Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,585
Nachukia sana tabia ya wana CCM kujifanya wao ndiyo wana kipimo cha Uzalendo wa watanzania wenzao. Yaani wanapoongea kuhusu Tanzania ni kama vile wasio wana CCM watanzania si wazalendo ama ni watu ambao wapo Tanzania kwa bahati mbaya.
Sifa mojawapo ya Uzalendo ni kulipa Kodi. Huwa najiuliza kama itakuwa sawa kwa wale wasioonekana kuwa si wazalendo kwa vigezo vya wana CCM kuacha kulipa kodi? Hata kauli za viongozi wanaojifanya wanataka mshikamano na umoja wa taifa letu hata wao huwa wanatoa kauli zinazokera sana. Unatafutaje umoja kwa kufanya abaguzi?