuliyonayo.

Kama si wewe, nani? Kama si sasa, lini?

* NEW UPDATE - July 08,MMXX *
MBINU YA 10: USIWE BOMBA, KUWA JUKWAA. (Do not be a pipe, be a platform)

Twende kwa mifano:
~ Millardo Ayo, Muungwana blog, Michuzi blog n.k. ni pipes Vs Jamiiforums ni jukwaa.
~ CNN, BBC, Aljazeera, CNBC n.k. ni pipes Vs Youtube, Netflix, Instagram, Facebook, Tik Tok n.k ni platforms.
~ ITV, EATV, Clouds TV, TBC n.k. ni pipes Vs Azam (Decoder & dish), Continental, Star times, DSTV n.k. ni platforms.
~ Samaki samaki, Nyama choma point, Choma hut, Tam tam BBQ n.k. ni pipes Vs Nyama choma festival ni platform.
~ Game supermarket, Danube, Tigo shop, Vodashop, CRDB, Merry Brown na maduka yote pale Mlimani City ni pipes Vs Mlimani City yenyewe (Mall) ni platform.
~ Vyuo vingi ni pipes Vs Udemy, Skillshare n.k. ni platform.
~ Jumia, Amazon, Alibaba n.k. ni Platforms

Mifano ni mingi lakini lengo langu upate mwanga kidogo wa utofauti wa pipe na platform. Kwa kifupi, pipe ni business model ambayo wewe mjasiriamali unazalisha bidhaa, kisha unazisukuma kwenda kwa mtumiaji (Mteja). Kwa upande mwingine, platform ni business model ambayo wewe mjasirimali 'UNAWAUNGANISHA' wazalishaji (Wauzaji) na watumiaji (Wateja) - kisha unapiga pesa in the process.

Kadiri platform yako inavyokuwa kubwa zaidi, ndivyo unavyovutia watumiaji wengi zaidi = pesa zingi zaidi. Kwa mfano; Mkoani Njombe hivi sasa kila mtu anakimbilia kulima parachichi. Kwahiyo, kila mtu anafanya biashara ya parachichi kwa mfumo wa pipe. Lakini, ni nani anayefikiria hizi parachichi zitaenda wapi msimu wa mavuno na zitaendaje? - hapo ndipo platform inapoingia.

Kwanini asitokee mbunifu mmoja akatengeneza platform inayowaunganisha wakulima wa parachichi na masoko, wauza pembejeo, taasisi za kifedha, wadau wa kilimo na serikali? Au kwanini asitokee msomi mmoja wa biashara akatengeneza network ya wakulima wa parachichi Tanzania na kuwaunganisha na soko moja kubwa huko ughaibuni? Tunakwama wapi? Au tunawasubiri wakenya waje na platforms zao, sisi tubaki kulalamika mitandaoni?

Ok, tuachane na kilimo (Najua wengi hawakipendi) - twende instagram; mbona kama kila mtu sasa anakimbilia kuuza mtandaoni? Ni nani anaefikilia kuanzisha Jukwaa la kuwakutanisha wauzaji na wanunuaji wa mitandaoni? Najua utanambia zipo Jumia, Amazon, Jiji, Alibaba, eBay, n.k. Na mimi nitakwambia kati ya zote hizo hakuna iliyofanikiwa kupenya sawasawa barani Afrika, achilia mbali Tanzania. Maanake bado kuna gap kwenye ecommerce platforms Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Bado kuna gap kwenye delivery platforms. Bado kuna gap kwenye banking industry. Bado kuna gap kwenye education platforms. Bado kuna gap kwenye healthcare platforms. Bado kuna gap kwenye agriculture platforms. Bado kuna gap kwenye dating platforms. Bado kuna gap kwenye logistics platforms. Bado kuna gap kwenye housing platforms. Bado kuna gap kwenye booking platforms. Bado kuna gap kwenye gig economy platforms. Bado kuna gap kwenye sharing economy platforms. Bado kuna gap kwenye Blockchain powered platforms. Bado kuna gap kwenye Big data, Artificial Intelligence, Machine Learning, Alternative energy, Alternative food.... Listi ni ndefu - wasomi wetu wapendwa sana, ivi mnakwama wapi?

Badala ya kuuza chakula, unaanzisha media inayofanya reviews za sehemu zinazouza chakula. Ukipata traffic ya kutosha, unaanza kuwauzia bidhaa zinazosaidia katika shughuli za upishi wa chakula. Unakula hela za matangazo, unakula hela za mauzo ya bidhaa, unapata passive income isiyoisha huko Youtube.

Badala ya kulima vitunguu, unaanzisha jukwaa la kuwakutanisha wamiliki wa mashamba na watu wanaoishi mijini ambao wanataka kuwekeza katika kilimo. Ila angalia usifanye kama wale wengine ambao huishia kudhulumu pesa za watu.

Badala ya kuuza viatu mtandaoni, anzisha platform ya 'escrow'. Platform ambayo mteja akitaka bidhaa analipia kabisa lakini pesa haiendi moja kwa moja kwa muuzaji, bali inatulia mahali ikisubiri muuzaji afanye delivery ya bidhaa. Muuzaji anafanya delivery akijua kabisa bidhaa ishalipiwa. Mteja akipokea bidhaa, muuzji anapewa pesa yake - wote wanaondoka wakitabasamu, no janja janja.

Badala ya kuwa bomba, kuwa jukwaa. Fanikiwa kwa kuwawezesha wengine. Youtube wamefanikiwa kwa kutuwezesha mimi na wewe kuwa waandishi wa habari na maprodyuza tunaojitegemea. Facebook wamefanikiwa kwa kutuunganisha mimi na wewe na kutusaidia kutupia kila upuuzi tunaotaka sisi. Tik tok wamefanikiwa kwa kutuwezesha kuonesha vipaji, vituko, na utopolo wetu kwa dunia nzima. Netflix wamefanikiwa kwa kutuwezesha mimi na wewe tuweze kutazama movie kali, tunazopenda, mfululizo, exclusively, popote, saa yoyote, kupitia kifaa chochote tupendacho.

Tunaloelekea, kila kampuni itakuwa ni kampuni ya kiteknolojia. Na tusibishane katika hilo tafadhali - asante. Mpaka wakati mwingine, kwa leo naishia hapa.

Virus.
July VIII, MMXX
Madini ya moto haya thanks mkuu! Umenifungua akili
 
Uzi mzuri sn na unakaribia mwaka Ila Una wachangiaji wachache Sana..hapa ndy utajuwa wabongo ni watu wa Aina gani

Wacha mama nae awaruhusu wakenya waje bila permit kisha tuendelee kulalamika wakenya wanatubaka kwenye kila sekta
 
Hata sijasoma ila nimepanga kusoma nikitulia ila nmekupa like kwa jitihada zako kuweka madini haya na pia nme comment ilu post iwe juu wengine nao waone.

Big up sana
 
Uzi muhimu sana huu kwetu sisi vijana watafutaji
 
Pokea 5 ✴️...
Sina Hakika Kama Kuna Uzi utakuja kufikia Level Hii
 
Huu uzi inapaswa kila mtu aupitie kwenye hili jukwaa la biashara

Pongez nying kwa mwandishi kwa elimu hii murua ya kibiashara
Ubarikiwe sana bro
 
Back
Top Bottom