Uzalishaji Korosho: Tuna mengi ya kujifunza Vietnam

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
Raw-cashew-nuts-with-shell-WW-210.jpeg


VIETNAM ni moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa ya maendeleo barani Asia. Mwaka 1986 Serikali ya Vietnam ilianzisha mageuzi makubwa ya uchumi yaliyowezesha kuitoa nchi hiyo kwenye kundi la nchi masikini yenye wastani wa kipato cha Dola za Marekani 100 kwa kila mtu hadi ku kia kuwa nchi yenye uchumi wa kati yenye kipato cha Dola za Marekani 2,000 kwa kila mtu mwaka 2014

. Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, imevutiwa na maendeleo ya nchi hiyo ambayo imetumia muda mfupi kupunguza umasikini wa wananchi wake kwa asilimia 50. Sifa kuu ya Vietnam ni uthubutu na uwezo wa kusimamia mipango yake. Mfano mwaka 1980 nchi hiyo iliamua kuingia kwenye uzalishaji mkubwa wa kahawa.

Ndani ya miaka 10 iliweza kukia uzalishaji wa tani 300,000 kwa mwaka na hatimaye kuwa nchi inayoongoza ulimwenguni katika uzalishaji na uuzaji wa kahawa aina ya Robusta. Vilevile miaka ya 1990, Vietnam ilikuwa ikiagiza mchele kutoka nje, kufuatia hatua madhubuti walizochukua mwaka 2004 ilishika nafasi ya pili duniani katika uzalishaji wa mchele kwa kuwa na misimu mitatu ya mavuno. Mafanikio makubwa ambayo Vietnam imeyapata katika kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo, yamekuwa chachu ya ukuaji wa sekta ya viwanda ambayo kwa sasa ndio imeshika hatamu ya uchumi wa Vietnam. Mkakati wa Mageuzi 2011- 2020 Vietnam inatekeleza mkakati wake wa kuwezesha mageuzi ya kijamii na kiuchumi wa mwaka 2011-2020 ambao umejikita kwenye kuwapatia wananchi elimu na stadi za ufundi kwa ajili ya kufanya kazi kwenye viwanda vinavyotumia teknolojia ya kisasa na ubunifu; kuboresha taasisi zinazoshughulika na masoko; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu.

Mkakati huo unaendana na utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa nchi hiyo ambao kwa sasa umelenga kufanya mageuzi makubwa katika taasisi za kibenki ili kuwezesha wananchi kupata mitaji ya kufanya shughuli za uchumi na maendeleo; na mageuzi ya makapuni ya biashara ya Serikali ili yaweze kushindana katika uchumi wa soko ndani na nje ya nchi pasipo kutegemea ruzuku kutoka serikalini. Ni dhahiri kwamba yapo mambo ambayo Tanzania inaweza kujifunza kutoka Vietnam katika safari yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ikapo mwaka 2025.

Tanzania inayo nafasi kubwa ya kuongeza uzalishaji katika mazao ya miwa, mpunga na uvuvi kwa kupitia ushirikiano na Vietnam. Vietnam ambayo mwaka 1986 ilikuwa na uchumi sawa na Tanzania hivi sasa imepiga hatua kubwa kiuchumi na hawana shida ya upungufu wa chakula kama ambavyo huwa inaweza kutokea katika baadhi ya maeneo Tanzania.

Kwa mfano, ukitembelea wilaya za Igunga na Nzega, utagundua kwamba kuna mabonde mengi yanayoweza kuzalisha mpunga hata mara tatu kwa mwaka lakini hajayaendelezwa kiasi hicho. Ingawa Vietnam ilianza kulima korosho miaka ya hivi karibu kwa sasa zao hilo linaongoza katika kuipatia nchi hiyo mapato mengi toafuti na Tanzania. Nini wamefanya Vietnam? Mtati wa Taasisi ya Utati wa mambo ya Biashara na Uchumi (Repoa) Dk Blandina Kilama ambaye aliwahi kufanya utati wake katika maeneo yanayolima korosho nchini anabainisha kuwa Tanzania ambayo miaka ya nyuma ilisika kwa kuwa miongoni mwa nchi zinazozalishwa kwa wingi korosho zao hilo limezidi kudidimia.


Katika utati wake ambao aliufanya huko Tandahimba mkoani Mtwara na eneo la Binh Phuoc huko Vietam akitaka kubaini kwa nini taifa hilo la Asia limepiga hatua kubwa kimaendeleo hasa katika uzalishaji katika zao la korosho kuliko Tanzania wakati mataifa hayo yanafanana kwa sehemu kubwa, nchini Vietnam uzalishaji wa zao hilo umeongezeka kutokana na sekta hiyo kuwa na wabanguaji wengi. Anasema nchini Vietnam korosho imeanza kulimwa kuanzia miaka ya 1980 na kwa sasa ndilo zao linaloiingizia nchi fedha nyingi za kigeni kuliko ilivyo hapa nchini. Anasema iwapo kutakuwa na wabanguaji wengi nchini kama ilivyo kwa Vietnam ni wazi kuwa wakulima watakuwa na nguvu ya majadiliano ya bei kuliko ilivyo sasa na pengine serikali isingelazimika kuingilia katika ununuzi wa korosho. Wakati wa utati wake, Vietnam ilikuwa na wabanguaji zaidi ya 300.

“Kwa hali hii mbanguaji anachotaka korosho zipatikane hivyo ni lazima wajadiliane na wakulima na kuweka bei inayoridhisha kwani wakulima wa Vietnam akiona bei sio nzuri ataacha kulima zao hilo na kugeukia kwenye kilimo cha mpira,” alisema Dk Kilama. Anasema kitendo cha Tanzania kuwa na wanunuzi wachache wa zao hilo pamoja na wabanguaji kumefanya wakulima kutokuwa na sauti hali ambayo ilifanya wanunuzi kuwa na nguvu hadi kufanya serikali ikaingilia kati miaka ya nyuma na kuweka utaratibu wa stakabadhi ghalani.

Anasema Tanzania ina ardhi kubwa mara tatu ya ile ya Vietnam huku idadi ya watu Tanzania ikiwa ni milioni 45 wakati Vietnam ni milioni 85 huku asilimia 70 ya watu wake kama ilivyo kwa Tanzania wakiishi vijijini. Anasema licha ya uchache wa ardhi yao; lakini katika ekari tatu wanapanda miche 600 ya korosho wakati Tanzania katika eneo hilo kunapandwa miche 200 tu kwa wakulima wadogo wa pande zote. Kwa upande wa wakulima wa kati ambao wanalima ekari sita katika eneo hilo la ardhi, Vietnam kunapandwa miche 1,500 wakati Tanzania wakulima wa kati wanamiliki ekari 10 na wanapanda miche 300.

“Utaona kuwa katika ardhi ndogo wenzetu wanapanda miche mingi wakati sisi ni michache katika ardhi kubwa tuliyo nayo,” anasema Dk Kilama wakati wa utati wake. Anaongeza kuwa wafanyakazi katika mashamba ya mikorosho mkulima mdogo anatumia watu sita wakati Tanzania mkulima anatumia nguvu kazi ya watu 11. Kuhusu idadi ya watu anasema idadi ya kaya ya Tanzania ni sawa na ile ya Vietnam lakini tofauti kwenye kilimo hicho ni kwamba Tanzania wakulima wenyewe wanapalilia na kuokota korosho wakati Vietnam wakati wa mazao nguvu kazi ya kuokota korosho inaongezeka. Hata kwa upande wa pembejeo Tanzania wakulima hawatumii bomba la kunyunyuzi kwa ajili ya kuuawa wadudu kwa vile wanapouza mazao yao wanakopwa hivyo inawawia vigumu kununua dawa za uhakika za kuulia wadudu.

Pia anasema pembejeo yenyewe inategemea serikali kuwapelekea pembejeo ya ruzuku. Kwa upande wa Vietnam wakulima wanafyeka mti kwa kutumia mashine wakati Tanzania wanatumia mapanga na mafyekeo. Mfumo wa soko la Vietnam ni mkulima kwenda kwa mnunuzi ambaye anaenda kuibangua korosho hiyo na kuiuza nje ya nchi. Upande wa soko pia korosho ya Tanzania inauzwa ikiwa gha kwa Serikali ambayo inatumia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao unalalamikiwa na wakulima kuwa hauwalipi. Lakini ni mfumo ambao ulianzishwa baada ya kuona wanunuzi wanakuwa na nguvu kuliko wakulima wenyewe.

Mtaalamu huyu anasema Vietnam na Tanzania zote zilikuwa wajamaa na baada ya mageuzi mengi ya kiuchumi Tanzania iliingia kwenye soko huria na Vietnam ikaenda na mfumo wa Doi Moi ambao ulihamasisha zaidi nchi kujitosheleza kwa chakula kabla ya kuuza nje ya nchi. “Tofauti ni kwama sisi tuliporuhusu soko huria tuliliacha hadi kufanya likawa soko holela na wahisani wakawa na nguvu na sauti wakati Vietnam ilipoachana na ujamaa waliingia kwenye soko huria; lakini wakawa na mfumo ambao wahisani hawakuwa na sauti na hii imewasaidia sana,” anasema Dk Kilama. Bila shaka hatua za Rais Magufuli zinatuelekeza huko waliko wenzetu wa Vietnam
 
Back
Top Bottom