Uzalishaji ndio utakuza uchumi wetu: Leaders must be told, CCM must understand

Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,907
4,771
Habari za Jioni Wakuu!

Naomba niende moja kwa moja kwemye mada bila kuchelewa. Kuwa na miundo mbinu ya kisasa kama tunavyofanya kwa sasa ni muhimu kwa nchi.
Lakini viongozi wetu wanajisahau, hawaambiwi, hawashauriwi au basi wanakataa na kushupaza shingo zao.
Naomba mimi niseme ukweli hapa kwenye hili jukwaa kwamba CCM na Viongozi wasahau uchumi bora na maendeeleo wanaliotuahidi kama wataendelea na misimamo yao ya sasa ya kujenga miundo mbinu tu na kusahau kanuni za uchumi.

Uchumi unaojengwa kwa sasa nchi hii kwa kuelekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa miundo mbinu ni uchumi wa huduma(service economy).

Na uchumi wa huduma hautasaidia lolote kwa nchi ya wananchi wengi maskini kama ilivyo Tanzania. Kwa hapa niseme tu, “Magufuli is misled or misadvised in his ‘rais wa wanyonge slogan”. Hautasaidia pia uchumi kukua hata kidogo. Rais asidanganywe hapa. Mbaya zaidi madhara yake hayataonekana leo. Mradi pekee unaochukua fedha nyingi utakaosaidia uchumi wan chi hii ukimalizika kwa ufanisi ni mradi wa umeme wa bwawa la Julius Nyerere katika mto Rufiji.

I oppose the approach of this government towards economic growth and prosperity.
Uchumi utakuaje bila uzalishaji? Kwanini uzalishaji umepigwa chini? Kilimo kwanza kiko wapi? Kwanini serikali haipeleki pesa even indirectly kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo na chakula? Kwanini Malawi inatuzidi katika kuuza bidhaa za chakula kama Soya, Karanga na sukari katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi? Kwanini Zambia inatuzidi katika kuuza mahindi kwa nchi za Africa ya mashariki?
Kwanini sehemu ya fedha haipelekwi kwenye uzalishaji wa mazao ya biashara? Kilimo hakihitaji subsidies from tax payer money?

Kwanini hatuna sera ya uzalishaji katika nchi hii? Tumewaachia kweli wanasiasa kutuburuza kama Taifa bila kujua wao wanawaza uchaguzi ujao?

Kwanini serikali iwadanganye wananchi kwamba ipo kwa ajili ya wanyonge?
Uchumi utakuaje bila ajira? Hivi wachumi wetu wanasoma au wamesoma vitabu gani vya uchumi? What kind of government we have which does not address and solve the problem of unemployment? How do it create consumers if a large number of youths are unemployed?

Kwanini serikali haumii inaposikia ajira katika sekta binafsi zimepungua?
Walaji wa huduma na bidhaa watapatikana wapi? Kwanini serikali haiajiri ili kutengeneza kundi la watu wenye uwezo wa kutumia huduma na bidhaa na hivyo kutngeneza mzunguko wa fedha na kutengeneza informal employment nyingi?

Kwanini Raia wa Tanzania waumie kwa hasira ya uzembe wa serikali zilizopita?

Uchumi utakuaje kwa negative incentives tu? Ili uchumi ukue, tunahitaji both negative incetives and positive ones especially the positive ones. Walaji walioko kwenye huduma na uzalishaji tayari wanahitaji motisha chanya ili waweze kuzalisha kwa utayari. Utayari ni muhimu sana katika uzalishaji ili uchumi uweze kukua.

Kwanini serikali haitoi wala haifikirii motisha kwa watumishi wake, wafanyabiashara wa TZ, wafanyakazi wa TZ ili waweze kuendesha uchumi wa nchi kwa utayari?

Naomba serikali ipeleke pesa katika maeneo ambayo italeta tija na ufanisi kwa watu wa Tanzania. Bila hivyo, ijue tu kwamba hii reli na miundombinu nyingine itakuwa imejengwa kwa ajili ya mabeberu. Watakuja kupitisha malighafi kutoka DRC kwenda nje ya nchi. Itakuwa kama kipindi cha ukoloni wa Mjerumani.
 
Back
Top Bottom