Uzee wanijia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzee wanijia

Discussion in 'Entertainment' started by kasimba123, Jul 1, 2010.

 1. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Uzee kitu adhimu, huo ninauingia
  Ujana sasa adimu, Shabani aliusia
  Maungoni mwangu humu, uzee unanijia,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Mbali ninamuachia, rafiki yangu ujana,
  Miaka inakimbia, ya leo siyo ya jana,
  Nabaki nakumbukia, nilipokuwa kijana
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Shabani aliandika, kaulilia ujana,
  Ni vipi unamtoka, kashindwa kuung’ang’ana,
  Meno yalimdondoka, na nguvu tena hamna,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Taratibu waingia, uzee wabisha hodi,
  Siwezi kuukimbia, hata niwe mkaidi
  Hata nikitukania, ndivyo napigwa baridi,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee

  Mvi sasa zanijia, nimejaribu kung’oa
  Kidevu zasalimia, na miye nazichomoa,
  Nikitoa zazidia, nami nazidi kutoa!
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Mapensi nayaachia, na macheni ya shingoni,
  Hereni nilivalia, kwenye sikio jamani,
  Mwendo nilibadilia, nilivyonesa njiani,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Niliwapata mademu, tena wengine kwa zamu,
  Nikaitwa mtaalamu, wa mambo yale matamu
  Sasa yanitoka hamu, nanyimwa hata salamu!
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Nilenda nilipotaka, wasiponitaka nilenda,
  Sikuwa na hata shaka, ati mtu kunidunda,
  Leo naogopa paka, ninavutwa kama punda,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Mwendo wa kudemadema, nikishika natetema,
  Uso umenikunjama, natembea nikihema,
  Magoti nayo yauma, uzee si lele mama!
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Kumbe maisha ni hivi, uzee haukwepeki,
  Ninazikubali mvi, hata kama sizitaki,
  Uzee siyo ugomvi, ujana haushikiki,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Kweli nilifurahia, enzi zile za ujana,
  Kamwe sintoyarudia, yalopita naagana,
  Uzee nakumbatia, kwani lingine hakuna,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

  Nasubiri wajukuu, nione na vitukuu,
  Nakunja miguu juu, na mshukuru Mkuu
  Kuona umri huu, enzi hizi ni nafuu,
  Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!
   
 2. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  we si shairi la mwanakijiji hilo sasa unalipost kama lako,...lol
   
 3. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  He kumbe!!!:A S tongue:
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  labda ndio katika kuhusudu huko! nimemsamehe
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  Busted lol!
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Husuda ni kitu kibaya mtu kuwa nayo.
   
 7. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  shairi hili nimelipost kwa sababu yaliyoandikwa humu yananifanya kila mara nilisome shairi ijapokuwa sikuomba ruhusa kwa mwenyewe lkn shukrani kwa msamaha
   
 8. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  msemakweli achaguliwa kuwa diwani.,..
   
 9. p

  phenomena Member

  #9
  Jul 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He kumbe
   
 10. M

  Mundu JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Diwani ashika tama
   
Loading...