Uzazi salama/safe motherhood - jukumu kuu ni la nani?

WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Messages
5,465
Points
0
WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined May 30, 2008
5,465 0
Katika mada moja kuna maoni kwamba First Lady wetu afanye kazi ya ziada kupunguza kero ya kulala chini ( adha iliyowahi kumpata yeye mwenyewe huko nyuma ) na manyanyaso ya manesi kwa wanawake wanaoenda kujifungua.
( Ushawishi wake kwa MWENYE NCHI..SIJUI MWAYA!)
Hizi ni hisia na maoni halali kabisa.

NB: First ladies wa third world na michango yao katika kutatua matatizo ya kitaifa ni tofauti na First ladies wa ulimwengu wa kwanza.Kuna hata kiongozi wa kuheshimika aliwahi kusema kuwa " rais hawezi kushauriwa na mkewe" - japo sikubaliani na usemi huu, ni kielelezo cha hali halisi cha viongozi wengi wa kiafrika. Pillow talk can work wonders but not always!

Twende mbele na turudi nyuma.....Cha kujiuliza, na hasa kwa wale ambao kidogo wana ahueni ya maisha, uzazi salama ni jukumu la nani? Nimeuliza kule kwenye mada - je hadi mama anajifungua - miezi tisa toka awe mjamzito, kuna matayarisho gani au ni mpaka mtu asikie uchungu aanze kukimbilia kwenye hospitali AMBAKO HANA UHAKIKA NA HUDUMA?

Tumewahi kushuhudia wanawake wakienda hospitali huku wakijua kabisa hiyo hospitali haipokei mzazi kama hana rufaa kutoka hospitali za wilaya..na bado wanalazimisha kwenda huko... hii hupelekea kuongeza mzigo na kufanya hadi wauguzi wawe na lugha mbaya. Sitetei wauguzi bali nasema hali halisi.
Mume naye huwa anachangia vipi katika kuandaa ujio wa mtoto? Au akishapanda mbegu basi kazi yake imekwisha?Leteni hoja ili tupate kulielewa vizuri tatizo hili.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,526
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,526 2,000
Hapana kuna jambo nitalisema litazua mgogoro.. ngoja wengine waje kwanza.. Mada nzuri sana hii kwani inanigusa.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,526
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,526 2,000
WoS,

Jukumu la uzazi salama huangukia jamii nzima na si mzazi mmoja au wazazi wawili tu. Kuweza kuelewa hili kwa namna ya pekee naomba niwe mwanafalsafa kidogo. Watoto huzaliwa katika jamii na ni kutoka katika jamii hiyo hukua na hatimaye wao nao huzaa watoto na kizazi kinaendelea kuelekea umilele. Kwa kadiri jamii inavyojiandaa kupokea watoto ndivyo hivyo hivyo inapokea watoto na nguvu yake ya uwepo hutegemea uzazi na malezi ya watoto hao.

Endapo kwa mfano, watoto wengi hufa wakiwa wachanga kwa sababu ya miundo mbinu mibaya, magonjwa ya utotoni, au matatizo ya uzazi ambayo yangeweza kuondolewa au kupunguzwa basi jamii inajikuta inapoteza kizazi au watoto wengi katika jamii hiyo. Lakini upande mwingine ni kuwa hata wale wenye kunusurika na matatizo ya utotoni wanaweza kujikuta bado wana matatizo katika maisha yao kwa sababu ya matatizo ya utotoni, mfano mzuri ni polio ilivyokuwa inatuathiri sana kabla ya hatimaye kufanikiwa kuindoa.

Hebu nilioneshe hili kidogo:

Kwa Tanzania mortality rate ya watoto kwa takwimu za hivi karibuni 2008 ni watoto 104 kati ya 1000 hufa kabla hawajatimiza miaka mitano. Katika Marekani kwa mwaka huo huo ni watoto 8 na kwa Australia ni 6. Nchi zote za Ulaya Magharibi ziko kwenye single digits. Unaweza kuangalia mlingano zaidi hapa: Child Mortality

Sasa, utaona kuwa jamii zilizoendelea vile vile ndizo zenye mazingira salama ya uzazi! Naweza kuchukua vipimo vingine mbalimbali kuonesha kuwa jamii ambazo hazijaendelea zinajionesha vile vile kwenye masuala ya uzazi salama. Huwezi kuwa na jamaa iliyoendelea halafu ukawa na uzazi mbovu!

Nchi hizi zilizoendelea zimeelewa kile ambacho sisi hatutaki, tumeshindwa na hatuna mpango wa kukielewa. Huwezi kuwa na taifa la kisasa bila kuwa na mambo ya kisasa katika mazingira ya uzazi! Wenzetu wameelewa kile ambacho natumaini nitapata muda kukimalizia ninakiita "Nadharia Mpya ya Maendeleo kwa Kupokezana Vizazi". Tukielewa nadharia hii tutaona kuwa kizazi kilichopo kisipoandaa kizazi kinachokuja au kizazi kinachoondoka kisipoandaa kizazi kinachojiandaa kutawala basi mbele ni vurugu kwa sababu kila mtu anajifanyia ya kwake tu.

Matokeo yake ni kuwa jukumu la uzazi salama anaachiwa mama kana kwamba katika jamii nzima yuko peke yake. Matokeo yake kina mama wanajikuta zaidi ya kuwa na jukumu kubwa la kuzalisha mali vile vile wanazidi kukandamizwa na jukumu la uzazi na malezi.

Hili linatuleta kwenye swali lako la mwisho. Kina Baba wako wapi? Jamii zetu bado ni jamii za mfumo dume, bado wanaume bado hawajazama sana katika suala zima la uzazi na hasa katika kufuatilia mazingira ya uzazi wa watoto wao.

Mfano mzuri ni hizo hospitali za Mwananyamala na Temeke; kama wanaume wangeona kuwa wake au wanawake wao wanazalia katika mazingira mabaya wangelalamika na hata kuandamana dhidi ya serikali mbovu! Wanaume wangekuwa wanajali uzazi salama wa watoto wao wasingechagua madiwani wale wale na kwa hakika wasingekaa kuona wake zao wanalala chini baada ya kujifungua!

Ndio maana ninaamini inatupasa kabisa kina mama kuingia kuongoza mabadiliko tunayoyataka. Kina baba tumeshindwa.
 
M

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2010
Messages
15,203
Points
2,000
M

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2010
15,203 2,000
Katika mada moja kuna maoni kwamba First Lady wetu afanye kazi ya ziada kupunguza kero ya kulala chini ( adha iliyowahi kumpata yeye mwenyewe huko nyuma ) na manyanyaso ya manesi kwa wanawake wanaoenda kujifungua.
( Ushawishi wake kwa MWENYE NCHI..SIJUI MWAYA!)
Hizi ni hisia na maoni halali kabisa.

NB: First ladies wa third world na michango yao katika kutatua matatizo ya kitaifa ni tofauti na First ladies wa ulimwengu wa kwanza.Kuna hata kiongozi wa kuheshimika aliwahi kusema kuwa " rais hawezi kushauriwa na mkewe" - japo sikubaliani na usemi huu, ni kielelezo cha hali halisi cha viongozi wengi wa kiafrika. Pillow talk can work wonders but not always!

Twende mbele na turudi nyuma.....Cha kujiuliza, na hasa kwa wale ambao kidogo wana ahueni ya maisha, uzazi salama ni jukumu la nani? Nimeuliza kule kwenye mada - je hadi mama anajifungua - miezi tisa toka awe mjamzito, kuna matayarisho gani au ni mpaka mtu asikie uchungu aanze kukimbilia kwenye hospitali AMBAKO HANA UHAKIKA NA HUDUMA?

Tumewahi kushuhudia wanawake wakienda hospitali huku wakijua kabisa hiyo hospitali haipokei mzazi kama hana rufaa kutoka hospitali za wilaya..na bado wanalazimisha kwenda huko... hii hupelekea kuongeza mzigo na kufanya hadi wauguzi wawe na lugha mbaya. Sitetei wauguzi bali nasema hali halisi.
Mume naye huwa anachangia vipi katika kuandaa ujio wa mtoto? Au akishapanda mbegu basi kazi yake imekwisha?Leteni hoja ili tupate kulielewa vizuri tatizo hili.
WOS whether wanawake mtasema ni mfumo dume au la ni kweli kuwa Rais wa nchi hawezi kushauriwa masuala nyeti ya nchi na usalama na mkewe maana ushauri wa mkewe hauna security na hauna pa kuupeleka. Namfahamu kiongozi aliyesema hayo maneno na wewe ila kwakuwa hujamtaja na kwa heshima yake uko aliko nami nisimtaje ila namuunga mkono 100%
 
WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Messages
5,465
Points
0
WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined May 30, 2008
5,465 0
WoS,

Jukumu la uzazi salama huangukia jamii nzima na si mzazi mmoja au wazazi wawili tu. Kuweza kuelewa hili kwa namna ya pekee naomba niwe mwanafalsafa kidogo. Watoto huzaliwa katika jamii na ni kutoka katika jamii hiyo hukua na hatimaye wao nao huzaa watoto na kizazi kinaendelea kuelekea umilele. Kwa kadiri jamii inavyojiandaa kupokea watoto ndivyo hivyo hivyo inapokea watoto na nguvu yake ya uwepo hutegemea uzazi na malezi ya watoto hao.

Endapo kwa mfano, watoto wengi hufa wakiwa wachanga kwa sababu ya miundo mbinu mibaya, magonjwa ya utotoni, au matatizo ya uzazi ambayo yangeweza kuondolewa au kupunguzwa basi jamii inajikuta inapoteza kizazi au watoto wengi katika jamii hiyo. Lakini upande mwingine ni kuwa hata wale wenye kunusurika na matatizo ya utotoni wanaweza kujikuta bado wana matatizo katika maisha yao kwa sababu ya matatizo ya utotoni, mfano mzuri ni polio ilivyokuwa inatuathiri sana kabla ya hatimaye kufanikiwa kuindoa.

Hebu nilioneshe hili kidogo:

Kwa Tanzania mortality rate ya watoto kwa takwimu za hivi karibuni 2008 ni watoto 104 kati ya 1000 hufa kabla hawajatimiza miaka mitano. Katika Marekani kwa mwaka huo huo ni watoto 8 na kwa Australia ni 6. Nchi zote za Ulaya Magharibi ziko kwenye single digits. Unaweza kuangalia mlingano zaidi hapa: Child Mortality

Sasa, utaona kuwa jamii zilizoendelea vile vile ndizo zenye mazingira salama ya uzazi! Naweza kuchukua vipimo vingine mbalimbali kuonesha kuwa jamii ambazo hazijaendelea zinajionesha vile vile kwenye masuala ya uzazi salama. Huwezi kuwa na jamaa iliyoendelea halafu ukawa na uzazi mbovu!

Nchi hizi zilizoendelea zimeelewa kile ambacho sisi hatutaki, tumeshindwa na hatuna mpango wa kukielewa. Huwezi kuwa na taifa la kisasa bila kuwa na mambo ya kisasa katika mazingira ya uzazi! Wenzetu wameelewa kile ambacho natumaini nitapata muda kukimalizia ninakiita "Nadharia Mpya ya Maendeleo kwa Kupokezana Vizazi". Tukielewa nadharia hii tutaona kuwa kizazi kilichopo kisipoandaa kizazi kinachokuja au kizazi kinachoondoka kisipoandaa kizazi kinachojiandaa kutawala basi mbele ni vurugu kwa sababu kila mtu anajifanyia ya kwake tu.

Matokeo yake ni kuwa jukumu la uzazi salama anaachiwa mama kana kwamba katika jamii nzima yuko peke yake. Matokeo yake kina mama wanajikuta zaidi ya kuwa na jukumu kubwa la kuzalisha mali vile vile wanazidi kukandamizwa na jukumu la uzazi na malezi.

Hili linatuleta kwenye swali lako la mwisho. Kina Baba wako wapi? Jamii zetu bado ni jamii za mfumo dume, bado wanaume bado hawajazama sana katika suala zima la uzazi na hasa katika kufuatilia mazingira ya uzazi wa watoto wao.

Mfano mzuri ni hizo hospitali za Mwananyamala na Temeke; kama wanaume wangeona kuwa wake au wanawake wao wanazalia katika mazingira mabaya wangelalamika na hata kuandamana dhidi ya serikali mbovu! Wanaume wangekuwa wanajali uzazi salama wa watoto wao wasingechagua madiwani wale wale na kwa hakika wasingekaa kuona wake zao wanalala chini baada ya kujifungua!

Ndio maana ninaamini inatupasa kabisa kina mama kuingia kuongoza mabadiliko tunayoyataka. Kina baba tumeshindwa.

Mwanakijiji,
Asante sana kwa kuchangia mada hii ambayo wengi hawajaona umuhimu kutoa mawazo yao.
Kuwa hakuna hata wachangiaji ni kielelezo tosha kwamba suala la uzazi na malezi ya watoto kijamii huchukuliwa kama ni swala lisilohitaji mjadala, swala la wahusika wawili - aliyesababisha mimba na anayebeba mimba.Hivyo kinadharia naweza kabisa kusema tena kwa uhakika kuwa assertion yako ya mwanzo kuhusu uzazi salama ni jukumu la jamii ni nadharia zaidi kuliko uhalisia wa hali ilivyo au inavyotakiwa iwe.

Jamii haijiingizi sana kwenye mchakato mzima kuanzia mimba hadi kuzaa.WATAJIHUSISHA KWENYE SHEREHE mbalimbali zinazomhusu MTOTO, ambapo ni kula na kunywa na siyo jukumu.CELEBRATIONS!

Umezungumzia uhusiano baina ya vifo na siha ya watoto na Uzazi kupitia malezi. Nakubaliana nawe kabisa.Lakini hata kabla ya kwenda kwenye IMR ( Infant Mortality Rate), ningependa tumlenge mama kwanza - ambapo maternal mortality rate kwa Tanzania inatisha.Katika kila wanawake 100,000 wanojifungua, ni wanawake zaidi ya 500 hufariki dunia.Hii siyo idadi ndogo ya kupuuzia.Kumbuka hakuna anayekuja duniani bila kupitia mwanamke. Kwa maana hii basi hao 500+ wanaopoteza maisha wakijifungua ingeweza ikawa mama yako ewe msomaji, dada yako,binti yako au mkeo - watu wa karibu mno na wewe. Fikiria ni huzuni iliyoje kumpoteza mpendwa wako kwa vile tu anatimiza wajibu wake wa kuleta kiumbe kipya dunia. Uzazi ni kitendo natural na ni jukumu la mwanamke na jukumu linapotekelezwa basi tunatarajia ushindi au matokeo mazuri na siyo kifo. kwa wenzetu nchi zilizoendelea
kama America, it is pretty rare for women to die from complications of birth!! Wao Maternal Mortality Rate yao hazidi wanawake 12 kwa kila 100,000! na wengi kifo kinatokana na haswa excessive bleeding baada ya kujifungua au uambuziko hasa kwa wanapofanyiwa C-Section.

Inasemekana na wataalamu watanisahihisha hapa - uzazi haupaswi kuleta kifo! Its a natural process na Mungu hakutuumba tuzae ili tufe kama alivyofanya kwa viumbe vingine.Nyuki dume anapo mate na jike huishia kufa maana ndivyo ilivyoumbwa.Kadhalika Praying mantis naye hivyo hivyo. Wako wanyama au ndege ambao kitendo cha kuzaa tu hummalizia life span.

Vidokezo vifuatavyo vinaweza kutuogoza kujua nani anapaswa kuwajibika wakati gani:
1.Uzazi salama unaanza kabla ya mimba kutungwa - afya ya mama, je anao umri unaostahili? Wataalam wanashauri mwanamke azae kati ya miaka 22-35.Isiwe kabla au baada maana hatari huongezeka na umri mdogo (viungo vya uzazi bado havijawa tayari) umri mkubwa hatari za complications kama kifafa cha mimba, HBP, na pia kutegemeana na kizazi kilivyo - haemorage/kuvunja damu nyingi na hii inaweza kupelekea kuongezwa damu.Damu haiko salama hata kama imepimwa maana kuna window period ambapo virusi vya ukimwi haviwezi kuonekana.Wako wanawake wamekuja kupoteza maisha kwa UKIMWI baada ya kuongezewa damu iliyodhaniwa ni salama!
Je wanaume au jamii huchangia vipi kulinda au kumhatarishia maisha mwanamke kabla ya kutungwa mimba?

2. Mimba ikishatungwa - je wahusika baba na mama watarajiwa wanapokea vipi? Je ndio kupigana chenga - ubishani kukana mimba; Je, watu wanafurahia matokeo ya kitendo walichoshirikiana hadi mimba ikatungwa? Kama jibu ni hapana - basi ndio hatari nyingine huingia- attempts za kuficha mimba na kushindwa kujitunza mama mjamzito; attempts za kutoa mimba ambapo vifo huongezeka; magonjwa ya uambukizo pale zoezi linapofanyika; Wakati mwingine wanaume hushinikiza wanawake watoe mimba hata wale walioko kwenye ndoa!
Tuchukulie kuwa mimba haijakataliwa - je wanaume wanashiriki vipi kulea mimba?Wanasindikiza wake zao klinik? wanawatunza kwa lishe bora? wanawapa faraja na matumaini?- Ikiwa jibu ni hapana basi usalama haupo - mama atakuwa na afya mbaya, hana lishe nzuri, kama anasononeshwa na manyanyaso hii huathiri na huweza kusababisha pressure ikapanda -( wanawake wengi hulalamikia waume kujihusiha sana na wanawake wa nje na kunyayasa mke! )

Wakati wa mimba mwanamke huweza kuwa na complications nyingi - wanaume hushiriki vipi kuwasaidia wake zao?

3. Kujifungua
Mwanaume mwenye kujali atakuwa bega kwa bega kufuatilia maendeleo ya mimba.Ataangalia kadi la mkewe na kuona vidokezo vyote vya hatari hata kabla siku ya kujifungua haijawadia.Je kwa kipindi hicho, anajiandaa vipi kumsaidia mkewe?

Ndio maana nikasena tusilalamike au kulaumu tu maana dalili nyingi mbaya huonekana mwanzoni kabisa na ndipo mwanaume kama alijisumbua kujua angeweza kufanya maandalizi.Jamii pana hata wazazi hawawezi kuja kuingilia wasaidie.Wao ni line ya pili ya intervention.

Hebu tuendelee na majadiliano .... mimi bado naona jukumu kuu ni la wawili waliosababisha mimba kuwepo.
 
WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Messages
5,465
Points
0
WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined May 30, 2008
5,465 0
Asante Companero..huo ni uhalisia.... but.....
hujachangia mawazo yako wewe.
 
Companero

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Messages
5,506
Points
1,500
Companero

Companero

Platinum Member
Joined Jul 12, 2008
5,506 1,500
WOS mawazo gani tena nichangie, kila siku tunachangia mawazo yaleyale tu, wakati suluhisho sote tunalijua - unayakumbuka mawazo haya:

SOME OF MUHALLEY'S FINAL CALL(S) TO ACTIVISTS

ON THE PAIN OF MATERNAL MORTALITY

Thanks for bringing the very touching pictures which remind me the past situation. My sister in law was admitted in a martenity ward two years ago (the name of hospital withheld) and I was to visit her and help out when necessary. I found her in a very bad labour pain and the way I saw her I thought she was about to give birth in any minute then I called the Nurse on duty and she said asubiri bado nakunywa chai bwana kwani yeye ndio anaumwa sana kuliko wengine. Then I called her again because I was so scared as I saw my sister in law losing consciousness and again she told me she doesn't want people to disturb her oftenly so go I will come. Then, furiously, I took her cup of tea and put it aside and I took her hand and I said 'you are going to help her or do you a piece of work with you'. With anger I was about to slash her face then she read my face but unfortunately the baby was dead and the mother was unconscious, they had to oparate her because the labour stopped.​

The situation like that we saw in the pictures is all over in most of the hospitals in Tanzania. I think you will agree with me. And the motivating working enviroment will help one to think prOperly, be creative and kujenga moyo wa huruma especially for those who are working to help other people's life. i dont blame the nurse for the behavior 100% but also the situation contributed a certain percent. The equipment which is a very cruicial part for the hospital to help out patients professionally - now nurses and doctors are improvised with some of the old or broken equipment, how can lives of people be improvised?????​

For the situation like the one I witnessed myself there are a lot of those kind. I think it is a very good idea to have a seminar in that direction but also we have to create the mode of how to collect the reported cases of an unethical behaviour which sometimes cause death or pain to mother and children. There should be a way to motivate those who are doing their job following the ethical conduct. I am looking forward for the great idea to be discussed in detail and find the way out. We can select one area to start with then see how better it will work.​

----------------------------------------------------
UDADISI: Rethinking in Action: BURIANI MWANAHARAKATI-MWANAMICHEZO
 
B

Bawa mwamba

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2010
Messages
351
Points
0
B

Bawa mwamba

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2010
351 0
WoS,

Jukumu la uzazi salama huangukia jamii nzima na si mzazi mmoja au wazazi wawili tu. Kuweza kuelewa hili kwa namna ya pekee naomba niwe mwanafalsafa kidogo. Watoto huzaliwa katika jamii na ni kutoka katika jamii hiyo hukua na hatimaye wao nao huzaa watoto na kizazi kinaendelea kuelekea umilele. Kwa kadiri jamii inavyojiandaa kupokea watoto ndivyo hivyo hivyo inapokea watoto na nguvu yake ya uwepo hutegemea uzazi na malezi ya watoto hao.

Endapo kwa mfano, watoto wengi hufa wakiwa wachanga kwa sababu ya miundo mbinu mibaya, magonjwa ya utotoni, au matatizo ya uzazi ambayo yangeweza kuondolewa au kupunguzwa basi jamii inajikuta inapoteza kizazi au watoto wengi katika jamii hiyo. Lakini upande mwingine ni kuwa hata wale wenye kunusurika na matatizo ya utotoni wanaweza kujikuta bado wana matatizo katika maisha yao kwa sababu ya matatizo ya utotoni, mfano mzuri ni polio ilivyokuwa inatuathiri sana kabla ya hatimaye kufanikiwa kuindoa.

Hebu nilioneshe hili kidogo:

Kwa Tanzania mortality rate ya watoto kwa takwimu za hivi karibuni 2008 ni watoto 104 kati ya 1000 hufa kabla hawajatimiza miaka mitano. Katika Marekani kwa mwaka huo huo ni watoto 8 na kwa Australia ni 6. Nchi zote za Ulaya Magharibi ziko kwenye single digits. Unaweza kuangalia mlingano zaidi hapa: Child Mortality

Sasa, utaona kuwa jamii zilizoendelea vile vile ndizo zenye mazingira salama ya uzazi! Naweza kuchukua vipimo vingine mbalimbali kuonesha kuwa jamii ambazo hazijaendelea zinajionesha vile vile kwenye masuala ya uzazi salama. Huwezi kuwa na jamaa iliyoendelea halafu ukawa na uzazi mbovu!

Nchi hizi zilizoendelea zimeelewa kile ambacho sisi hatutaki, tumeshindwa na hatuna mpango wa kukielewa. Huwezi kuwa na taifa la kisasa bila kuwa na mambo ya kisasa katika mazingira ya uzazi! Wenzetu wameelewa kile ambacho natumaini nitapata muda kukimalizia ninakiita "Nadharia Mpya ya Maendeleo kwa Kupokezana Vizazi". Tukielewa nadharia hii tutaona kuwa kizazi kilichopo kisipoandaa kizazi kinachokuja au kizazi kinachoondoka kisipoandaa kizazi kinachojiandaa kutawala basi mbele ni vurugu kwa sababu kila mtu anajifanyia ya kwake tu.

Matokeo yake ni kuwa jukumu la uzazi salama anaachiwa mama kana kwamba katika jamii nzima yuko peke yake. Matokeo yake kina mama wanajikuta zaidi ya kuwa na jukumu kubwa la kuzalisha mali vile vile wanazidi kukandamizwa na jukumu la uzazi na malezi.

Hili linatuleta kwenye swali lako la mwisho. Kina Baba wako wapi? Jamii zetu bado ni jamii za mfumo dume, bado wanaume bado hawajazama sana katika suala zima la uzazi na hasa katika kufuatilia mazingira ya uzazi wa watoto wao.

Mfano mzuri ni hizo hospitali za Mwananyamala na Temeke; kama wanaume wangeona kuwa wake au wanawake wao wanazalia katika mazingira mabaya wangelalamika na hata kuandamana dhidi ya serikali mbovu! Wanaume wangekuwa wanajali uzazi salama wa watoto wao wasingechagua madiwani wale wale na kwa hakika wasingekaa kuona wake zao wanalala chini baada ya kujifungua!

Ndio maana ninaamini inatupasa kabisa kina mama kuingia kuongoza mabadiliko tunayoyataka. Kina baba tumeshindwa.
 • HAPO NDIPO ULIPONIFANYA NIINGIE KWENYE JF FORUM,umegusa mengi na umeyachambua vya kutosha
 • Sasa, utaona kuwa jamii zilizoendelea vile vile ndizo zenye mazingira salama ya uzazi! Naweza kuchukua vipimo vingine mbalimbali kuonesha kuwa jamii ambazo hazijaendelea zinajionesha vile vile kwenye masuala ya uzazi salama. Huwezi kuwa na jamaa iliyoendelea halafu ukawa na uzazi mbovu!
 • SIASA KWENYE AFYA HAIFAI.WATU WACHANGIE MATIBABU.SERIKARI PEKEE HAIWEZI,MATIBABU NI GHALI MNO.MAMBO YA SIFA KWAMBA MAMA MJAMZITO KUJIFUNGUA NI BURE,HIZO NI SIFA ZA KIJINNGA.BIMA YA AFYA IPO KWANINI WALIPIE WACHACHE ?KWA NINI ISIWE SHERIA KWA NCHI NZIMA.KAMA WATU WANA UWEZO WA KUDAI MAENDELEO SABABU YA KODI ZAO, JE HUDUMA BORA ZA AFYA WANGESHINDWA KUZIDAI?
 • NCHI ZA WENZETU, MFANO CHINA UNALIPA KWANZA NDIO MAMBO YANAENDA HATA KAMA MAMA NI MJA MZITO.SASA HIVI WANANCHI WOTE WANIADAI SERIKALI BIMA YA AFYA.SISI BONGO JE ?
 • Nchi hizi zilizoendelea zimeelewa kile ambacho sisi hatutaki, tumeshindwa na hatuna mpango wa kukielewa. Huwezi kuwa na taifa la kisasa bila kuwa na mambo ya kisasa katika mazingira ya uzazi!
 • Kwa bongo siasa itaongelewa vipi?bila kuwa na sifa ya matibabu bure,mbunge katoa msaada wa vitanda bure?na magodoro?,Fulani kamwita Naomi Camp..ll , na kaja mwananyamala ,kamwaga machozi baada ya kuona kinamama wanalala chini.anatoa msaada na akiondoka kesho tunakuta hali ni ile ile .Pres KARUME KAPIGA CHINI MSAADA WA RAZA KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, ni mama yake tu anayetakiwa kutoa hiyo misaada.Kuna sheria au sera kweli ya wananchi kuudai masaada wao? au Tususubiri bakuli jipya la J.Z.. labda utafika palengwa ?Kama bima ya afya ingefanya kazi at least kwa 40 % na ingesimamiwa vyema yote haya yangetukuta?
 • Wanaume hawana uwezo wa kulalamikia ubovu wa hizo huduma kwani wamechangia nini?hivi nani mwenye haki ya kulalamikia kitu cha bure?Jibu lake siku zote ni rahisi.,..serikali yetu kwa sasa haina hela?uchumi wa dunia umeyumba hivyo tumebalance //n.k.KAMA WANGEKUWA WANALIPIA UWEZO WA KUULIZA WANGEKUWANAO.
 • BURE YA MISAADA na MENGINEYO NDANI YAKE NDIO YANAYOTUSUMBUA,.MPAKA TUNAPLAN BAJAJI KUWA AMBULANCE?du,.KAZI SIASA TU.,NA MIPANGO ISIO ELEWEKA INAUZI MNO
 
B

Bawa mwamba

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2010
Messages
351
Points
0
B

Bawa mwamba

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2010
351 0
 • Acheni kuandikia mate ihali wino huu hapo upo: Childbirth in Tanzania - Slide Show - The New York Times
  DU ASANTE SANA KWA HIZO PICHA ,.NA MAELEZO YAKO,.HIZI PICHA HAZIFURAHISHI KABISA NA NI UNETHICAL KUWEKA PICHA KAMA HIZI,.ALIYETOA RUHUSA YA KUPIGA PICHA KAMA HIZI NI NANI.?
 • YAANI UNAONYESHA MPAKA SURA YA MADAKTARI NA PICHA KABISA YA MAMA AKIJIFUNGUA,TENA WANAANDIKA NA JINA LAKE KABISA[digna AYO],.HESHIMA IKO WAPI SASA?HIYO NI NORMAL DELIVARY BWANA INA UHUSIANO GANI NA MATATIZO YETU.KAMA SIO KUSHUSHIANA HESHIMA?LOl AU NI TUMIKO LA KUOMBEA MISAADA
 • LAKINI UUKWELI BADO HALI HAIPENDEZI,.HAO WENGINE HATA SISEMI WAMECHOKA ILE MBAYA..,.BIMA YA AFYA IWE KWA KILA MTU,.KUTOKEA HAPO ZITAPATIKANA HELA ZA KUBORESHA MAZINGIRA.SERIKALI IMESHINDWA KUTOA HII HUDUMA BURE
 • MISAADA KITU KIBAYA MNNO INATUTIA HATA UVIVU KUFIKIRI,.New york times noma mno
 
Forum statistics

Threads 1,334,142
Members 511,876
Posts 32,466,195
Top