Uzalendo wa Mwl Nyerere: Alimtoa mwanae kwenda vitani Uganda. Je, Mwinyi, Mkapa na Kikwete?

Nisilolifahamu vizuri ni baadhi ya watoto wa Mwalimu kuonekana kama wagonjwa wa akili vile na chapombe kwa sana kama huyu Makongoro na Rosemary. Kwa malezi nyumbani Mwalimu hakuwa mzuri sana. Hakuwa na muda? Mzee Karume hakwenda shule. Watoto wake wawili wamefika mbali. Mzee Ali Hassan Mwinyi watoto wake wengi wamesoma vizuri na wana nafasi zao. Infact, yule aliyegombea ubunge wa EALA jana alijieleza vizuri kuliko mgombea yeyote.

Mkuu kua mlevi nafikiri si tatizo la kimalezi,kuna umri ukifika mtu unakua na maamuzi yako mwenyewe,kuhusu elimu mbona hata watoto wa Nyerere sio wazembe sana kielimu?magige ni engineer,makongoro ana masters ya Edinburgh university,John na Andrew walikua ma pilot,Rose nae nafikiri ana elimu yake nzuri tu!tofauti ya Nyerere na waliomfuata yeye hakuwapa nyadhifa/vyeo vya serikali kama hawa wengine!kuhusu ulevi mbona Abbas Mwinyi na Miraji Kikwete ni walevi wa kutupwa?
 
true kamanda ..... mzee mwinyi alimkimbizia Hussein Mwinyi Turkey kusomea udaktari ....mara tu baada ya kumaliza form six..ili kumkwepesha na JKT...Tuseme sio Mwinyi pekee aliyechangia jeshi kufutwa ....kwanza kulikuwa na changamoto za benki ya dunia ,walikuwa hawalitai kabisa ...labda walikuwa na sababu za kimkakati ,.....na kuangalia uwezo wa Tanzana kivita ulioopelekea kupiana vita ya uganda,msumbiji,zimbwabwe ,angola na operesheni zake za kikachero south africa,nmibia na Angola....hii iliwatisha......pili ni ukiritimba wa maafisa wa serikali ya mwinyi waliokuwa wakikusudi kuwacheleweshea pesa jkt ..ili tu kujenga hoja kuwa serikali haiwezi kulihudumia ili tu watoto wao wasiende jkt........

kwa kuongezea Tanzania ilikuwa nchi pekee ya kiafrika iliyopata kuikalia nchi zingine ,,,na ikaondoka kwa hiari bila kuwaibia......kama alivyosema makongoro jana ,...baada ya ushindi wa vita mwaka 1979 wao kama maaskari na maafisa wa jeshi [chini ya maj gen msuya..enzi hizo kanali],polisi [akiwamo mahita]....waliendelea kuitawala uganda hadi mwaka 1982 na bado waliendelea kukaa hadi kusimamia ulinzi wa ndani na mipaka hadi Obote alivyoingia mara ya pili...waliondoka baada ya Nyerere kuona Obote hashauriki..n ushahidi ni kuwa Majeshi ta Tanzania yalipoondoka tu uganda ..vita vikaibuka upya......nyerere alikuwa na uwezo wa kufanya uganda kolonni...

pia tanzania imepata kuitawala Sychells kwa siku kadhaa baada ya kuzima mapinduzi '...pale na kanali iddi ganhu ,baadaye luteni jenerali na mnadhimu enzi ya mkapa ....alikuwa gavana kwa muda tu pale....hadi uchaguzi ukafanyika.....akarudi ....ache re -union etc

Wakati wa mkapa tena jeshi letu kwa kiasi kikubwa ndilo lilikuwa likimlinda kabila mkubwa ...na alipotofautiana na maafisa wa jeshi letu kwa kuchonganishwa na mapandikizi ya rwanda ndipo walipata fursa ya kumuuwa
Mkuu nisahihishe kidogo. Hussein Mwinyi hakumaliza Form Six. Aliondoka kwenda kusomea udaktari akiwa kidato cha tano pale Tambaza! Kama sikosei zilikua ni nafasi zinatolewa kupitia taasisi moja ya Kiislamu ambayo imeishapigwa marufuku hapa nchini. Ni waziri wa Ulinzi raia kweli kweli ambaye hajawahi pitia mafunzo yoyote ya ukakamavu!!!
 
Nilifurahi sana Makongoro Nyerere alipogusia bungeni ushindi walioiletea tz baada ya uvamizi wa IDD AMIN DADAA,najiuliza marais waliomrithi Nyerere wamepeleka watoto wao vitani kama vile kulinda amani Somalia,Comoro,Burundi nk au wanao siku hizi ni kupelekwa kusoma ulaya na kuja kugombea vyeo vya juu vilivoachwa na wazazi wao?. Mwenye details za mtoto wa rais mwanajeshi au polisi kwa sasa aujuze umma wa Watanzania

Kwa mimi ninavyojua na baadhi ya watoto wake JK Nyerere kuwafahamu sijawahi kusikia hata mmoja kuwa aliweza kusoma na kufikia level ya Degree.

Wengi waliishia form four tu na baadhi ndio kama hao aliwapeleka jeshini.

sasa marais waliofuatia waliwekeza katika Elimu. Mfano Mwinyi, ndio hao akina Dr Husein na wengine wengi wasomi. Akina mkapa nao kadhalika na akina Kikwete ndio hao akina Ridhwan ambao ni wanasharia na mawakili.

Kamanda MBOWE yeye alifikia cheo gani jeshini. Maana yeye naye anajeshi lake la ukombozi. Vile vile na yeye si kama makongoro.
 
Mkuu nisahihishe kidogo. Hussein Mwinyi hakumaliza Form Six. Aliondoka kwenda kusomea udaktari akiwa kidato cha tano pale Tambaza! Kama sikosei zilikua ni nafasi zinatolewa kupitia taasisi moja ya Kiislamu ambayo imeishapigwa marufuku hapa nchini. Ni waziri wa Ulinzi raia kweli kweli ambaye hajawahi pitia mafunzo yoyote ya ukakamavu!!!
Ni kweli alisomea nje na aliporudi akajiunga na jeshi na amewpigana vita yake ya kwanza pale gongolamboto na ya pili pale mbagala safi sana!
 
NIMEIFUTA KAULI YANGU;

reason;

i was wrongly informed.

munisamehe kwa usumbufu uliojitokeza.
mtoto wa nyerere hakufia vitani, lakini nasisitiza idi amini zilimnyeshea za masika hilo halina ubishi!!!!!!!

Very admirable!
 
Mkuu kua mlevi nafikiri si tatizo la kimalezi,kuna umri ukifika mtu unakua na maamuzi yako mwenyewe,kuhusu elimu mbona hata watoto wa Nyerere sio wazembe sana kielimu?magige ni engineer,makongoro ana masters ya Edinburgh university,John na Andrew walikua ma pilot,Rose nae nafikiri ana elimu yake nzuri tu!tofauti ya Nyerere na waliomfuata yeye hakuwapa nyadhifa/vyeo vya serikali kama hawa wengine!kuhusu ulevi mbona Abbas Mwinyi na Miraji Kikwete ni walevi wa kutupwa?
Well said mkuu,nafikiri pia masuala ya ulevi saa nyingine hutokana na msongo wa mawazo,hawa watoto wa nyerere wanajikuta wametengwa na system halafu wanawaona baadhi ya wale waliokuwa wakijidai wafuasi wa baba yao hapo awali wanatanua huku wao wakisaga sori za viatu mitaani.unadhani ni nini inakuwa matokeo yake?
Pia nafikiri watu wengi tu wakubwa ni walevi wakubwa,tofauti inakuja pale ambapo wengine wanalewea kwenye MINI BAR zilizoko kwenye mahekalu yao na akianguka anabebwa aidha na bodyguards au wapambe wa ndani ya nyumba wakishirikiana na mama mji na siri inabaki sirini.
Hawa wa mwalimu wao hawana mahekalu kama hayo na walizowea kujichanganya kama raia wa kawaida na pale inapotokea mtindi ukakolea basi wao hawana wa kuwafichia siri.
 
Kajipange upya marubani watoto wa Nyerere hakuna aliyefia vitani,wote wapo Andrew na John wapo hai ni wanajeshi wastaafu hadi sasa

Inaonekana we ni mtoto wa Samaki nchanga anayebishana na familia ya baba wa watanania wote
 
NIMEIFUTA KAULI YANGU;

reason;

i was wrongly informed.

munisamehe kwa usumbufu uliojitokeza.
mtoto wa nyerere hakufia vitani, lakini nasisitiza idi amini zilimnyeshea za masika hilo halina ubishi!!!!!!!
Huu ndio uungwana. Usisahau kumkumbusha yule binti yako wa std 4 naye afute historia uliyomfundisha kwani imempotosha.
 
Nilifurahi sana Makongoro Nyerere alipogusia bungeni ushindi walioiletea tz baada ya uvamizi wa IDD AMIN DADAA,najiuliza marais waliomrithi Nyerere wamepeleka watoto wao vitani kama vile kulinda amani Somalia,Comoro,Burundi nk au wanao siku hizi ni kupelekwa kusoma ulaya na kuja kugombea vyeo vya juu vilivoachwa na wazazi wao?. Mwenye details za mtoto wa rais mwanajeshi au polisi kwa sasa aujuze umma wa Watanzania

Mwinyi yeye mwanae amepewa uwaziri wa ulinzi japo ni Dr sijui wa mifugo au binadamu

Mkapa yeye nafikiri tumuulize Two Money manake wa kwake wako share

Jk yeye wa kwake anasimamia bei za mafuta bongo..

Halafu kumalizia Tanzania tumewahi kuwa na raisi mmoja tu. Wengine jaza....
 
Usilinganishe kifo na usingizi. Nyerere hakuwa juha, mwoga, mwongo, fisadi, msanii, mzuraraji wala mbabaishaji. Nyerere alikuwa na uchungu na nchi siyo hawa wenye uchu na nchi.
 
NIMEIFUTA KAULI YANGU;

reason;

i was wrongly informed.

munisamehe kwa usumbufu uliojitokeza.
mtoto wa nyerere hakufia vitani, lakini nasisitiza idi amini zilimnyeshea za masika hilo halina ubishi!!!!!!!

Wewe omba radhi na piga kimya hakuna haja ya kuanza kujitetea na kujusitfy your incompetency bwana
 
hongera kwa uungwana, posibly wewe ni CHADEMA, ungekuwa ni mCCM ungekomaa hata km umeujua ukweli. Tunahitaji watu wenye tabia hiyo wakikosea wanakubali.
Peoplesss pooooooooooooooooooooooooooooooooooooower
 
Dah! Nadhani wewe ndo unatakiwa ukafanye homework yako upya na vizuri zaidi. Habari za kifo cha rubani mtoto wa Nyerere hata binti yangu wa std 4 anazijua.

Mkuu ni kweli kuna mtoto wa Kambarage aliyekuwa rubani wa ndege za kivita lakini yu hai, hakufa vitani.
 
Hata ukiangali ni watoto wa Nyerere tu ndio waliokwenda Jeshini - Wa Mwinyi, Wa Mkapa, Wa Kikwete hakuna

Na Mwinyi yeye ndie alieyeondoa JKT sababu watoto wake walifikia umri wa kwenda angalia sasa

Mmoja waziri wa Ulinzi mwingine Mbunge wa East Africa
 
Kajipange upya marubani watoto wa Nyerere hakuna aliyefia vitani,wote wapo Andrew na John wapo hai ni wanajeshi wastaafu hadi sasa

Dah! Nadhani wewe ndo unatakiwa ukafanye homework yako upya na vizuri zaidi. Habari za kifo cha rubani mtoto wa Nyerere hata binti yangu wa std 4 anazijua.

Mkuu jamaa ana point usimbishie. Unajua wakati wa Mwl ulikuwa wakati wa giza kwa watanzania wengi na wengi wetu tulikuwatukipata habari kupitia redio mbao. Hebu fuatilia hii thread hapa chini ujiridhishe. Inawezekana habari za kifo cha mtoto wa Mwl wakati wa vita ilikuwa ni strategy ya ku-boost Morale wa Askari na kushinda vita. Inawezekana ilikuwa ni mbinu ya kuonesha askari na watanzania kuwa Nyerere is also a victim of the war by losing his son kama kweli habari hizo zilikuwepo.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/27134-andrew-nyerere-on-mwalimu-humble-children.html
 
Kwa mimi ninavyojua na baadhi ya watoto wake JK Nyerere kuwafahamu sijawahi kusikia hata mmoja kuwa aliweza kusoma na kufikia level ya Degree.

Wengi waliishia form four tu na baadhi ndio kama hao aliwapeleka jeshini.

sasa marais waliofuatia waliwekeza katika Elimu. Mfano Mwinyi, ndio hao akina Dr Husein na wengine wengi wasomi. Akina mkapa nao kadhalika na akina Kikwete ndio hao akina Ridhwan ambao ni wanasharia na mawakili.

Basi huwafahamu watoto wa Nyerere. Magige ni engineer kama alivyotaja hapo juu 1800. Anna ana degree mbili za elimu kutoka Carlton University, Canada. Vile vile Madaraka. John na Andrew walijiunga jeshini baada ya kumaliza masomo yao ya A level. Usiwe unasema vitu usivyokuwa na hakika navyo, unatupunguzia sifa zetu hapa JF kama great thinkers.
 
Back
Top Bottom