Uzi kwa tuliowahi na tunaofanya kazi kwa Wahindi tupeane changamoto za mabosi zetu

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
6,895
2,000
Sasa jibu wewe busara zako zilikuwa wapi? Kabatini?...

...uzi unaongelea walioajiriwa na wahindi wewe unaleta ulivyotemewa mate na mtoto wa kihindi barabarani ambae hujaajiriwa na babake wala mamake...
Mchepuko wangu "Happy Christmas "
Mbona umeniblock ku simu?
 

naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,718
2,000
Hulijui usemalo, Mhindi kama unamfahamu tu juu juu utasema haya, hakuna mtu aliyefanya kazi na Mhindi anaweza kuandika huu utumbo hata awe extraskilled, Kama Wahindu ndio kabisa hata wenyewe wana Casts na wanadharauliana na hawachangamani hata kwa kuoana na Banians ndio Superiors, Ukifanya nao kazi utaona hata wenyewe kwa wenyewe wanatengana ukichunguza unagundua ni casts tofauti au Dini tofauti, Nilikua na Boss wale Wahindi weusi tunawaita Goa nadhan alinipa hizi story na kunitajia wahindi wote na Dini na casts zao pale kazin na kweli walikua wanatengana na kama huyo mweusi walikua wanamponda Sana wakiwa na waswahili though alikua Boss wao pia.
Wana saikolojia yao yakuwavika kilemba cha ukoka baadhi ya waswahili nao wanajiona wahindi pia na kusnitch wenzao,
Tena nabisha kweli kweli kwa sababu wahindi nawajua vilivyo.

Ukiona mhindi anakuletea dharau ujuwe kakuona upo "under par".

Mhindi anaheshimu sana mtu anaejuwa kazi yake na atafanya lolote asikupoteze ukiwa mchapa kazi.

Ukiona mhindi anakuletea nyodo ujuwe kishakuona kazini hauna umuhimu yaani "you are either semi skilled or unskilled".

Hivi uwe "skilled" kweli Mhindi akuletee nyodo? Khaa! Uongo huo. Kina Mo wasingeajiri watu zaidi ya 100,000 Tanzania hii, wengine ni "highly skilled".

Nyie mnaolalamika humu wote hamkidhi vigezo, hata mkiajiriwa na nani mtasema mnanyanyaswa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MMOJA

JF-Expert Member
Aug 30, 2012
439
250
Binafsi nimeshawahi kufanya kazi kwa Muhindi kama Bosi wangu. Kipindi naanza kazi nilikutana na ahadi kibao na mambo mazuri mazuri tuliahidiwa kama kazi ikiwa nzuri marupurupu yataongezeka. Pigo la kwanza niliomba mkataba bahati mbaya nilipigwa chenga palikuwa na sijui sijui nyingi.

Nikapotezea nikaanza kazi moja kwa moja. Miezi ya mwanzo nilipwa fresh ila masharti ya bosi yalikuwa lazimausipendeze alikuwa anahisi napendeza kwa pesa zake. Nasonga nao mpaka sasa

Kwa mdau aliyepitia huku atiririke na je kuna yeyote aliyefanikiwa kupitia ndugu zetu hawa?
Kuna kampuni zingine za kitanzania, ni wahindi weusi,
Kwa tabia zao kasoro rangi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ManDizzo

Senior Member
Jun 25, 2014
133
250
Dah! Kazi kwa mhindi skia tu
Full kutukanwa,kufokewa,kupelekeshwa hujamaliza kazi hii unapewa nyingn
Ukiweza kufanya kazi kwa wahindi hakuna kazi itayokushinda.


Boss hajasoma wakijua kingereza basi nafasi za juu wanapeana kifamili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom