Uzalendo wa Mwl Nyerere: Alimtoa mwanae kwenda vitani Uganda. Je, Mwinyi, Mkapa na Kikwete?

hapana ndugu yangu, fanya utafiti kwanza kwa ulisemalo hapa JF.Mtoto wa nyerere rubani anaitwa Endrea/enduru yupo ni mzima mpaka sasa hakufa anaishi hapa dar es salaam.Makongoro ni mtalaam wa kutengua mabomu na mengineyo ni askari mzuri pia, John naye alikuwa askari alistaafu.hao ndiyo wanae mwalimu maaskari.hakuna aliyekufa usipotoshe umma.

Salute mkuu!!

ila ni kweli zilimnyeshea za masika huyu iddi amini
 
Je tukishambuliwa hivi leo ,wananchi wana hanasa ya kulinda nchi yao kama walivyomshuhulikia Amin?Kama hawana hamasa hiyo kwanini?
 
To put the records in a correct way, Nyerere alikuwa na adopted daughter mmoja na adopted son mmoja. Adopted daughter yuko hai na adopted son ndiye alikuwa mwanajeshi na ndiye aliyekufa from enemy fire. Kiasi habari yako ilikuwa na ukweli lakini haikusimama sawasawa
 
Huko ndio kuongoza kwa mfano na sio kwa mashairi. Mwalimu alisimamia umoja na umoja unaanzia nyumbani. Vita ni kafara ya nchi na hakuna njia nzuri ya kuhamasisha wazazi waruhusu watoto wao kwenda vitani bila ya kiongozi naye kuonyesha mfano.
Kuna mifano mingi tu ya namna Mwalimu alivyotenda yale aliyohubiri na sio kama hawa wa siku hizi wenye kutuambia tuwajibike ilihali wao wanaponda nchi. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Amiri jeshi mkuu aliyeiva ..lazima aongoze kwa mfano ......kitendo cha nyerere kuwatoa watoto wake wa tatu kwenda mstari wa mbele ilikuwa cha kijasiri...akiwamo Makongoro akiwa na umri wa miaka 18 tu............hata uingereza malkia watoto na wajukuu zake wanapigana mstari wa mbele...
 
sera za nyerere kila raia awe askari ndo maana ilikuepo jkt,mabalozi walirudishwa nyumbani kufanya kozi ya uaskari haijalishi cheo au familia lzm upitie jeshini,sera imebadilika si watoto wa maraisi wengine sote kizazi kipya hata jkt hatujaenda
 
Nilifurahi sana Makongoro Nyerere alipogusia bungeni ushindi walioiletea tz baada ya uvamizi wa IDD AMIN DADAA,najiuliza marais waliomrithi Nyerere wamepeleka watoto wao vitani kama vile kulinda amani Somalia,Comoro,Burundi nk au wanao siku hizi ni kupelekwa kusoma ulaya na kuja kugombea vyeo vya juu vilivoachwa na wazazi wao?. Mwenye details za mtoto wa rais mwanajeshi au polisi kwa sasa aujuze umma wa Watanzania
Hata hao wengine wamewapeleka watoto wao mstari wa mbele kutuibia.
 
Nilifurahi sana Makongoro Nyerere alipogusia bungeni ushindi walioiletea tz baada ya uvamizi wa IDD AMIN DADAA,najiuliza marais waliomrithi Nyerere wamepeleka watoto wao vitani kama vile kulinda amani Somalia,Comoro,Burundi nk au wanao siku hizi ni kupelekwa kusoma ulaya na kuja kugombea vyeo vya juu vilivoachwa na wazazi wao?. Mwenye details za mtoto wa rais mwanajeshi au polisi kwa sasa aujuze umma wa Watanzania

Nyerere alikua na watoto watatu ambao walikua ni wanajeshi,wawili walikua ni marubani wa jet fighters ambao ni Andrew na John,wakati Makongoro yeye alikua ni captain wa jeshi kwa cheo na ni mtaalam wa mabomu
 
Natamani nipate maoni toka kwa wachambuzi hasi wa utawala wa Baba wa Taifa, katika hili!
 
Nilifurahi sana Makongoro Nyerere alipogusia bungeni ushindi walioiletea tz baada ya uvamizi wa IDD AMIN DADAA,najiuliza marais waliomrithi Nyerere wamepeleka watoto wao vitani kama vile kulinda amani Somalia,Comoro,Burundi nk au wanao siku hizi ni kupelekwa kusoma ulaya na kuja kugombea vyeo vya juu vilivoachwa na wazazi wao?. Mwenye details za mtoto wa rais mwanajeshi au polisi kwa sasa aujuze umma wa Watanzania

Kuna Mtoto wa Mwinyi alikuwa Mjeshi tena alikuwa Major kama sikosei!
 
Amiri jeshi mkuu aliyeiva ..lazima aongoze kwa mfano ......kitendo cha nyerere kuwatoa watoto wake wa tatu kwenda mstari wa mbele ilikuwa cha kijasiri...akiwamo Makongoro akiwa na umri wa miaka 18 tu............hata uingereza malkia watoto na wajukuu zake wanapigana mstari wa mbele

1800

Nyerere alikua na watoto watatu ambao walikua ni wanajeshi,wawili walikua ni marubani wa jet fighters ambao ni Andrew na John,wakati Makongoro yeye alikua ni captain wa jeshi kwa cheo na ni mtaalam wa mabomu..

Makongoro alikua Kapteni akiwa na umri wa miaka 18??
 
Member of East African Parliments Elected!
1301.jpg

shy+ccm.jpg
 
Kuna ndege ilitunguliwa Rwamlimi jirani na Musoma alliance na inasemekana rubani alikuwa ni mtoto wa Nyerere na alifariki. Hapo Rwamlini kuna kibao cha kumbukumbu mimi nilishasahau jina maana nilisoma huko early 90s.
 
Huko ndio kuongoza kwa mfano na sio kwa mashairi. Mwalimu alisimamia umoja na umoja unaanzia nyumbani. Vita ni kafara ya nchi na hakuna njia nzuri ya kuhamasisha wazazi waruhusu watoto wao kwenda vitani bila ya kiongozi naye kuonyesha mfano.
Kuna mifano mingi tu ya namna Mwalimu alivyotenda yale aliyohubiri na sio kama hawa wa siku hizi wenye kutuambia tuwajibike ilihali wao wanaponda nchi. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Huko kwao anakotoka (Musoma) enzi hizo Jeshi ndio ilikuwa kazi yenye sifa kwa mwanaume kuliko kazi zingine zote, hivyo ni dhahiri kwamba Nyerere pia-kama wazazi wengine wote- aliwapatia wanawe kazi yenye hadhi kwa wakati husika.
 
NIMEIFUTA KAULI YANGU; reason; i was wrongly informed. munisamehe kwa usumbufu uliojitokeza. mtoto wa nyerere hakufia vitani, lakini nasisitiza idi amini zilimnyeshea za masika hilo halina ubishi!!!!!!!
umesamehewa.
 
Nilifurahi sana Makongoro Nyerere alipogusia bungeni ushindi walioiletea tz baada ya uvamizi wa IDD AMIN DADAA,najiuliza marais waliomrithi Nyerere wamepeleka watoto wao vitani kama vile kulinda amani Somalia,Comoro,Burundi nk au wanao siku hizi ni kupelekwa kusoma ulaya na kuja kugombea vyeo vya juu vilivoachwa na wazazi wao?. Mwenye details za mtoto wa rais mwanajeshi au polisi kwa sasa aujuze umma wa Watanzania

Nyerere ni saint, nilikua na mwanasiasa mmoja siku moja na akaniambia jinsi walivyoshangzwa na Mwalimu alipoona anashindwa kulipia nyumba pale Msasani akairudisha kwa serikali wakati wa enzi za mwinyi, kwa aibu kubwa Serikali baada ya muda ikakaa na kumsamehe malipo yaliobaki na kumpa ile nyumba pale Msasani.. Jamaa anasema hata kitendo cha kuilipia tu kilikua ni uzalendo wa hali ya juu kwa mwanzilishi wa taifa asiye na mali yeote mji mkuu wa kibiashara na kimataifa wa nchi
 
Nilifurahi sana Makongoro Nyerere alipogusia bungeni ushindi walioiletea tz baada ya uvamizi wa IDD AMIN DADAA,najiuliza marais waliomrithi Nyerere wamepeleka watoto wao vitani kama vile kulinda amani Somalia,Comoro,Burundi nk au wanao siku hizi ni kupelekwa kusoma ulaya na kuja kugombea vyeo vya juu vilivoachwa na wazazi wao?. Mwenye details za mtoto wa rais mwanajeshi au polisi kwa sasa aujuze umma wa Watanzania

Nadhani uko sawa kabisa.hawa wa siku hizi nao wanawatuma vitani ndiyo, ila tofauti ni aina ya majeshi mfano
*HUSSEN ALLY MWINYI, amejiunga na jeshi na amepigana pale mbagala na Gongolamboto hivi karibuni na kufanikiwa kuwafurusha wakazi wa dar es salaam kwa siku kadhaa na wengine bado wako kwenye kambi za wakimbizi.

*RIZ ONE K,amejiunga na jeshi la mafi**di na sasa wanaendelea kusonga mbele wakiwachakaza watanzania sehemu mbalimbali nchini hadi kupelekea wananchi kuanza harakati zao binafsi na wakijinunulia magwanda kwa kuchangishana na kuanzisha falsafa yao ya peoples power ili kupambana na jeshi hilo hatari
 
Back
Top Bottom