Uzembe TANESCO: Mikoa minane kuingia kwenye mgawo wa umeme kuanzia Jumapili

Makaayamawe

JF-Expert Member
Feb 21, 2009
341
9
Mikoa minane kuingia kwenye mgawo wa umeme kuanzia Jumapili
Na Boniface Meena

SHIRIKA la umeme nchini(Tanesco), limeeleza kuwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Singida, Mara na Tabora itaingia kwenye mgawo wa umeme kuanzia kesho hadi Julai 13.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Meneja Mawasiliano wa shirika hilo, Badra Masoud, ameeleza kuwa shirika hilo, litasimamisha shughuli za ufuaji wa umeme wa mtambo wake wa maporomoko wa New Pangani, kwa ajili ya marekebisho makubwa.

Kutokana na marekebisho hayo, Masoud ameeleza kuwa umeme utapungua kwa megawati 68 katika gridi ya taifa, hivyo mikoa hiyo itaingia katika mgawo wa umeme kwa takriban saa nne.

Masoud alieleza kuwa, kutokana na sababu hiyo nishati ya umeme inayopelekwa Kaskazini Magharibi mwa gridi ya taifa, italazimika kupitia katika njia kuu ya umeme Mtera mkoani Dodoma, ambayo iko katika hali ya kuzidiwa katika usafirishaji wa nishati ya umeme.

Mtambo huo, utazimwa kuanzia kesho hadi Julai 13 mwaka huu.
 
Kwa jinsi utendaji wa Serikali yetu na TANESCO ulivyo wa kizembe, suala la kukosesha mamilioni ya watu na viwanda umeme kwa mwezi mzima, limechukuliwa kama ni jambo la kawaida tu. Kama vile mtu anavyoshughulikia matengenezo ya gari binafsi.
  1. Hivi kweli nchi inayozalisha gesi inashindwa kuwa na umeme wa dharura wakati matengenezo ya mitambo ya Hydro yanapofanyika? Au hii ndio itatumika kuialika tena DOWANS?
  2. Je Tanesco wanaweza kuufahamisha umma hasara itakayopata na itakayowapata watumiaji umeme kwa hatua yao hii isiyo ya kitaalamu?
 
inachukuliwa jambo la kawaida kwa sababu tayari wameshasema kuwa kelele za mlango haziwazuwii kulala
tutasema wee ............lakini wao msimamo wao ule ule
 
Siku Tanesco na serikali ya Tz vinapelekwa mahakamani, kuku mtetea atawika! maana nadhani imefikia muda muafaka wa kuvipileka mahakamani kutokana nu ujinga vinavyoendeleza.
 
Back
Top Bottom