Uyole CTE
Member
- Apr 17, 2015
- 7
- 12
Katika jamii zetu nyingi za kiafrika mtu au familia ipatapo mtoto huchukuliwa kuwa jambo la heri au Baraka sana katika familia husika, japo ilikuwepo tofauti kubwa endapo mtu ama familia Fulani watabahatika kuzaa watoto mapacha jambo lilikuwa linageuka na kuwa laana/ balaa ama mkosi mkubwa sana.
Mama mjamzito akiwa anakaribia kujifungua (Zikibaki siku chache ama miezi michache) Mke na mume wake walikuwa wanafanya maamuzi ni wapi hasa mwanamke anaweza kwenda kujifungulia, lakini popote watakapo chagua walikuwa wanaambatana na mama mzazi au mlezi wa Mwanamke na mama mzazi/ mlezi wa mwanaume (Mama Mkwe) katika uzazi (NKUPANJA UBHUFYELE), Endapo walichagua ajifungulie kwa wazazi wa mwanamke ilikuwa ni lazima akaishi kwa wazazi wa mwanaume japo siku chache ikiwa kama heshima kwa mumewe.
Siku ya kujifungua alikuwa anachukuliwa mama mwenye uwezo na uzoefu wa kuzalisha (Mkunga) (UNGANGA UGWA KUPAPISYA). Jamii kubwa haikuwa ikizalia ndani walikuwa wanazalia kwenye Mgomba uliojificha na wenye majani mengi ili kuzuia watu wasiweze kuona kinachoendelea, mama mjamzito akijifungua kondo la nyuma likitoka walikuwa wanachimba shimo na kulikalisha vizuri kwa imani yao mama mzazi azidi kuwa na uzao mzuri, vivyo hivyo kitovu cha mtoto aliyezaliwa kikikatika walikuwa wanautaratibu maalum wa namna ya kukifukia kwa maana ya kwamba kiliko katika kunakuwa chini na kulikofungwa uzi kunakuwa juu walikuwa wakifanya hivyo ili mtoto wao mzazi aendelee vizuri.
Mama mjamzito akijifungua mapacha (BHA MBASA), ambao waliitwa kulwa (MBASA) Doto (SINDIKA) jamii ilikuwa inaamini kwamba ni mkosi hivyo alikuwa anatafutwa mganga wa kienyeji ili kuja kutakasa familia, ukoo na ikiwezekana na majirani wote ili isiweze kujirudia tena. Kama itatokea katika familia kuna wanafamilia hawapo wako nje ya mkoa ama nchi walikuwa wanatunziwa dawa za kienyeji mpaka watakapo rudi, hata kama watakaa miaka kadhaa.
Dawa maalum za kienyeji zenye kutoa mikosi zilikuwa zinachemshwa kwenye kwenye chungu kikubwa (ISYALA), ambacho pia kilitumika kupikia makande wakati wa msiba, mganga wa kienyeji anachukua ufito wa majani ya mgomba mabichi na kuutwanga kama mswaki (IFUNGUBHO IMBISI) analoweka kwenye maji ya moto na kuanza kuwapiga wanafamilia, ukoo au majirani wanaume kwa wanawake na watoto kuanzia magotini mpaka kwenye unyayo huku akisema maneno ya kutoa mikosi.
Kwa kizazi cha leo familia ipatapo watoto mapacha imekuwa Baraka kubwa sana kwa familia husika.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na
Uyole cultural tourism enterprise
uyolecte@gmail.com
0783545464