Uzamiaji Afrika Kusini: Mikasa katika harakati za kuzamia Afrika Kusini kwa njia za panya

Hivi ukiacha ile story yako, kuna nyingine ya SA ambayo imeshafika mwisho?

Na ulijibu maswali mengi wadau waliyouliza.

Insecurities ni tatizo, sasa mtu kawekewa uthibitisho kwamba ni fake, lakini badala amfate huyo anakomaa na wewe.
Acha kumpamba huyo jamaa, au hii ni I'd yako nyingine.
Unachekesha eti "Hivi ukiacha ile story yako"
Soo unataka kumaanaisha story za SA ni yake tu ndio iliyofika mwisho.??
Alijibu maswali yapi huu jamaa story, yake ilijamaa makando kando alipakua hadi picha fake mtandaoni ya kumbu, watuu wakamuumbua akaifuta kisha akatomomea, Baada ya watu kumbembeleza ikabidi arudi kwa fedhea. Ila kila mtu alikwisha jua kua ile story yake ni yakutunga
 
Acha kumpamba huyo jamaa, au hii ni I'd yako nyingine.
Unachekesha eti "Hivi ukiacha ile story yako"
Soo unataka kumaanaisha story za SA ni yake tu ndio iliyofika mwisho.??
Alijibu maswali yapi huu jamaa story, yake ilijamaa makando kando alipakua hadi picha fake mtandaoni ya kumbu, watuu wakamuumbua akaifuta kisha akatomomea, Baada ya watu kumbembeleza ikabidi arudi kwa fedhea. Ila kila mtu alikwisha jua kua ile story yake ni yakutunga

Unaweza kunipa jibu la story ya SA iliyoisha?
 
Kwel mkuu huyu jamaa kawa hovyo sana yani akiona tu neno south Africa basi anasimamisha masikio na kutoa macho nilisoma comment kama 60 sijaona comment yake Mara paa huyu hapa sijui anajikuta ndio nan ndan ya south mtu mwenyew umeenda kwa ndege na kurud kwa ndege lakn unajidai unaijua kila boda
Jamaa ndio amekuwa regulatory director wa mambo ya south Africa.
 
Unaweza kunipa jibu la story ya SA iliyoisha?
Jamaa unasikitisha sana kwa hili swali lako nimeshaelewa wewe niwale wafata mkumbo, kweli huyo jamaaa kafanikiwa kuwachota akili na story yake ya uongo.
Ngoja nikuwekee moja nyingine ukafanye research sawa
 
Jamaa unasikitisha sana kwa hili swali lako nimeshaelewa wewe niwale wafata mkumbo, kweli huyo jamaaa kafanikiwa kuwachota akili na story yake ya uongo.
Ngoja nikuwekee moja nyingine ukafanye research sawa

Shukrani Mkuu.
 
1. Kwenye Gari hamkupigwa pingu wakati mnasafirishwa?

2. Begi ulitoa wapi? Ulinunua jingine Lusaka? Kwani wakati mnaenda kumwaga mtondoo mlienda na mabegi yenu?
Tulia Kijana,,,, beg alinunua lingine kwa machinga
 
Ndio maana sikuhizi tunasubiri kwanza wiki moja ipite ndio tunaanza kusoma story endapo tukijiridhisha haina makando kando,

Storytellers wengi sikuhizi hususan hawa wa story za Sauzi ni wamekuwa bogus ni kama ngoma ya watoto haikeshi. Shame!
 
Hii stori ipo kwenye kitabu tayari hivyo ni suala la ku copy na ku paste yani ingekua naruhusiwa na mda nilio nao leo ningei paste yote watu wakukuruke nayo......
Mkuu uliweza vp kufungua ile attachment...mm inanipeleka home page
 
Kuna thread yake humu ya kutaka kwenda South kufata mwanamke, anasema ana miaka 29.

Nikilinganisha na miaka ya huu uzi nikasema ngoja nisubiri nione mwisho wake.
Mmeanza kutuharibia uhondo
 
SAFARI YA KUZAMIA AFRIKA YA KUSINI KWA NJIA ZA PANYA.

Sehemu ya saba.

Haikuchukua muda mrefu kile kikosi maalumu kikawa kimefika na mara
moja nikachukuliwa na kufungwa pingu kisha nikapandishwa hadi kwenye gari ya polisi baada ya hapo polisi kama wawili hivi wakaingia ndani kuandikishana makabidhiano. Nikabaki na askari watatu ambao wawili walikuwa
wamesimama kwenye mlango wa gari mbele yangu na mmoja nyuma yao, nilipopiga mahesabu yangu ya mbinu za kimapambano nilizozipata Kongo na
uzoefu wangu kwenye hayo masuala yaani kuangaika ya polisi na kiwango changu cha kimapambano ambacho kilikuwa kimefika kabisa
nilichofundishwa na vikundi vya waasi na kuiva vizuri, nikaona kabisa naweza nikatoroka kwa mazingira nilivyokuwa nayaona. Nikainuka kutoka pale nilipokuwa kwa kasi sana nikawakumba wale askali waliokuwa kwenye mlango wa gari wote nje kama vile wamegogwa na kichwa cha treni iliyo kwenye mwendo kasi, walienda chini
moja kwa moja na hakuna alieinuka wakatulia kimya. Yule dereva asijue nn cha kufanya haraka nikachukua funguo ya pingu ambapo muda huo ilikuwa imeanguka chini kisha nikachukua mashine moja ya SMG na magazine mbili
za ziada kutoka kwa wale askali waliokuwa chini.

Nikaanza kukimbia wakati naanza kuondoka wale askali waliokuwa chini nao wakapata fahamu, bahati mbaya kwangu muda huo huo zikaja gari mbili za askari polisi wakiwa wamejaa kutoka upane wa Afrika kusini.Haikuchukua muda ikaja na gari nyingine kutoka upande wa Zimbabwe, kwa
kweli kulingana na uwingi wa askari hao ilikuwa sio rahisi kukabiliana nao, pia
wananchi wa pande zote mbili za border walikuwa wanamiminika kuja upande wangu, kwa kweli nikawa sina namna nikakimbia hadi kwenye daraja la mpaka
juu ya mto Limpopo huku nafyatua risasi kuelekea kwa askari kama kichaa ili wasinisogelee na kuzuia uwezekano wa kunishambuli, nilipofika juu ya daraja
nikatupa ile silaha kwa kuwa najua madhara ya kuondoka na silaha ya askari ambayo huongeza uhalali wa kukusaka zaidi, kitu ambacho mpaka sasa sijafahamu, kwa nini hawakunipiga risasi wakati nakimbia pale darajani, hili swali mpaka leo sina majibu yake.

Nikiwa pale juu ya daraja, nikawaachia silaha yao juu, mimi nikajirusha
kwenye mto. Hivyo wakati askari wanafika pale tayari nilikuwa nimesha fika mbali kiasi hata ukipiga risasi utakuwa tu unaziharibu kwa sababu sio rahisi
ukamlenga mtu.
Nikawachoropoka huku nikiwa najua hatari iliyokuwa mbele yangu kwenye huo mto wenye mamba wengi na maporomoko makari na zaidi ni kwamba ulikuwa umejaa sana maji kutokana na msimu wa mvua, lakini jemedali nikapiga moyo
konde nakuendelea kuambaa juu ya Mto Limpopo moja ya mito mikubwa kabisa barani Afrika. Hata wale wananchi na Polisi waliobaki pale kwenye daraja lao hawakuamini kilichokuwa kimetokea.

Baada ya kuwatoka askari na wananchi wenye hasira kali, niliendelea kutiririka na maji ya mto Limpopo kwa kufuata uelekeo wake, lakini kadiri nilivyokuwa naenda mbele ndivyo maji yalivyozidi kuongeza kasi, kasi ilizidi kiasi kwamba nikawa siwezi kuyamudu tena. Jitihada ambayo nilikuwa
nimebakiwa nayo ni kujiokoa, jambo ambalo lilikuwa limeanza kushindikana
pia. NiIikuwa nikidaka mizizi ya miti inang’oka, matawi ya miti pia yalikatika kwa
kweli nikaanza kuona kifo kina nikaribia kabisa, kwa mbali mbele yangu nilianza kuona maporomoko makubwa sana. Nikajua ndio maana maji yameongeza
kasi ndipo nilipofika karibu sana na maporomoko kwa njia ya ajabu sana ambayo siwezi kuielezea nikajikuta nikadaka tawi la mti. Nikaling’ang’ania kwa nguvu zote na kwa kweli safari yangu ya kupelekwa na maji sehemu isiyo
julikana ikaishia hapo.
Nikafanya utaratibu wa kujinasua hapo kwenye mto, nikafanikiwa kutoka kwenye mto hadi nchi kavu pembeni yake, nikaanza kupumzika huku natafakari uelekeo wangu uwe wapi, sikuwa na nguvu kutokana na ile dhoruba ya maji lakini nilikuwa na uhakika kwamba nipo upande wa Afrika ya Kusini.

Nikapumzika kwa masaa matatu hivi ndipo nikaanza kutembea huku sijui ninakoelekea tena kwenye msitu mzito sana ambao si rahisi binadamu wa kawaida
kufika kwenye msitu huo kwa njia za kawaida.
Baada ya kutembea kwa masaa kadhaa nilianza kuona Moshi kwa mbali mbele yangu, nikazidi kusogea ndipo baada ya kusogea kwa mwendo wa kutosha nikafika sehemu iliyokuwa inafuka moshi. Baada ya kufika sehemu ile ambayo ilionekana ni kama kambi tu ya watu wanaofanya shughuli fulani, nilikuta watu
wawili ambao walikuwa wanaongea lugha ya kishona kwa bahati nzuri mmoja wao alikuwa anajua Kiingereza kidogo basi tukaongea na kisha wakanipokea japo kwa wasi wasi. Wale jamaa walikuwa wema walinipa chakula nikala vizuri nikashiba kabisa, na kwa kiasi nikaanza kurejea kwenye nguvu zangu za kawaida ambazo zilikuwa zimekaribia kuisha kabisa.
Baada ya kula tukafanya mazunguzo ya kina na wale jamaa, walinieleza
kwamba wao ni wenyenyeji wa kijiji cha Malale.kutokana na harakati za kutafuta maisha na ugumu wa maisha nchini kwao wameshindwa kukaa kijijini wameamua kukaa hapo porini. Wakati huo nilikuwa tayari nipo ndani ya Afrika ya kusini, kwenye nchi yangu ya ahadi, walinipa stori nyingi sana za kwenye
machimbo ya dhahabu na shaba huko Afrika ya kusini, wakati wote huo mimi nilikuwa sijawaambia stori yangu ya harakati zangu, walipo niuliza nikawajibu
kwa kifupi sana na sehemu kubwa ilikuwa ni uongo, lengo langu ilikuwa kuwafanya wasiniogope wanione ni mtu wa kawaida.

Nikakaa na wale jamaa kwa muda wa siku moja, kisha siku ya pili yake
wakanisindikiza hadi karibu na kijiji chao ambapo waliishia njiani kutokana na wao kutokutaka kabisa kukutana na watu wa kijiji chao. Sijui sababu hadi leo ya wale vijana wa makamo kukataa kabisa kuonana na watu wa kijiji chao. Baada ya kufika katika kijiji ambacho kilionekana kuwa kimeendelea vizuri tu na kinakaribia kuwa mji, niliongeza umakini sana kwenye fedha zangu ili zisipotee kwa sababu nilijua ndio uhai wangu. Bado nilikuwa na kama kiasi cha
shilingi milioni 12 kwa fedha za kitanzania ambazo nilikuwa nimezibadilisha
kuwa dollar za Kimarekani. Kwa hiyo nikatafuta nyumba ya kulala wageni kwa
ajili ya mapumziko wakati natafakari nifanye nini!!. Haikunipa shida kupata hiyo sehemu kutokana na uzoefu wangu katika nchi za kusini mwa Afrika.

Baada ya kupata sehemu ya kujihifadhi, nilikaa pale kama siku tatu hivi, ilipofika siku ya nne nikaanza kujisikia vibaya kama homa hivi, sikutaka kwenda hospitali kutokana na rekodi zangu za uhalifu, kwa hiyo nikawa nimenunua tu dawa kutoka kwenye duka la dawa na kuanza kutumia. Zile dawa hazikunisaidia hali yangu ilizidikudhoofika na kuwa mbaya. Ndipo siku ya siku nikazidiwa nikawa siwezi kuongea wala kusimama nikachukuliwa na watu wa Gesti ambao nilikuwa naishi huku wakiwa wanaogopa
sana hadi hospitali ya hapo kijijini. Hali yangu haikuruhusu kutibiwa hapo kijijini nikasafirishwa hadi kwenye hospitali kubwa zaidi katika mji wa Polokwane kwa gari ya kubebea wagonjwa, hali yangu ilikuwa mbaya kiasi kwamba watu
walikuwa wanasema huyo jamaa hafiki. Lakini Mungu akanifikisha hapo hospitali na mara tu baada ya kufika nikapelekwa ICU na kuanza kupata matibabu ya dharula.

Uchunguzi wa madaktari ulionesha kwamba sehemu ya kichwa ilikua imepata ufa. Walisema umetokana na kugonga au kugogwa na kitu kizito. Baadae
nilikuja kubaini kwamba itakuwa nilijigonga kwenye ile purukushani ya spidi ya maji kwenye mto Limpopo, huenda nilijigonga kwenye mawe bila kujua kutokana na mwili wote kuwa ulikuwa umekufa ganzi kutokana na baridi kali niliyoipata kwenye yale maji na hali ya eneo lile kuwa ya baridi sana. Nikakaa ICU kwa siku mbili ikaonekana ile hospitali haina vifaa vya kufanya
upasuaji wa kichwa ambao ilikuwa natakiwa kufanyiwa, kwa hiyo nikahamishiwa hospitali kubwa zaidi inchini Afrika ya kusini katika Jiji la Johannesburg.
Nilisafirishwa nikiwa mahututi sana.
Kwa hiyo ni kweli nilikuwa nimefika kwenye mji wa ndoto yangu, lakini nikiwa
naumwa sana tena sijitambui kabisa, na nikiwa sina uhakika kama nitapona
tena. Muda wote huo nilikuwa natibiwa na zile fedha zangu. Nashukuru wale jamaa walikuwa waaminifu kiasi kwamba hawakuniibia kiasi chochote cha
fedha zangu na hata niliposafirishwa zilikabidhiwa kwa watu salama.

Baada ya matibabu ya siku 4 jijini Johannesburg, nikatolewa ICU na kulazwa kwenye wodi ya wagojwa wa kawaida. Baada ya kuingizwa kwenye hiyo wodi
nilikutana na maajabu ya dunia ambayo huwezi kuyategemea. Jamaa aliyekuwa pembeni yangu alikuwa ni moja ya wale askari ambao nilipambana nao
kule boda, nilimkumba lakini kwa bahati hakufa, akawahishwa hospitali.
Mambo yakawa mabaya huku hali yangu ikiwa bado mbaya siwezi hata kuinuka, nae pia alikuwa na hali mbaya sana. Yeye alikuwa bado hajanifahamu
hadi muda huo. Ikabidi nigeukie upande wa pili ili asije akaniona.

Nikawaza kwamba ugonjwa umenileta kwenye mikono ya serikali kwa urahisi sana, yaani jitihada zangu zote zile za kujiokoa hadi kupata matatizo ya kupasuka kichwa itakuwa kazi bure, Nilihisi nataka kufa lakini sikufa. (Kuna wakati binadamu anapitia
wakati mgumu kiasi kwamba anatamani hata afe lakini kifo kinakuwa kimejitenga nae mbali sana.) Tukalala hadi asubuhi. Muda wa kuona wagojwa ulipofika watu wengi tu kutoka kule boda walikuja kumjulia hali yule askari, na bahati mbaya wengi wao walikuwa ni askari wenzake ambao kati yao ni pamoja na wale niliopambana nao. Hapo mimi nilikuwa nimejifunika uso wote kabisa huku
namuomba Mungu wasije wakasema wanione wanipe pole. Siku hiyo ikapita
wakaahidi watarudi tena baada ya siku nne kumjulia hali. Nikamshukuru Mungu kwa kuniongeza siku nne mbele. Niliamini hadi siku nne ziishe nitakuwa nimepata nafuu naweza kufanya maarifa yoyote. Hata hivyo ilikuwa ni kujipa moyo tu kwani nilijua siku nne hata nyuzi zitakuwa hazijatolewa hata dripu za damu na maji zitakuwa bado.

Baada ya wale wageni kuondoka hali ya yule afande ilibadilika na kuwa mbaya sana hivyo ikabidi arejeshwe ICU. Kwa upande wangu nilimshukuru sana
Mungu kwa kuniweka nae mbali japo ni eneo moja la hospitali. Niliendelea kupata matibabu katika hiyo hospitali na bahati nzuri hali yangu iliendelea
kuimarika kadiri siku zilivyosonga mbele. Baada ya siku 20 nilikuwa nimepata
nafuu sana, hivyo nikahamishwa wodi na kupelekwa katika wodi ya wagojwa ambao wanakaribia kuruhusiwa kutoka. Wakati huo nilikuwa naweza kutembea mwenyewe na nilikuwa naweza hata kufanya mazoezi mepesi. Nilipelekwa kwenye kile chumba majira ya usiku, nilipofika tu na kukabidhiwa
kitanda nilikutana tena kwa mara nyingine na yule askari ambaye nilikutana nae kwenye kile chumba cha wagojwa wanaotolewa ICU. Safari hii alikuwa ameimarika sana afya yake, alikuwa anakaribia kuruhusiwa kutoka. Kwa bahati mbaya nilipangwa kitanda kilichokuwa karibu naye sana.
Kwa hiyo mara baada ya kufika tu kitandani kwangu na kuwekewa vifaa vyote muhimu. Yule askari alinitambua na kuniambia ‘it’s you’, ikimaanisha kuwa ni wewe. Nikajifanya naumwa sana ili kumpumbaza ajue naumwa sana.

Yule askari alisikika akisema kwamba aliambiwa kwamba nilijitosa kwenye
mto Limpopo na kwamba alijua siwezi kutoka salama na ndicho kimenikuta. Akasema anamshukuru sana Mungu kwa kumletea adui yake jirani, akasema lazima haki itapatikana, nitapata malipo sawasawa na nilivyotenda. Wakati wote huo mimi nilikuwa nimelala tuli, namsikiliza na bahati nzuri ile
wodi siku hiyo wagonjwa tulikuwa wawili tu mimi na yeye. Huyu jamaa alikuwa anajua mimi ni mgonjwa sana siwezi kufanya lolote. Alitamba na kumshukuru sana Mungu kwa kumletea adui yake karibu, yaani ni kama vile kifaranga alijirusha kwenye tanuru la moto mwenyewe. Mimi kwa upande wangu nilikuwa nimetulia kimya najifanya hali yangu ni
mbaya sana, lakini kiukweli hali yangu ilikuwa imeimarika sana.

Nilikuwa naweza hata kutoka. Hesabu zangu zilianza, kuonesha kwamba kama nitaruhusu uwepo wangu hapo hadi asubuhi maana yake ni kwamba nimekubali kukamatwa na polisi. Kwa hiyo kwa namna yoyote japo nilikuwa sijamaliza matibabu ilikuwa inani-
lazimu kuondoka usiku huo huo, lakini nilikuwa na vikwazo viwili ambavyo vingefanya kuondoka kwangu kuwe kugumu sana; cha kwanza ilikuwa ni
ulinzi wa ile hospitali, na cha pili ni kwamba fedha zangu ambazo zingebaki baada ya kutoa gharama za matibabu zilikuwa bado zipo kwenye uongozi wa hiyo hospitali. Kati ya haya mawili la kwanza sikuwa na tatizo nalo sana
kutokana na uzoefu wangu wa masuala ya kutoroka ambapo walinzi kwangu ilikuwa ni suala dogo sana. Kwangu gumu ilikuwa ni kuacha fedha zangu.

Fedha ambazo nilizipata kwa damu na jasho.
Wakati naendelea kuwaza namna hiyo, nikamuona yule askari anapiga simu
kwa wenzake anawaeleza juu yangu. Nikawasikia wanasema watafika hospitalini hapo majira ya saa 9 usiku yeye aendelee kunichunga na kuchukua tahadhari. Kitendo cha kusikia hii habari kwangu ilikuwa ni kosa kubwa sana kwa sababu
sasa sikuwaza pesa zangu tena, niliwaza tu namna ya kutoka kabla ya huo muda. Nikasema kwamba fedha zinatafutwa na kwa kuwa zilikabidhiwa kwa
utawala wa hospitali nitazifuata siku yoyote. Kwa hiyo sasa hatua ya kwanza kwangu ikawa ni kusuka mkakati kichwani kwangu namna ya kutoka pale ndani wodini, halafu nikitoka nje nitajua namna ya kufanya ili kutoka eneo hilo. Nikapata wazo kwamba nisubiri yule askari alale kwa sababu haitawezekana awe macho hadi saa tisa usiku ndipo nitoke mle wodini. Lakini wazo hili lilikuwa na mashaka kiasi fulani kutokana na wasiwasi wangu kwamba askari wanaweza wakaamua kuwahi kuja. Kwa hiyo nikapata wazo kwamba kwa kuwa nilikuwa nina nguvu kidogo iliyotokana na nafuu ambayo nilikuwa nimeipata,
kutokana na tukio hilo. Basi wakati nasubiri afande kama atalala nikajiapiza kwamba, kama itatokea akazembea basi nitumie mbinu za kiumafia kumdhibiti kisha nitokomee.

Wazo hili ndio lililoshinda kichwani mwangu, kwa uzoefu wangu wa mambo ya vyombo vya usalama na kwa namna Afrika ya Kusini walivyowekeza teknolojia kwenye jeshi lao la polisi nilijua haitawezekana waje huo muda walioutaja saa 9 usiku. Nikahisi watafika muda wowote pale hospitali. Kwa hiyo nikaanza
kumlia mingo yule afande kwamba kama itatokea azembee hata kidogo nifanye kweli. Haikuchukua muda yule afande akarudi kitandani kwake akajilaza,
alikuwa anajua kuwa mimi ni mgonjwa sana. Kwa hivyo hakuwa na wasiwasi wowote, baada ya dakika chache akajifunika shuka, na mimi sikuchelewa niliruka haraka na kumkaba sehemu ya kifua ambayo alipigwa aliumia na alikuwa
hajapona vizuri, hakuwa mbishi akatulia nikambana puani na mto sekunde chache tu akawa amepoteza fahamu. Baada ya hilo tukio nikatoka nje ya wodi, nilikuwa na changamoto ya kuonekana mapema kutokana na kuvaa zile nguo za hospitali. Nikajihami huku naambaambaa na ukuta hadi mwisho, wakati nazidi kusogea nikamuona mlinzi
mbele kwenye mlango wa kutokea nje ya hospitali, nikatumia akili kali sana, mana nilichukua chombo cha kuwekea taka nikakirusha nyuma yangu kwa nguvu kisha nikazima taa ya korido na kujibana ukutani, yule mlinzi akaja anakimbia kuelekea sehemu ‘dust bin’ lilikorushwa, akawa amenipita nami
bila kuchelewa nikanyata hadi kwenye mlango wa kutokea, nikatoka nje nikaacha yule mlinzi haelewi kilichotokea.
Muda huo ilikuwa kama saa 7 usiku hivi, oooh!! hakika bahati ilikuwaje kwangu, wakati nafika nje tu magari ya Askari
wenye silaha, yakawa yanaingia kwa kasi kubwa sana. Kwa kuwa niliona wakati
gari zinaingia nilikimbia hadi kwenye maua yaliyokuwa yamepandwa pembeni ya fensi ya hospitali, nikatulia pale huku nimelala chini. Wale askari walishuka haraka kwenye gari na wote kukimbilia ndani ya hospitali, hilo kwangu
lilikuwa ni kosa kubwa. Haraka sana nilikimbilia geti la kutokea nje na kuanza kukimbia, sikuwa najua naelekea wapi katika hilo jiji kubwa la Johannesburg.
Hivyo ndivyo nilivyowatoka polisi, na ndivyo nilivyoacha pesa zangu pale hospitali, nilikuwa nimepata hasara kubwa ya kuacha zaidi ya milioni 6 (makadirio), lakini nilikuwa nimepona mikononi mwa polisi huku nikiwa na kesi ya
kuua askari kule mpakani na nikiwa na kesi ya kummalizia askari wodini. Faida
moja niliyoipata ni kwamba nilikuwa nimefanikiwa kufika kwenye mji wa ndoto yangu Johannesburg kwa mtindo huo wa maajabu mengi.

_*Itaendelea.*
 
Hii story ni ya kufikilika na haina uhalisia wowote kwa great thinker kuendelea kuisoma ni kupoteza muda hii labda uwasimulia la darasa la pili C
Chapter ya kwanza na ya pili ilikuwa na kauhalisia flani ila alianza kuweweseka baada ya wale maaskari kupata ajari wote wakafa ila wanne wakatoka wakiwa wasizima na je nani aliwafungua pingu??
2. Kingine cha kutia mashaka na story yako begi la nguo ulilipata wapi wakati ulikimbia polisi wakati wa kwenda kumwaga ndoo ya uchafu
3. Mlipovamiwa kwa yule mama ukavaa nguo za kike na ukasema wewe uliwakaribisha kwa lugja gani?
4. Tunarudi Tanzania umekamatwa na dawa za kulevya unaachiwa uende hotelini kula alafu na hao maaskari wanaziacha kwenye gari bila kulifunga unazifuata sijawahi kuona askari wapumbavu kama hao tangia dunia iundwe na hakuna askari mwenye mapenzi na mtuhumiwa kiasi hicho
 
Hii story ni chai iliyojaa tangawizi ya kutosha.Huyu muandishi hana weledi, tungo yake imejaa maswali Kama yote.Me nimeishia pale walipopata ajali askari wote wakafa wahalifu wakapona.
Hii imeshawahi kutokea.

Sababu kuu ni kuwa, wakati Wa kusafirisha wahalifu hulazimishwa kuketi ama kulala kwenye floor ya Gari. Na Askari kusimama Kwa lengo LA kumlinda Mhalifu, sasa ikitokea ajali Mara nyingi huwa rahisi zaidi kwa Askari aliyesimama kurushwa nje na kupata madhara makubwa kuliko wahalifu waliokalishwa ama kulazwa kwenye floor ya gari..
 
Back
Top Bottom