Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
Kumbe kabla ya zama za Barick na FIPA kulikuwa na uzalendo wa hali ya juu miongoni mwa viongozi na wasomi wetu katika kufuatilia usiri wa makampuni ya madini ya kigeni nchini. Enzi hizo Mzalendo Mwalimu Nyerere alikuwa na tabia ya kuwakabidhi viongozi kazi ya kuchunguza nyendo za makampuni mbalimbali ili yasitunyonye. Kwa mujibu wa Waziri wa Zamani katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Al Noor Kassum, Nyerere aliwahi kumkabidhi jukumu la kufuatilia nyendo za siri za Kampuni ya madini ya De Beers katika mgodi wa almasi (Williamsond Diamonds) wa Mwadui. Hivi ndivyo anavyobainisha Kassum kwa Kiingereza katika ukurasa wa 85 wa kitabu chake kipya cha 'Africa's Wind of Change', yaani, 'Upepo wa Mabadiliko Afrika':
When Mwalimu told me what he had in mind, I was surprised and said: 'But I am a lawyer! I have done all these international jobs... I don't know anything about diamonds!' He said, 'Don't worry, just go there, stay for a while, let's see what happens. I just want you to go there.' I said, 'All right, if that is what you want.' Mwalimu said he wanted me to find out what was going on at the company since it was being very secretive about its operations. [Mwalimu aliponieleza alichodhamiria, nilipatwa na mshangao na kuhamaki: 'Lakini mimi ni mwanasheria! Nimefanya kazi zote zile za Kimataifa...Sijui lolote kuhusu almasi!' Mwalimu akanijibu, ' Usiwe na wasiwasi,wewe nenda tu, kaa kwa muda, tuone nini kitatokea. Nataka tu uende kule.' Nikamwambia, 'Sawa, kama hivyo ndivyo unavyotaka.' Mwalimu akasema kuwa anataka niende kuchunguza nini kinaendelea katika kampuni hiyo maana ilikuwa inaendesha shughuli zake kwa siri sana.']
Kassum alikwenda huko kama alivyoagizwa, na ingawa Waingereza na Makaburu wa De Beers walimweka pembezoni katika vikao vya menejiment japo alikuwa Meneja Mkuu Msaidizi, alifanikiwa kupata taarifa nyeti zilizokuja kuisadia Tanzania. Kwa kushirikiana na aliyekuwa Mzalendo Basil Mramba waliandika ripoti nzito ya 'The Future of Mwadui', yaani 'Hatma ya Mwadui', ambayo iliwakasirisha sana menejimenti ya De Beers. Kwa mfano ripoti hiyo iligundua kuwa Williamson Diamonds ilikuwa inamiliki kamgodi kwa jina la New Alamasi kalikokuwa hukohuko Mwadui. Kamgodi haka kalikuwa kanasamehewa kulipa ushuru wa almasi wa 5% kwa kuwa kalikuwa hakazalishi almasi ya kiwango cha kulipia ushuru huo kisheria. Lakini cha ajabu ni kuwa haka kamgodi kalikuwa mali (au sehemu ya) Williamson Diamonds ambayo yenyewe ilikuwa inazalisha madini kwa kiwango kinachotakiwa kutozwa ushuru huo. Pia cha ajabu ni kuwa Williamson Diamonds ilikuwa inatozwa mrahaba wa 15% wakati katoto kake,yaani New Alamasi, kalikuwa kanatozwa 7.5% tu!
Kwa ufupi mwisho wa siku ripoti ya Kassum na Mramba ililisaidia Taifa kufanya mabadiliko ya uongozi ambapo Matthew Luhanga aliteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Williamson Diamonds. Pengine ni muhimu tukirejea baadhi ya mapendekezo ya ripoti hii hasa wakati huu ambapo tunapata mirahaba finyu baada ya kujiingiza kwenye mikataba ya ajabu ya madini. Pendekezo lililonivutia zaidi ni kuhusu 'sera ya kutochimba madini kupita kiasi' (overmining policy). Nikilielewa vizuri nitalielezea kwa undani zaidi. Kwa sasa naishia hapa. Nawasilisha.