Uzeruzeru ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzeruzeru ni nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, May 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,002
  Likes Received: 3,592
  Trophy Points: 280
  [h=1]Anemia ya Sickle Seli[/h]Watu walio na hali hii huwa wana upungufu wa chembechembe nyekundu kwenye damu mwilini. Hivi ni kumaanisha kuwa miili yao huwa haibebi hewa ya kutosha ya oksigeni. Hali hii inaweza kuwafanya wawe wagonjwa. Kuna kitu chekundu katika damu kinachotwaa oksigeni katika hwa na kuipeleka kila mahali mwilini. Huwa kemikali ndani ya chembechembe zilizo asili ya kila kitu chenye uhai, kisipoumbika vizuri na kikose kupita ndani ya mishipa ya damu, mishipa inaweza kuziba na kusababisha maumivu makali.
  Sickle Cell ni hali inayorithiwa. Mtu huipata kutoka kwa wazazi wake. Kila mtu hupata nusu ya jeni (genes) zake kutoka kwa mzazi wa kiume nusu na kutoka kwa mzazi wa kike. Iwapo wazazi wote (baba na mama) wana jeni ya Sickle Cell, wanaweza kupata mtoto aliye na ugonjwa huu hata kama wao wenyewe hawana.​
  Sickle Cell – hali hii hupatikana sana sana kwa watu wanaotoka sehemu za Afrika ya Kati na Magharibi.​
  Watu walio hatarini zaidi ya kupata ugonjwa wa Anemia ya Sickle Cell
  Wengi walio na hali hii katika damu yao hutoka sehemu za Afrika ya Kati, Amerika ya Kusini na Kati, India ya Kati na nchi za Mediterania kama vile Uhispania, Uturuki, Ugiriki na Italiano.​
  Kutambua iwapo una ugonjwa huu
  Mtu yeyote anaweza kuenda kuangaliwa na daktari kuchunguza iwapo ana ugonjwa huu. Iwapo wewe na mpenzi wako mnapanga kuoana na kuwa wazazi, ni lazima ufanyiwe uchunguzi hasa iwapo mnatoka sehemu ya Afrika ya Kati au mna wazazi wanaotoka kwenye sehemu ambako ugonjwa huu upo. Daktari wako anaweza kukufanyia uchunguzi au akutume kwa daktari mwingine aliye na ujuzi wa kukagua tabia zinazorithiwa za kifamilia.​
  Iwapo mna mtoto ni muhimu afanyiwe uchunguzi iwapo ana ugonjwa huu au upo ndani ya uzao wake. Ni muhimu kutambua mtoto wako anapoendelea kukua iwapo ana huu ugonjwa. Muone daktari mara moja kama utaona dalili zifuatazo:​

  • Homa
  • Maumivu ya kifua
  • Kupumua haraka haraka
  • Uchovu
  • Kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake
  • Kupoteza nguvu mara moja na kukosa hisi
  • Maumivu ambayo hayataisha hata baada ya kupewa dawa za kupunguza uchungu pale nyumbani
  • Kuhisi kujamiana ambako ni kuchungu mno na hakuwachi
  • Mabadiliko ya kighafla katika namna unavyoona vitu
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,002
  Likes Received: 3,592
  Trophy Points: 280
  [h=1]Matibabu na njia za kukuwezesha kuishi na afya[/h]Ugonjwa huu hautibiki. Lakini madaktari wanaweza kutibu dalili ndogondogo hata zile kubwa. Iwapo una huu ugonjwa na unahisi maumivu makali, madaktari watakupa dawa za kuzuia maumivu na vinywaji vingi.
  Kuwekwa damu ingine kila mara kunasaidia kukabiliana na upungufu wa damu mwilini (Ni muhimu upewe damu nzuri)

  Hapa kuna namna ambavyo unaweza kuishi ukiwa na afya nzuri.

  • Kila siku meza dawa ya asidi ya vitamini C (folate) ili ujenge upya chembechembe nyekundu zilizo asii ya kila kitu chenye uhai
  • Meza dawa za penisilini iliyoandikiwa kila siku mpaka utakapotimua miaka sita ili uzuie maambukizi
  • Kunywa maji mengi kila siku (kati ya glasi 8 – 10 kila siku kwa watu wazima)
  • Jiepushe kukaa mahali ambapo ni baridi sana au pana joto jingi sana
  • Jaribu usifadhaike au kuchosha sana mwili wako
  • Pumzika vya kutosha
  • Tazamwa inavyostahili kila mara na daktari anayejua sana kuhusu ugonjwa huu

   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 45,970
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  Mzizi Mkavu, kuna uhusiano gani kati ya Zeruzeru na Sickle Cell?...nijuavyo upungufu wa kiini cha rangi ngozi "melanin" ndio hupelekea mtu au kiumbe jamii ya wanyama au wadudu kuwa zeruzeru.
   
 4. L

  Luushu JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 478
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 60
  Hapo MZIZI MKAVU umenichanganya nimeshindwa kukuelewa unamaana zeruzeru ana sikoseli au zeruzeru ni tatizo tofauti na sikoseli fafanua mkuu
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,272
  Likes Received: 4,250
  Trophy Points: 280
  asante kwa somo la 'sikoseli'
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,002
  Likes Received: 3,592
  Trophy Points: 280
  @watu8 samahani nilikosea Kichwa cha maneno (ZeruZeru) badala ya kuweka ( Anemia ya Sickle Seli) samahani.

  @Luushu Kichwa cha maneno ni Anemia ya Sickle Seli sio Zeruzeru Samahani kwa usumbufu.
   
Loading...