Uzalendo wa kweli hautaki chembe chembe za ubaguzi

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Heshima kwa Wakuu,
Awali ya yote naungana na wote wanaoitakia mema Tanzania. Hawa ni watu wanaounga mkono jitihada za rais Magufuli kufuatilia ikiwa rasilimali za nchi zinavunwa na zinanufaisha wananchi kama inavyopaswa. Ameonesha uthubutu ambao wenzake waliotangulia hawakuuwaza.

Katika vita ya kutetea maslahi ya nchi ,lazima tuwe wamoja kwa kuwa Tanzania ni yetu site. Hakuna mwenye haki kuliko mwingine. Wanaotakiwa kuanzisha vita ya kupigania rasilimali zetu zisiibiwe ni wawakilishi wetu, waheshimiwa wabunge.

Inavyoonekana ni kuwa wawakilishi wa wananchi siyo kitu kimoja. Badala ya kuungana na wenzao kuibana Serikali ili mikataba ya madini ijadiliwe kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa, wabunge wengine, wabunge wa Chama Chetu Chakufaana wameamua kuasi wajibu wao wa uwakilishi wa wananchi na kuamua kuunga mkono mikataba ya kinyonyaji inayopora rasilimali za nchi na kutuachia hela ya mboga.

Jambo hili walilifanya kwa kutumia nguvu nyingi za kiwango cha hata kudiriki kufukuza wenzao Bungeni na walipohoji walifurushwa kwa kubebwa juu juu kama vibaka na mgambo wa Bunge. Mikataba ya uchimbaji dhahabu na mikataba ya mafuta na gesi ni mifano mizuri.

Mh. Zito akiwa CHADEMA alifukuzwa Bungeni mwaka 2007 baada ya kuambiwa amelidanganya Bunge kwa kutoa taarifa ya kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi amesaini mkataba kinyemera akiwa hotelini London, Uingereza. Ilibainika kuwa Zito alikuwa sahihi.

Katika kikao cha kujadili bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa 2017/2018,Mh. Mnyika mbunge wa Kibamba alibebwa mzobemzobe na kutupwa nje kwa kuhoji kwa nini anaitwa mwizi(wa madini) na mwenzake Mh. Lusinde. Wabunge wa CCM wanaona kuwa wezi wa madini si wawekezaji Bali in wabunge wenzao wa upinzani! Wanatetea wizi kwa kufukuza wenzao Bungeni.

Jambo jingine la kusikitisha ni kitendo cha kibaguzi cha kuwasafisha marais wastaafu Mh. Mkapa na Mh. Kikwete kuwa hawahusiki na mikataba ya kinyonyaji ila mawaziri husika, mawaziri wakuu wastaafu, makamishna na wanasheria wa kipindi husika.

Hapa kuna Mh. Lowasa na mwenzake Sumaye, waliokuwa mawazirj wakuu. Mawaziri wa madini ni Abdalah Kigoda(marehemu), Daniel Yona na Nazir Karamagi, Edgar Maokola Majogo, Prof. Muhongo, Dr. Ibrahim Msabaha, Lawrence Masha, Bernard Membe, William Ngeleja, Adam Kighoma Malima, Steven Masele na George Simbachawene.

Makamishna ni Paulo Masanja, Dalali Kafumu na Ali Samaje. Wanasheria Wakuu na wasaidizi wao, ambao ni washauri wa Serikali kwa mambo ya sheria ni Andrew Change, Johnson Mwanyika, Felix Mrema, Sazi Salula, Maria Kejo na Julius Malaba.

Watumishi hawa wa Umma walihudumu toka mwaka 1998 mpaka karibu na mwisho wa muhula wa awamu ya nne.Majina haya yametajwa katika ripoti ya Kamati ya Pili ya Mh. Rais ya kuchunguza madini katika mchanga/makinikia. Ripoti hii bado haijawekwa wazi ili wananchi waijadili.

Katika kuwasafisha marais wastaafu, Mh. Palamagamba Kabudi Waziri wa Sheria amenishangaza kwa kusema wametumikia nchi kwa hiyo wasihusishwe.

Spika Ndugai alimkemea Mbunge wa Kilombero Mh. Lijualikali kwa kumwambia kuwa hata upande wa pili kuna mawaziri wakuu wastaafu(Lowasa na Sumaye) .Mh Zungu akiwa mwenyekiti wa Bunge, alisoma vifungu vinavyowa-exclude marais wastaafu kwenye tuhuma za mikataba mibovu ingawa wanakuwa wenyeviti wa vikao vya baraza la mawaziri.

Katika kutetea marais wastaafu, panga limewashukia gazeti la Mawio kwa kuandika kisichopendwa na Mh. rais Magufuli, kuhusisha Mh. Mkapa na Mh. Kikwete na mikataba ya kinyonyaji. Wamefungiwa kwa miezi 24.

Napenda nirudie kusema kuwa nia ya rais ni njema lakini asibague watu katika vita hii, wala asizuie mijadala kwenye media na fora mbalimbali. Kazi ya kutia mtuhumiwa hatiani ni kazi ya mahakama pekee, siyo ya chama au serikali.

Kuna uwezekano mkubwa, na sitashangaa wanaotajwa kuchunguzwa wakiwa acquitted na mahakama.Watu wachunguzwe, ushahidi utolewe na mahakama iamue.Katika nchi yoyote ya Kidemokrasia, mawazo na hoja tofautitofauti ndiyo msingi wa kujenga nchi na kuleta maendeleo.

Mawazo kwamba sisi ndiyo tumepewa dhamana ya nchi kwa hiyo mawazo mbadala hayatakiwi, yamepitwa na wakati. Tuwe wamoja, tupingane kwa hoja, tusibaguane, tusitafute sifa za kichama na kutoana kafara. Tusizuie mawazo mbadala,hayo ni afya ya nchi.

Mungu ibariki Tanzania.
 
well said mkuu Ila MaCCM yanataka kujifanya ndo yana tetea rasilimali wakati wao ndo walishirikiana na wezi kusaini mikabata mibovu ya kupora rasilimali zetu,waache ubaguzi nchi yetu sote tuwe kitu kimoja
 
well said mkuu Ila MaCCM yanataka kujifanya ndo yana tetea rasilimali wakati wao ndo walishirikiana na wezi kusaini mikabata mibovu ya kupora rasilimali zetu,waache ubaguzi nchi yetu sote tuwe kitu kimoja
Ccm ni nambali wani kwa wizi aisee
 
Watu ni wazalendo kweli kweli ila tatizo CCM hawapendi kuona watu wanakuwa wazalendo
 
umeongea vizuri sana, ombi langu ni kuwa mkumbushe na tundu lissu nae asiwe na ubaguzi katika kuwataja wahusika....tuyasikie na majina ya lowassa na sumaye akiyataja kwa kinywa chake, na hili lianze kesho. ayapange maneno vizuri ili na majina hayo yapate nafasi ya kutajwa. tafadhali fanya hivyo!
 
well said mkuu Ila MaCCM yanataka kujifanya ndo yana tetea rasilimali wakati wao ndo walishirikiana na wezi kusaini mikabata mibovu ya kupora rasilimali zetu,waache ubaguzi nchi yetu sote tuwe kitu kimoja
Well said my brother.
 
umeongea vizuri sana, ombi langu ni kuwa mkumbushe na tundu lissu nae asiwe na ubaguzi katika kuwataja wahusika....tuyasikie na majina ya lowassa na sumaye akiyataja kwa kinywa chake, na hili lianze kesho. ayapange maneno vizuri ili na majina hayo yapate nafasi ya kutajwa. tafadhali fanya hivyo!
Saw a Mkuu
 
Back
Top Bottom