Uzembe wa TANESCO, Nguzo iliyo anguka yaua Mwanafunzi Kyela

Ndugu mpendwa mteja wetu

Tumefatilia kwa kina mpaka kwa uongozi wa eneo husika hakuna nguzo iliyoanguka bali ziliinamana na kazi ya kuzibadilisha ilishindikana kutokana na uwepo wa nyuki wengi kwenye nguzo hizo.Usiku wa kuamkia leo tumefanikiwa kuondoa nyuki na sasa zitabadilishwa.Aidha hakuna kifo chochote kilichotowe taarifa au kutokea eneo husika hivyo kama una taarifa ya ziada weka hapa na namba yako tukusikilize.
Asante kwa kufuatilia, ila swali langu kwako kwa nini mlishidhwa kuondoa nguzo kwa siku zote hizo mpaka kifo kimetokea ndo mmeweza kuwaondoa nyuki. Si mngewaondoa toka first day mlipopewa taarifa
 
Je umepitia majibu yetu ya kukanusha hii taarifa?

Tunahitaji transparency
Kwenye website yenu wekeni ukurasa wa wazi kwa public ukionyesha malalamiko yanayowasilishwa na wateja wenu kila siku na hatua mnazochukua na wale waliowasilisha malalamiko wacomment kama kweli issues zao zimefanyiwa kazi au hadaa
 
Hii iwe funzo iondoke na meneja wa taa mi siko mkoa, wilaya na hata taifa, wameweka namba za simu hadharani wakati hazipatikani, zikipatikana hazipokelewi, zikipokelewa hazifanyiwi kazi, cha kushangaza unakuta magari yao yameegesha kwa mamalishe wanakula supu
Na kwenye vigrocery wanakata umeme wa konyagi
 
Tanesco mnathibitisha udhaifu wenu hadharani.

Ina maana baada ya malalamiko ya kuwa nguzo imeua ndiyo mkaja na majibu ya kukanusha?

Kama malalamiko hayo yasingekuwepo maana yake hakuna kazi ingefanyika.

Hao nyuki waliwashinda akili hapo kabla. Ila leo dawa ndiyo imepatikana. Rungu Spray iliwashinda kununua?

Pathetic!...
 
Hivi mnacho kikosi cha uchunguzi cha shirika?
Mmepewa tip anzeni kufuatilia mtawaona watendaji wenu wakifanya hayo na Landcruiser zenu
Mpaka malori Yani, unakuta foreman anaenda kunywa chai ,hafu wafanyakazi wamekaa kwenye Lori wanamsubiria . Saa tatu au nne . Tena hili la kunywa supu mda wa kazi ni limeota mizizi Yani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa hatua zaidi
Yaani whistle blower unataka atoe namba ya simu tena? Hivi wengine akili zenu zinafanyakazi kweli?? Amekueleza eneo cha kwanza kabisa ungecheki na ofisi zenu za huko Kyela ama ofisi ya serikali ya huko.
 
Ndugu mteja,
Soma hapo juu tumetoa maelezo ya kina hakuna nguzo ilioanguka wala kusababisha kifo
Afisa habari, kama tatizo limeshashughulikiwa, nikushauri uache kujibizana na wateja, walio na nguvu nyuma ya keyboard na wengi wetu tuna machungu juu ya uzembe mwingi wa shirika ndani ya maeneo yetu husika.

Kyela mjitafakari mchukue hatua stahiki, wateja waridhike.
Kiukweli nyuki waliowashinda siku 6 zilizopita mmeweza kuwadhibiti baada ya uzembe kutangazwa humu, nguzo iliyolala bado ni nguzo hatarishi kiusalama, hata kama haijadondoka.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Back
Top Bottom