Uzee si kashfa, uzee si laana

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,401
1,604
Hii ni aina mpya ya ubaguzi ambayo imekuwa ikizidi kushamiri kadri siku zinavyozidi kwenda, kiufupi ni kwamba mtu hatakiwi kubaguliwa kwa namna yoyote ile iwe umri, mahali anapotoka, jinsia, dini wala kabila..... nk

Kwa bahati mbaya, Chama Cha Mizigo(CCM) wameanza kubagua wazee katika chama chao. Kumekuwa na kauli ambazo zinaanzia kwa mwenyekiti wa chama mpaka watendaji wake kwamba wazee hawatakiwi kuwa maraisi, sijui ni katiba ipi wanayoitumia wenzetu.?

Baba Mwanaasha alisema muda huu anatakiwa raisi kijana, January Makamba anasema kama umezaliwa kabla ya 1961 sahau kuhusu uraisi. Kauli kama hizo na nyingine zinazofanana na hizo zinazidi chochea matabaka baina ya wazee na vijana.

Kiufupi ni kwamba, mtu yeyote anayeamini kuwa kijana pekee ndiye anayeweza kuwa raisi mtu huyo ni mpuuzi tena sana na si mtu wa kuachwa hata kidogo. Imagine, ccm vijana wanao wasema wao ni kina mwigulu nchemba, livingstone lusinde, nape nnauye. Hivi kwa akili ya kawaida mtu kama Livingstone unaweza kumpa uraisi?

Unaweza ukawa na kijana na asifanye kazi akaishia kutembea na wake za watu na ukawa na mzee akawa mchapakazi, CCM angalieni ni nani anayefanyakazi, kiongozi mwajibikaji na si kutaka kumchagua mtu kwa kigezo cha umri huo ni ubaguzi na haufai kufumbiwa macho. Dhambi ya ubaguzi inawatesa sana CCM.

UZEE SI KASHFA, UZEE SI LAANA.

Nawasilisha.
 
Sijaelewa...kuna masuala mawili unachanganya hapa...Uzee na Urais,nadhani unaweza kuwa mwathirika katika mojawapo...Ila pole msemaji wa Chama atakuja kutoa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom