Uzi kwa wanawake wanaotembea na waume za watu wasio na uwezo kifedha

lhera

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
1,835
3,603
Nyinyi wanawake/wasichana mnaotembea na waume za watu wenye kipato cha chini hata wanashindwa kuwa hudumia wake zao ipasavyo mna akili gani au mnafikilia nini?

Kuna mwanamke/msichana anatembea na mume wa mtu ambaye ana kipato cha chini sana na huyo mwanamke/msichana nae ndio walewale kipato chake nae cha chini sana zaidi au wanalingana kipato,mwanaume hana msaada wowote zaidi ya kufanya zinaa hata ukiomba 100,000/hana uwezo wa kukupa zaidi zaidi anakulipia nauli ya daladala Sababu mnapanda wote mnaelekea njia moja,

Akilipia daladala ndio imetoka hiyo, labda siku akikupa pesa labda 2000/ ikizidi sana 5000 napo si mara kwa mara na mwanamke/msichana na umepanga chumba anakuja ana kuzini kwenye chumba chako unacho lipia kodi kwa gharama zako, si mtu wa kuchangia kodi hata nusu, si wakutoa hata pesa ya umeme au maji hata pesa ya kula. Anakuja kwenye chumba chako na anafika na ushampikia kwa gharama zako.

Jiulize anavyokufanyia ww mchepuko hata mkewe anamfanyia hvyo? Ww ndio kila siku wakukwambia pesa hana umvumilie na ahadi kibao za kukupa matumaini labda atapata kesho atanipa,au utasikia kuna mipango nafuatilia ikikaa sawa ntakuoa dini inaruhusu,mipango hiyo miaka nenda miaka rudi haikai sawa ni hivyohvyo kila siku afadhali ya Jana.

Mwanamke/msichana unaona kabisa huyu mwanaume hana msaada wowote zaidi ya zinaa lakini umo tuu,
Yaani bora huo uvumilivu kwa mwanaume ambaye hajaoa pengne labda anaweza akinioa tutasaidiana, mwanamke/ msichana hapo ndio kapendaaa kufa kuoza hata akitongozwa na wanaume ambao hawajaoa ana kataa, anasubili ahadi za bahati nasibu,tena wanaume kama hawa wabaya wanakubana yaan wanajifanya wanawivu na ww kinoma noma yaan hataki uchepuke.

Siku ukija ukishtuka mwanamke/ msichana muda ushaenda na hakuna ulichoambulia zaidi ya maumivu tu,

Nb: Yaan utakuta mwanamke/msichana anasema mwanaume hana pesa ila nilichompendea mpole, mkweli, muaminifu, hana gubu, muelewa n.k angekuwa ana hayo yote ange msaliti mkewe?

Bhasi mwanamke/msichana ana kazi ya kuwaomba wanawake/wasichana wenzie pesa nikopeshe kiasi Fulani ntakulipa! Hadi unamuuliza pesa ndogo kama hiyo bwana wako hana uwezo wa kukupa hana cha kusema anaguna guna na kubinua midomo.

Wanawake/wasichana acheni matumizi mabaya ya dhambi.
 
Kwani kuna tamuu zaidi ya hiyo zinaa? wache wenzio wapate raha kama kampata wa kumzinisha vizur wewe baki na maisha yako ukipata hizo pesa umtafute MTU akuweke vizur
 
Kudate na Mume mwenzio awe na pesa au asiwe nayo ni kharam.

Usishauri wadate na wenye pesa tu.
 
Mbona wanawake wenzio hawachangii huu uzi wako?
Nilishangaa siku moja kusikia mwanamke anamtukana mwanamke mwenzie eti "wewe ni **** tu"
Hivi kuna mwanaume atakaye toa ushauri huu? Ana jua machungu yake anayejua ni mwanamke,na wala sijabuni mambo hayo yapo nimeyaona
 
Back
Top Bottom