Uzalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzalendo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Boniphace Kichonge, Jan 12, 2018.

 1. Boniphace Kichonge

  Boniphace Kichonge Verified User

  #1
  Jan 12, 2018
  Joined: Jul 31, 2017
  Messages: 1,020
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  LOWASSA ALIWASALITI WENZAKE.

  Na Thadei Ole Mushi.
  Maana halisi ya chama cha siasa ni kikundi cha watu wenye nia moja na Lengo moja la kushika madaraka ya nchi.

  Hii maana imekuwapo karne na karne na ndio msingi na lengo kuu la kuundwa kwa vyama vya siasa.

  Hakuna chama cha Siasa duniani ambacho kiliundwa na hakitambui lengo hili kama lengo la msingi.

  LOWASSA HAFAI TENA KUWA MGOMBEA URAIS KUPITIA UPINZANI.

  Huu ni ukweli ulio uchi kuwa kwa kitendo cha Lowassa kujitokeza hadharani na kusifia serikali ya awamu ya Tano moja kwa moja inamvua sifa ya kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu.

  Kitendo alichokifanya hakina Tofauti na wabunge au madiwani walioamua kujivua nafasi zao na kujiunga ccm kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

  Lowassa amesema kuwa Rais kafanya mazuri sana katika uongozi wake moja kwa moja kaunga Mkono juhudi za Rais Magufuli sasa huyu unamtofautishaje na Dr Molel? Au kina Mtulia?

  Lowassa atapata wapi tena ujasiri wa Kusimama jukwaani na kusema achaguliwe huku yote yaliyofanywa amekubaliana nayo? Litakuwa ni kosa la Kiufundi kweli kama chadema itamchagua tena Lowassa kuwa mgombea Urais 2020.

  Huu ni usaliti katika dhana ya maana ya chama cha Siasa kama nilivyoielezea hapo mwanzo.

  NINI KINAWEZA KUFANYIKA.

  Kwa sasa Chadema inatakiwa ianze kuoiga mahesabu mapya ya nani anauzika kwa wananchi. Kwa upande wao wafikirie majina haya mawili.

  1. Fredrick Sumaye.

  2. Tundu lisu.

  SUMAYE.

  Huyu anafaa kwa sifa moja tu kubwa kwamba aliwahi kushika nafasi kubwa ya kiuongoz nchini lakini hakuwahi kuwa mwanasiasa mkubwa.

  Kuna tofauti kati ya kuwa mwanasiasa mkubwa na Kiongozi mkubwa. Hii ina maana kuwa Sumaye alidondokewa na bahati ya kupitishwa kuwa waziri mkuu na sio kwamba alikuwa na ushawishi kwa jamii kuipata nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka 10.

  HASARA YA SUMAYE.

  Sumaye kama alivyo Lowassa ni mtu mwenye makando kando mengi. Kama ilivyo kwa viongozi wengi wamedhulumu sana taifa hili kwa kujilimbikizia Mali.

  Sumaye naye amekuwa akitajwa tajwa kama ataanza kujiandaa kwa ajili ya kushika form ya urais basi CCM wanajua pa kugusa ili atulie. Na wakipagusa sana anaweza akahamia kabisa CCM kulinda asife maskini. Huu ndio ukweli wenyewe......

  Hawa kina Lowassa wanalinda tu mali zao kwa sasa hawana ubavu tena wa kuzungumza lugha ya kuiondoa ccm madarakan.

  LISU.

  Huyu pamoja na kuwa ni msomi mzuri, ni mwanaharakati na ni mpinzani haswa haswa. Kwa sifa hizo anatosha sana kupeperusha bendera za Chadema Kwa sasa.

  Huyu hakuwahi kushika nafasi kubwa za kiuongozi ila ni mwanasiasa mkubwa sana kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki.. angelikuwa CCM huyu ni dhahiri angeliteuliwa kushika nafasi kubwa kabisa za Kiuongozi.

  Narudia kama tunataka kuona kampeni zenye mvuto 2020 Lisu ndio chaguo pekee la Chadema. Wakimsimamisha huyu atatusumbua sana CCM.

  HASARA YA LISU.

  Kipingamizi kikubwa cha Lisu kwa sasa ni Afya yake. Lisu anatakiwa kwa sasa apiganie zaidi Afya yake kuliko kitu kingine kile.

  Kipingamizi cha pili cha lisu hana agenda ya msingi ya Kiuchumi ya kumpeleka Ikulu zaidi ya kuwa mkosoaji mkubwa. Lisu anapaswa sasa kuanza kuonyesha Plan B zake katika maswala ya kitaifa yaani kama jambo limefeli yeye kama yeye angelifanyaje.

  Naamini na ndivyo ilivyo kiongozi mzuri ni yule mwenye maono yake juu ya mambo flan yaani mawazo yake binafsi na sio ya kuandikiwa (Ilani) na ndio maana hata Rais wetu kuna saa anaweka ilani Pembeni na kunyoosha kwa namna anavyoamini yeye.

  Lisu anatakiwa sasa atuonyeshe nje ya Ukosoaji wake nini plan na Dira yake kwa taifa hili.

  Ole Mushi
  0712702602
   
 2. M

  MBITIYAZA JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2018
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 14,516
  Likes Received: 23,643
  Trophy Points: 280
  wamefanya nn !
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...