Uzao wa mapacha katika jamii ya Wanyakyusa

Uyole CTE

Member
Apr 17, 2015
7
12
Katika jamii zetu nyingi za kiafrika mtu au familia ipatapo mtoto huchukuliwa kuwa jambo la heri au Baraka sana katika familia husika, japo ilikuwepo tofauti kubwa endapo mtu ama familia Fulani watabahatika kuzaa watoto mapacha jambo lilikuwa linageuka na kuwa laana/ balaa ama mkosi mkubwa sana.

Mama mjamzito akiwa anakaribia kujifungua (Zikibaki siku chache ama miezi michache) Mke na mume wake walikuwa wanafanya maamuzi ni wapi hasa mwanamke anaweza kwenda kujifungulia, lakini popote watakapo chagua walikuwa wanaambatana na mama mzazi au mlezi wa Mwanamke na mama mzazi/ mlezi wa mwanaume (Mama Mkwe) katika uzazi (NKUPANJA UBHUFYELE), Endapo walichagua ajifungulie kwa wazazi wa mwanamke ilikuwa ni lazima akaishi kwa wazazi wa mwanaume japo siku chache ikiwa kama heshima kwa mumewe.

Siku ya kujifungua alikuwa anachukuliwa mama mwenye uwezo na uzoefu wa kuzalisha (Mkunga) (UNGANGA UGWA KUPAPISYA). Jamii kubwa haikuwa ikizalia ndani walikuwa wanazalia kwenye Mgomba uliojificha na wenye majani mengi ili kuzuia watu wasiweze kuona kinachoendelea, mama mjamzito akijifungua kondo la nyuma likitoka walikuwa wanachimba shimo na kulikalisha vizuri kwa imani yao mama mzazi azidi kuwa na uzao mzuri, vivyo hivyo kitovu cha mtoto aliyezaliwa kikikatika walikuwa wanautaratibu maalum wa namna ya kukifukia kwa maana ya kwamba kiliko katika kunakuwa chini na kulikofungwa uzi kunakuwa juu walikuwa wakifanya hivyo ili mtoto wao mzazi aendelee vizuri.

Mama mjamzito akijifungua mapacha (BHA MBASA), ambao waliitwa kulwa (MBASA) Doto (SINDIKA) jamii ilikuwa inaamini kwamba ni mkosi hivyo alikuwa anatafutwa mganga wa kienyeji ili kuja kutakasa familia, ukoo na ikiwezekana na majirani wote ili isiweze kujirudia tena. Kama itatokea katika familia kuna wanafamilia hawapo wako nje ya mkoa ama nchi walikuwa wanatunziwa dawa za kienyeji mpaka watakapo rudi, hata kama watakaa miaka kadhaa.

Dawa maalum za kienyeji zenye kutoa mikosi zilikuwa zinachemshwa kwenye kwenye chungu kikubwa (ISYALA), ambacho pia kilitumika kupikia makande wakati wa msiba, mganga wa kienyeji anachukua ufito wa majani ya mgomba mabichi na kuutwanga kama mswaki (IFUNGUBHO IMBISI) analoweka kwenye maji ya moto na kuanza kuwapiga wanafamilia, ukoo au majirani wanaume kwa wanawake na watoto kuanzia magotini mpaka kwenye unyayo huku akisema maneno ya kutoa mikosi.

Kwa kizazi cha leo familia ipatapo watoto mapacha imekuwa Baraka kubwa sana kwa familia husika.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na
Uyole cultural tourism enterprise
uyolecte@gmail.com
0783545464
 
Momumo aisee yaani nyumbani kwetu huko nina dada yangu mpaka sasa anaitwa Mbassa kweli haya mambo yapo aisee
 
Asante kwa mafundisho mazuri sana hasa kwetu BHAJANGA. Ila nahisi kuna tatizo hapo kwa Mapacha (MBASA NA SINDIKA). SINDE ni yupi kati ya hao... Au ni jina lililotengenezwa baadaye?
 
Hahaha tunakumbuka mbali sana.....kuna hili jambo pia heshima ya mke kwa baba wa mume huwa inanifanya nikumbuke mila na desturi za kinyakyusa zilivyokuwa na nguvu....yaani mke wangu haruhusiwi kumtazama sura au kumwonyesha sura yake baba yangu na ni mwiko kumtaja jina lake hadi "ambonole".
 
Doto ni Sinde sio Sindika, sijui lakini kwasababu kuna Kinyakyusa cha bara na cha visiwani, mengine yote yako sahihi
 
Ndaga fijho!
 
Asante kwa mafundisho mazuri sana hasa kwetu BHAJANGA. Ila nahisi kuna tatizo hapo kwa Mapacha (MBASA NA SINDIKA). SINDE ni yupi kati ya hao... Au ni jina lililotengenezwa baadaye?
Kinyakyusa ni kipana sana, inawezekana kwa Kinyakyusa cha kwao yuko Sindika ndiye huyo huyo Sinde
 
Hahaha tunakumbuka mbali sana.....kuna hili jambo pia heshima ya mke kwa baba wa mume huwa inanifanya nikumbuke mila na desturi za kinyakyusa zilivyokuwa na nguvu....yaani mke wangu haruhusiwi kumtazama sura au kumwonyesha sura yake baba yangu na ni mwiko kumtaja jina lake hadi "ambonole".
Ni kwasababu ya ushenzi wa baba wakwe wa Kinyakyusa wa miaka hiyo, ndipo ikatolewa amri na Machifu, mkwe mwana harusiwi kuonana na baba mkwe.
 
Hahaha tunakumbuka mbali sana.....kuna hili jambo pia heshima ya mke kwa baba wa mume huwa inanifanya nikumbuke mila na desturi za kinyakyusa zilivyokuwa na nguvu....yaani mke wangu haruhusiwi kumtazama sura au kumwonyesha sura yake baba yangu na ni mwiko kumtaja jina lake hadi "ambonole".
Hata 'akikubonola ' hutakiwi kumuangalia angalia hovyo, kiti alichokalia usikae. Halafu wanyakyusa wa Tukuyu ndiyo wanafuatisha sana hayo mambo kwa Kyela sijaona wakifuatilia sana.
 
Mkiambiwa ustaarabu ulianzia pwani mnakataa maana huwezi kuta huu upuuzi kuanzia Tanga beach hadi Mtwara beach areas.
Proudly to be Twin from the Indian Ocean in Tanzania
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom