WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Katika mada moja kuna maoni kwamba First Lady wetu afanye kazi ya ziada kupunguza kero ya kulala chini ( adha iliyowahi kumpata yeye mwenyewe huko nyuma ) na manyanyaso ya manesi kwa wanawake wanaoenda kujifungua.
( Ushawishi wake kwa MWENYE NCHI..SIJUI MWAYA!)
Hizi ni hisia na maoni halali kabisa.
NB: First ladies wa third world na michango yao katika kutatua matatizo ya kitaifa ni tofauti na First ladies wa ulimwengu wa kwanza.Kuna hata kiongozi wa kuheshimika aliwahi kusema kuwa " rais hawezi kushauriwa na mkewe" - japo sikubaliani na usemi huu, ni kielelezo cha hali halisi cha viongozi wengi wa kiafrika. Pillow talk can work wonders but not always!
Twende mbele na turudi nyuma.....Cha kujiuliza, na hasa kwa wale ambao kidogo wana ahueni ya maisha, uzazi salama ni jukumu la nani? Nimeuliza kule kwenye mada - je hadi mama anajifungua - miezi tisa toka awe mjamzito, kuna matayarisho gani au ni mpaka mtu asikie uchungu aanze kukimbilia kwenye hospitali AMBAKO HANA UHAKIKA NA HUDUMA?
Tumewahi kushuhudia wanawake wakienda hospitali huku wakijua kabisa hiyo hospitali haipokei mzazi kama hana rufaa kutoka hospitali za wilaya..na bado wanalazimisha kwenda huko... hii hupelekea kuongeza mzigo na kufanya hadi wauguzi wawe na lugha mbaya. Sitetei wauguzi bali nasema hali halisi.
Mume naye huwa anachangia vipi katika kuandaa ujio wa mtoto? Au akishapanda mbegu basi kazi yake imekwisha?Leteni hoja ili tupate kulielewa vizuri tatizo hili.