Uzembe wa Idara ya Mawasilliano Ikulu na Mgogoro wa Ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzembe wa Idara ya Mawasilliano Ikulu na Mgogoro wa Ukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 12, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa natafuta namna moja ya kuelezea mgogoro ambao ninao na Idara hii nyeti ya Ikulu kwa muda mrefu. Mgogoro ambao tayari umeshawahi kujadiliwa hapa mara kwa mara lakini itoshe leo niuweke kwa maneno machache ili maana yake isije kupotea katika maneno mengi. NI mgogoro wa maono, uongozi, utendaji, uwajibikaji na zaidi ya yote ni mgogoro wa ukweli.

  Kuna uzembe uliokubuhu ambao unaakisi tu matatizo ambayo tunayo kwenye idara nyingine mbalimbali za seriklali.

  1. Tumelalamika miaka nenda miaka rudi sasa kwanini Ikulu haina mtandao mzuri kiintaneti wenye kusheheni taarifa mbalimbali za shughuli za Rais na hivyo kufanya kuwa chanzo cha kuaminika cha habari kwa vyombo vingine vya habari. Ninaamini wao ndio walipaswa kusimamia mambo hayo ya TEKINOHAMA hapo Ikulu ili kuhakikisha Ikulu ya Tanzania ina mtandao wa kisasa wa habari.

  Tovuti ya http://www.statehouse.go.tz haipo kwa muda mrefu sasa na ukienda Ikulu.go.tz utashangaa kuambiwa ni "Tanzania Building Agency"! na tumelalamikia hili kwa muda mrefu. Ili kuweza kuelewa ninachozungumzia angalia tovuti za Kenya - statehousekenya.go.tz, Uganda-statehouse.go.ug, au Rwanda (wanayo ya Paul Kagame, na ya Serikali).

  Kwanini vitu hivi ni muhimu? sababu moja ni kwamba vinakuwa ni kiungio cha haraka na cha uhakika katika ya wananchi na Rais wao na Ikulu yao. Badala ya wananchi kusubiri kila siku magazeti yaeleze nini Rais kafanya au nini kimetokea Ikulu leo au kitatokea kesho, Ikulu ingeweza kabisa kuwa na habari hizi kila siku na kwenye tovuti ambayo ni rahisi pia kukisiwa.

  Lakini kinachouudhi ni kuwa Idara hii inadaiwa kuwa imetengewa karibu dola laki mbili! kwa ajili ya kuendeleza tovuti ya Ikulu! Sasa miaka minne na hawa watu wameshindwa kufanya jambo dogo linalochukua masaa 24 tu?

  2. Tovuti ya Tanzania.go.tz; sasa baada ya hilo la hapo juu tatizo jingine ni ni tovuti rasmi ya serikali yetu, yaani ile ya anuani hiyo hapo juu. Japo tovuti hii imekuwa ikiwekewa taarifa mpya mara kwa mara lakini ni mojawapo ya tovuti zenye sura mbaya, mpangilio mbaya na inatumia teknolojia ya karibu miaka 15 ya nyuma katika mambo ya internet.

  NI sawasawa na watu wanaoisimamia wamefungwa katika kile kinachoitwa na rafiki yangu Kiranga kuwa ni time warp na hawawezi kutoka humo na matokeo yake wanatuzungusha mle mle. Lakini kinachoudhi zaidi ni kuwa tovuti hii ndio imegeuka kuwa ni tovuti ya Ikulu! NI kama hawa kina Salva, Premi (huyu mdada tena nina kesi naye nyingine.. na atajibu siku moja) wanaishi katika sayari nyingine hivi. Tovuti hii ya serikali ingekuwa inasimamiwa na Wizara ya Habari na utamaduni badala ya Ikulu! Ingekuwa ni mahali ambapo mtu akitaka kujua kuhusu Tanzania au mahali pa kuanzia kuhusu utendaji wa serikali ya Tanzania au vyombo vyake mbalimbali angeweza kwenda hapo.

  Halafu cha kukera zaidi badala ya kuwa na tovuti mbili zenye lugha mbili tofauti (Kiswahili na Kiingereza) basi wameamua kuchanganya tu mumo kwa mumo; kuna nyaraka za Kiingereza, zipo za kiswahili zote zimesambazwa ukurasa mzima bila kufuata mpangilio wowote wa kimantiki au maudhui. Wenyewe wanaita "Online Gateway"! my foot!

  3. Katika tovuti zao zote na habari zote zilizopo inaonekana hawa jamaa wa Ikulu (Mawasiliano) hawajawahi kukaa chini na kusema waanze kuweka kumbukumbu za taarifa mbali mbali za serikali yetu kwenye mtandao hasa taarifa ambazo zimekuwa declassified na ni haki ya wananchi kuzijua (nyingi zimepita tayari miaka 30 ya kawaida ya kuzizuia). Kuna mambo mengi ambayo wasomi wetu wangeweza kuyapata kwa kupata taarifa hizo mbalimbali za mwanzo wa jamhuri yetu, kwanini Ikulu isiziweke hadharani kwa mtandao ili kila mtanzania aweze kuzipitia?

  Inaonekana katika fikra zao historia ya Tanzania imeanza wakati wa Mkapa! Hebu angalia:

  - Picha zilizopo kwenye tovuti hiyo ya tanzania.go.tz kuhusu Rais ni za mwaka 2007!
  - Press Release waliyonayo (as of leo) ni ya Aprili 8, 2010. Ina maana kwa haraka haraka hawa jamaa hawajatoa press release kwa mwezi mzima. Kwa taifa kama la kwetu idara inatakiwa kutoa press release kila siku iendayo kwa Mungu ya nini Rais kafanya au nini kimetokea Ikulu.
  -Ukienda kwenye hotuba za marais wanazo kuanzia awamu ya tatu tu! Kwa maneno mengine awamu ya pili au ya kwanza haina nafasi katika Tanzania yao hii mpya. Hivi hawaoni kuwa historia yetu ni ya moja kwa moja tangu Nyerere hadi leo hii? Hata kama hawampendi Nyerere au kutaka kumkumbuka na hata kama wanaona Mwinyi hakuwafaa hawawezi kamwe kufuta historia zao. Tunahitaji watu pale ambao wataweza kuunganisha historia nzima kwa manufaa ya watanzania. Ingesaidia sana wanafunzi katika shule na vyuo vyetu wanaofanya utafiti mbalimbali au hata kwa waandishi na watafiti wa mambo mbalimbali.

  4. Kilichonitibua hata hivyo zaidi ni upotoshaji wa wazi unaofanywa na idara hiyo linapokuja suala la hotuba za Rais. Nimefuatilia kwa muda mrefu (tangu hotuba ile ya Kikwete kuhusu Muungano Bungeni) hadi sasa na nimegundua kuwa kina Salva, Premi, na wenzao wanaamini kabisa kuwa hotuba ya Rais ni ile iliyoandaliwa na siyo iliyotolewa!

  Katika mawazo yao potofu, ile hotuba iliyoandikwa ndiyo rasmi na ile iliyotolewa siyo rasmi na hivyo utaona kuwa katika tovuti ya Tanzania hotuba za Rais zilizowekwa siyo zote ndizo zilizotolewa na Rais. Wamekuwa wakiweka mtandaoni hotuba zilizopangwa kutolewa lakini SIYO zilizotolewa.

  Mfano mzuri ni hotuba ya mwaka jana ambapo Rais alizungumzia suala la asilimia 30 za bajeti kutafunwa na mafisadi wakati akifungua jengo la PCCB. Japo alizungumza hadharani hilo kwenye hotuba yao kina Salva hilo hakuna!

  Mfano mwingine ni hii hotuba ya juzi kwa Mbayuwayu, Watanzania wengi wanakumbuka mfano huu wa Kikwete na porojo nyingine alizozitoa. Ile ndiyo ilikuwa hotuba rasmi. Lakini kina Salva katika hekima yao ya milele wameamua kuweka hotuba ambayo Kikwete alikuwa aitoe!

  Ukweli ni kuwa hapa wanapotosha watu kwa sababu wanatuweka hotuba ambayo Kikwete mwenyewe hakuitoa. Wakati umefika waache hili, kama Rais wao hawezi kukaa makini na kusoma alichoandikiwa kama Obama basi ni watoe hotuba zake kama zilivyo, kama walivyokuwa wakimfanyia George Bush kwani hizo ndizo hotuba rasmi! Nakumbuka vizuri hili kwa sababu katika ile hotuba ya kutetea Muungano Kikwte alisema mengi sana na mengi yaliyokuwa yakushagaza zaidi lakini ndugu zetu hawa katika hekima yao isiyo na mwisho wakaonelea wasitoe hotuba ile bali watoe kile "alichopaswa" kusema.

  Ndugu zangu, kuna mgogoro wa mawasiliano na wakati umefika Salva na Premi waachie ngazi wawape watu wengine nafasi ya kufanya kazi ya mawasiliano ya Ikulu kwa uhakika, ufanisi na ukweli.
   
 2. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...Couldn't say it better......
   
 3. B

  Bobby JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji, once again thanx a lot na please usikate tamaa keep on saying though hawa watu wamegoma kabisa kutusikia.

  Mimi sijuwi ni nani aliyewaambia kwamba hii nchi ni ya kwao kwamba wanaweza kufanya watakavyo, lakini anyway ipo siku. Huu udhalilishaji wanaoendelea kutufanyia its too much sasa kweli jamani. Nchi gani hii inaendeshwa kihuni namna hii jamani?

  Please salva na wenzio tumechoka na hii aibu wandugu. Hivi kwani hamjuwi ni nchi nzima tunadhalilika na si kikwete peke yake? Mwanakijiji ametoa mifano ya nchi zinazotuzunguka wala hakwenda mbali tena maskini zote zimepata uhuru baada yetu na kiresources hakuna hata moja inayofika nusu yetu kwani sisi tunashindwa wapi jamani? No please do something enough is enough.
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu naomba unihakikishie hayo uliyoandika hapo juu kwa kumhusisha salva na premi moja kwa moja katika tuhuma zako , hao watu ni waajiriwa wana majukumu mengine yanayohusiana na mawasiliano lakini siamini kama majukumu yao yanahusiana na teknohama moja kwa moja kutokana na mkataba wao wa kazi eneo hilo , hili ni jukumu la idara zingine za kiserikali zinazotakiwa kusimamia masuala ya teknohama pamoja mawasiliano kwa ujumla sasa tunatakiwa kujua idara hii na wakuu wake ni wakina nani , kina nani walipewa kazi ya kusimamia masuala ya teknohama eneo hili .

  Masuala ya kuendesha tovuti yanahusiana na mambo mengi sana ndio maana huko nyuma kwanza tuliwahi kushauri kuwe na mfumo mmoja wa kueleweka wa tovuti zote za serikali nchini Tanzania hizo tovuti ziwe chini ya kitengo kimoja cha taasisi inayohusika na masuala ya teknohama nchini chini ya wizara ya mawasiliano kwa kushirikiana na kampuni zingine za sekta binafsi ambazo zinaweza kutoa changamoto kwenye masuala ya kiteknologia .

  Kwahiyo tukiwa na vitu kama hivyo mtu yoyote anayechaguliwa kuingia kwenye serikali na idara zake italazimika kuingia mkataba na hiyo taasisi kuu ya teknohama ambayo itakuwa na viidara vidogo kwenye kila wizara serikalini pamoja na sekta binafsi .

  Tukiwa na mipango mizuri naamini haya yote yanaweza kutimia lakini ni hadi pale tutakapoweka tofauti zetu pembeni na kuamua kufanya kazi kama taifa kwa maslahi yetu na vizazi vijavyo .

  Kuna watu wanafanya kazi kwa muda maalumu uongozi Fulani ukiisha basi nae anaacha kila kitu kwa wengine bila maelezo yoyote kwa hao wengine wanaokuja hii tabia tuache .
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ni nani, Msemaji Mkuu wa Ikulu ni nani? Na jukumu lao ni nini katika kutoa habari za Ikulu?


  Ushauri huo uliitoa wapi, lini, na umefanyiwa nini hadi hivi sasa na nani alitakiwa aufanyie kazi?

  Nani anapewa ushauri huu?

  mumbo jumbo! Huwezi kufanya kazi na utawala wa kifisadi mkafanya kazi kwa maslahi ya taifa!


  Ina maana Mkapa aliondoka bila kutoa maelezo ya kutosha kwa serikali ya JK?
   
 6. n

  nndondo JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Ndugu Yonomara naomba sana tubaki kwenye hoja ya mwanakijiji,

  Nadhani tunahitaji kujua namna ufanisi katika utendaji ulivyo na sio kuangalia sisi tunavyofanyakazi. Kwa maana hii Mwanakijiji kasema yote tatizo lisilojulikana mpaka leo kati ya Premi na Salva ni nani haswa mkurugenzi?

  Sasa kama idara ya kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu haiwezi kuwa juu ya mapungufu ya teknohama yanayo affect shughuli za idara yenyewe, sahau shughuzi za serikali kwa ujumla sasa kuna sababu gani ya hiyo kurugenzi kuwepo. Si haya yangefanywa tu na admini assistant wa ofisi ya masijala?

  Tusiogopane kwenye ukweli tuambiene na tujifunze toka kwenye best practices sio kwenye any practice. Hayo anayoyasema mwanakijiji ni tone tuna barafu kwenye bahari, hajarudi kutuambia makala za kuvuruga na kutarget watu wasiowapenda wao katika chama na serikali zinazotoka ofisini kwao n.k Mapungufu yako sisi tunayaona Jk Mwenyewe anayaona lakini route cause ni ile ile aliyosema Wole Soyinka, tatizo la Africa na kuwa na watu kwenye civil service wasio na uwezo na quality za kufanya hizo kazi.

  Kikwete ameamua kuliko kulitatua kwa kufanya kazi zao sasa hili la internet nadhani sasa ameambiwa atatafuta mtu ampe kazi ya kushughulikia internet ya ikulu, again pasipo kufuata utaratibu one of his close people of closer to his people.
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  May 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu mimi nimezungumzia masuala ya tovuti unapokuja kwenye masuala ya tovuti yale hayaingizwi tu unavyotaka ni tovuti inaandaliwa kuna kuwa na watu wa kuendesha tovuti sio kama unavyofikiria wewe kwahiyo inabidi kuandaliwa idara maalumu ya masuala hayo itakayoshugulikia tovuti zote za kiserikali , Ushauri kama huu niliwahi kuutoa kwenye mada moja kwenye www.ethinktanktz.org tembelea hapo tafuta sikumbuki ilikuwa kichwa cha habari gani ila ni miaka karibu 3 iliyopita , ushauri huu ni kwa ajili yako na wengine wanaosoma na kuandika kwa kushutumu serikali bila kuwa na taarifa za kutosha kama ulivyofanya hapo kwenye mada hii ni aibu kweli .

  Huo utawala wa kifisadi unausemea wewe mwenyewe huyu raisi ni wetu sote na serikali ni mimi na wewe lazima tuhakikishe tunafanya kazi pamoja kuhakikisha tunaitoa jamii yetu sehemu moja katika maisha kwenda nyingine bila kuangalia tofauti zetu za kidini , chama wala makundi yoyote hii ni nchi yetu sote haina hati miliki
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  May 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu naona hili suala linaendeshwa kisiasa zaidi na mwanakijiji pamoja na wewe hawataki kujua ukweli wala kuutafuta
   
 9. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukweli: Ikulu haina tovuti inayopasha habari jamii kuhusu mbali mbali yanayofanywa na Rais.
  Ukweli: Imekuwa na muda mrefu tangu suala la tovuti lianze kuongelewa

  Bw Maro kwa kuwa unaonekana kutetea sana hali iliyopo, naona utueleze kama Mkurugenzi wa Habari Ikulu hausiki, ni nani mhusika mkuu katika hili?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Hao watu wa kutengeneza hizo tovuti watakuwa chini ya nani? Yaani, wewe huoni umuhimu wa Idara ya Mawasiliano ya sasa hivi huko Ikulu kuwa na tovuti yao sasa hivi siyo mbele ya safari? Ni kitu kimewashinda ndani ya miaka minne hii iliyopita au kumi na tano tangu Mkapa awe madarakani?

  Ulipoutoa serikali imeufanyia kazi? Kwanini hawajafanyia kazi au raha iko kwenye kutoa ushauri tu?

  Taarifa gani wakati nimesema hapo juu kuwa mengine ninayosema yameshasemwa lakini wakati umefika ni lazima tuwabebeshe mzigo walioinama kubeba. Idara ya Mawasiliano Ikulu wana wajibu wa kuhakikisha mawasiliano ya Ikulu yanawafikia wananchi kwa ukweli, uhakika, na bila upotoshaji kama walivyofanya na wanavyoendelea kufanya hadi hivi sasa. Hili siyo suala la tovuti tu ni suala la substance ya tovuti hizo. Jambo hili kwako inawezekana likawa gumu kidogo kuelewa.

  Bahati mbaya watu wa Ikulu wanaamini kuwa nchi hii ni yao peke yao na sisi wengine ni wahanga tu wa utawala wao. Kama nchi hii ni yetu sote basi mimi ndio nimejenga hoja kuwa kina Salva na wenzie wanafanya kazi mbaya sana ya kuleta habari za Ikulu kwa wananchi?

  Hivi tovuti ya tanzania.go.tz inasimamia na idara gani ya serikali na ni kina nani wanaifanyia updates?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Ukweli gani sasa? onyesha kati ya niliyoyasema hapo juu lipi si la kweli?
   
 12. m

  mfundishi Member

  #12
  May 12, 2010
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jamii yetu haitafika kokote kama tukiendelea fumbia macho uozo
   
 13. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji

  Wakati mwingine huwa najiuliza labda na hili linahitaji wawekezaji?

  Tumepiga kelele toka 2007 kuhusu hili ila hakuna chochote

  Au ni moja ya masuala yanayohusu usalama wa Taifa?

  Imefikia wakati wa watu kuwajibika sasa.

  Kama wameshindwa kutengeneza tovuti ya ikulu waache kazi!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Siku za nyuma niliishawahi kuandika tunahitaji wawekezaji wa kuendesha Ikulu na nchi ya Tanzania kwa Jumla.....watu wakanirushia mawe!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Unajua kinachonisumbua ni "kitu gani wanaweza".. maana ukifirikia sana inabidi ujiulize hivi kuna kitu gani ambacho wanaweza kusema kwamba wanaweza kufanya? Na siyo kufanya tu hivi hivi lakini kufanya kwa ubora wa juu kabisa? tovuti siyo jambo gumu hivyo, kukusanya taarifa siyo jambo gumu, kuendesha tovuti siyo jambo gumu. Rais anapokwenda mahali wanamfuata na camera zao ambazo ni digital tena kuna maktaba ya video nyingi sana za tangu enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete, lakini hazipatikani, hazionekani, wao wakimaliza tu wanazihamisha, kuzilabel na kuziweka maktaba yao ambapo ni wao wenyewe wanajua zilipo na ni wao ndio wanaziangalia! Msomi wa Tanzania akitaka kufanya utafiki wa kutaka kujua Rais Mwinyi mwaka 1992 alisema nini tarehe gani hakuna anayekumbuka isipokuwa kurudi kwenye magazeti!
   
 16. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Naomba uwatumie ujumbe huu kwenye email yao ile ya yahoo..siikumbuki...mawasilianoikulu@yahoo.com ???

  Hivi namba ya Muungwana ni ile ile?kuna haja ya kumtumia ujumbe wa simu na kumueleza kuhusu hili na naamini kama asemavyo yeye ndiyo muajiri mkuu wa serikali basi atawafuta kazi..


  Kudos
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Ngoja nimtumie text mkuu na ninatuma hiyo kwa email uliyonipatia. Thanks
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Done!!!
   
 19. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tatizo kubwa ni kwamba wanataka kuiendesha nchi kigizagiza ili wanapo fanya maovu yao yasiweze kuwafikia wananchi, ikulu giza, raisi giza, katibu mkuu wa ikulu giza, washauri wa raisi giza, shida ni umbumbumbu walionao viongozi husika juu ya utandawazi, wapo kwa ajiri ya majungu na hotuba mbofu mbofu tu, kuwapiga mikwara wanchi pale wanapodai haki zao,

  pengine ikulu na nchi nzima ibinafisishwe, na kupewa muwekezaji wa kihindi
   
 20. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  unamaanisha kuwa inaongozwa na Nguvu za Giza?

  Salva should Go na sitafute Mchawi hapa
   
Loading...