Uzazi wa mpango: Kipimo kipi ni sahihi katika kupima idadi ya watoto wa kuwa nao?

Jan 15, 2013
77
27
Katika swala la uzazi wa mpango; walio katika mahusiano wanashauriwa kuwa na idadi ya watoto ambao watamudu kuwalea.

Kipimo kipi ni sahihi katika kupima idadi sahihi ya watoto wanaopaswa kuwanao?
  1. Kipato chao (Fedha),
  2. Umri wa wao (wazazi),
  3. Tofauti ya umri kati ya mtoto mmoja na anaefuatia,
  4. Gharama za maisha (living standard).
Kipimo sahihi ni kipi?

MJUZI NITOE UKUNGU KATIKA FIKRA
 
Kuwa na watoto wengi kuna punguza uwezo wa kufanya mambo mengine kama binadamu. Muda Wote unakuwa unatafuta Pesa ya kuikimu family. Family nyingi zipo katika umasikini Mkubwa kutokana na kuwa na family kubwa. Mfano unakuwa na watoto wanne alafu una kazi ya maana, una insurance ya maisha na vitu vingine ikitokea ugonjwa mdogo unampoteza mtu kwa sababu ya upungufu wa kipato wa kuikimu family. Hali ni mbaya sana vijijini, mtu ana family kubwa awezi kuimudu ni shida mwanzo mwisho matokeo yake ni family inakuwa na utapia mulo na matatizo mengi tuu
 
Katika swala la uzazi wa mpango; walio katika mahusiano wanashauriwa kuwa na idadi ya watoto ambao watamudu kuwalea.

Kipimo kipi ni sahihi katika kupima idadi sahihi ya watoto wanaopaswa kuwanao?
  1. Kipato chao (Fedha),
  2. Umri wa wao (wazazi),
  3. Tofauti ya umri kati ya mtoto mmoja na anaefuatia,
  4. Gharama za maisha (living standard).
Kipimo sahihi ni kipi?

MJUZI NITOE UKUNGU KATIKA FIKRA
- Je unajua kuwa masikini na wasio enda shule ndo huwa wanazaa watoto wengi sana?
- Je unajua kuwa wananchi wa kijijini ndo huzaa watoto wengi zaidi ya wamjini?
- Je wajua kuwa sisi waisilamu tunazaa watoto wengi zaidi?
- Je unajua wasukuma ndio wanaongoza kwa kuzaa idadi kubwa ya watoto?
 
Hata kama una uwezo kiasi gani watoto standard in 3 tu kama Obama lakini mkiwa hamna uwezo mmoja tu anatosha angalia matajiri wote watoto wao wamezidi sana ni watatu tu, tatizo sio uwezo was kuwalea lakini mama naye anatakiwa amantain umbo lake msichana akianza kuzaa akiwa ma miaka 24 au chini ya hapo asipoendelea kuzaa baada ya kufikisha miaka 30 anapendeza sana na huwezi kuamini kama ana watoto unaweza kudhani ni wadogo zake. Nawasilisha.
 
Mkuu nadhani ni kauli mbiu hii "kuwa na watoto ambao utawamudu kuwalea", hawa hawakuwa straight katika hili kama wewe, "Standard kwa tajiri wa 3, asie na uwezo wa 2" kutokuwa kwao straight ndio msingi wa thread hii... kipimo kipi wanapaswa kutumia walio katika uhusiano ikiwa wanamudu au hawamudu?
 
Nadhani angalia kipato chako. Kazi ulonayo ni ya kudumu?? Je ukiazaa 2 utawamudu? Je watatu?? Jiulize ukiona una vyanzo vya mapato stable unaweza zaa hata 5. Watoto ni neema na baraka kutoka kwa Mungu ila pia sio unazaa tuu kuja kuwatesa kwa kushindwa kuwahudumia. Zamani wazazi wetu walitufyatua tuu kwa sbb magonjwa hayakua mengi kama sasa na gharama za maisha hazikua kubwa kama leo. Pia ardhi ilikua na rutuba ya kuweza kulima na kupata chakula cha kulisha familia leo hali hyo haipo. Tuzae kwa mpango
 
mmoja au wawili wanatosha.Duniani kuna jipya gani ambalo litakufanya uwalete watoto waje washangae?!!? hata usipozaa ni poa tu ...usawa wenyewe huu matukio mengiii...kufa kupo njenje.Mxuuw!
 
mmoja au wawili wanatosha.Duniani kuna jipya gani ambalo litakufanya uwalete watoto waje washangae?!!? hata usipozaa ni poa tu ...usawa wenyewe huu matukio mengiii...kufa kupo njenje.Mxuuw!
aisee naona hutaki zaa kwann lakin
 
Kipato chako ndo msingi vingine ni kujiongeza tu,kipato kama kinaruhusu zaa hata 100 PERMISSION GRANTED
 
Back
Top Bottom