Uzalendo wa “Itikadi” Binafsi kutumia Mgongo wa Maslahi ya Jumla ya Taifa

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Kuna kitu kimoja kimeendelea kwa muda mrefu sasa na si ajabu tangu tupate Uhuru wetu nacho chaendana sambamba na jinsi Chama Tawala (TANU/ASP mpaka sasa CCM) ambapo kuna nguvu kubwa sana za muonekano wa kutetea na kulinda maslahi ya Taifa lakini kila mwaka na kila awamu mpya, udhahiri wa Maisha ya Mtanzania bado uko pale pale na hauendani na “uendelevu” wa vitu vionekanavyo kwa macho (Majengo ya Kisasa, Majumba, Magari ya Kisasa, Miundombinu, Uwekezaji) na kusadikika ni kwa manufaa ya Taifa. Aidha kuna uendelevu mwingine wa ukuaji wa maslahi binafsi wa watendaji na wapambe wa Viongozi wakuu wa nchi.

Natafakari sana jinsi gani Awamu ya Tano inavyojikita katika kutoa sifa na hoja za uwasili na utimilifu wa Safari mpya ya Maendeleo ya Tanzania na nguvu kubwa inayotumika kurembesha na kusifia mipango na “matokeo” ya umakini wa utendaji wa Awamu ya Tano hasa Rais Magufuli n ahata uwepo wa vikundi na mikakati ya vitisho na ukware wa hoja na matendo kwa wale wanaohoji au kupinga “kazi safi” ya Awamu ya Tano.


HIli limenirudisha miaka yangu ya kupevuka, mwisho wa awamu ya kwanza wakati Malimu Nyerere alipoachia ngazi na kumpisha Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, Mzee Ruksa. Kisha najikuta namtazama Mzee wa Uwazi na Ukweli, Mstaafu Benjamin Mkapa na miaka yake 10 ya utawala.Ukigeuka kwa Mjomba wa Msoga, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, nako kwenye Ari,kasi, nguvu mpya, Maisha bora kwa kila Mtanzania na komeo la Big Result Nowbado kuna ufanano mkubwa wa wapambe na wauza propaganda, dhidi ya wanaohoji na kupinga mambo yaliyofanywa na awamu zote hizi.

Lakini kuna common denominator ya awamu zote hizi nne, unono wa ghafla wa maslahi wa wapambe na watendaji wa karibu wa marais wetu hawa wanne.

Pima sera za “kitaifa” zilizoletwa na Marais wote hawa wanne, mfumo wa propaganda na ulinzi wa hali ya juu wa hoja, mipango, maamuzi n ahata matokeo ya kila kilichowekwa kuwa ni msingi mkuu wa awamu na dira ya Rais. Angalia kwa kina jinsi gani Chama CCM ambapo kwa namna moja au nyingine, kimekuwa mstari wa mbele kunadi kwa Watanzania hizi Sera n ahata ukikitazama Chama, unaona kinaneemeka kwa uharaka sana.

Je propaganda hizi za kuuza seraza Rais ni mfumo mwingine wa kujichumia kwa wale washauri wa karibu wa Marais wetu?

Naangalia enzi za Mzee Mwinyi na wale walionufaika na kutajrika. Mkapa pale alipojiuzia mgodi na mawaziri wake wawili wakubwa wa usimamizi wa uchumi wa nchi walivyopatikana na “hatia” an kufungwa. Hata kwa Kikwete si watendaji pekee, bali wapambe na tuhuma dhidi ya familia.

Sasa hivi, tunaona shaping up ya wapambe ambayo inajijenga kimfumo wa kiutawala kwa kuegemea Ukanda na mamlaka ya kidola huku nchi nzima tukilazimishwa tuamini kuwa tunanyooshwa. Lakini angalia miradi yote mikubwa n ahata matumizi mengine ambayo yamekiuka taratibu.

My point is, kukosekana kwa mfumo imara wa uwajibikaji wa kuleta uwiano wa Check and Balances, na Zaidi kukosekana kabisa kwa udhibiti wa muingiliano wa maslahi- conflict of interest, kunatufanya tuendelee kuimanishwa utendaji kwa manufaa ya Taifa ilhali ni maslahi binafsi yanayojengewa mazingira wezeshi.

Siwatupii lawama za moja kwa moja (direct) marais wetu, ila kutokana na awamu zao kuendeleza mfumo ambao unapinga kwa nguvu zote uwazi, uwajibikaji na utawala bora, tutakapomaliza awamu ya tano, tutajikuta pale pale tukiwa na Masihi mpya wa kuwaaminisha Watanzania kuwa yeye ndio mwenye uchungu wa kweli dhidi ya kero zinazolea umasikini, ujinga na maradhi.
 
Kuna nguvu kubwa sana za muonekano wa kutetea na kulinda maslahi ya Taifa na kusadikika ni kwa manufaa ya Taifa.

Aidha kuna uendelevu mwingine wa ukuaji wa maslahi binafsi wa watendaji na wapambe wa Viongozi wakuu wa nchi.

Natafakari sana jinsi gani Awamu ya Tano inavyojikita katika kutoa sifa na hoja za uwasili na utimilifu wa Safari mpya ya Maendeleo ya Tanzania na nguvu kubwa inayotumika kurembesha na kusifia mipango na “matokeo” ya umakini wa utendaji wa Awamu ya Tano hasa Rais Magufuli n ahata uwepo wa vikundi na mikakati ya vitisho na ukware wa hoja na matendo kwa wale wanaohoji au kupinga “kazi safi” ya Awamu ya Tano.


My point is, kukosekana kwa mfumo imara wa uwajibikaji wa kuleta uwiano wa Check and Balances, na Zaidi kukosekana kabisa kwa udhibiti wa muingiliano wa maslahi- conflict of interest, kunatufanya tuendelee kuimanishwa utendaji kwa manufaa ya Taifa ilhali ni maslahi binafsi yanayojengewa mazingira wezesha.
Mkuu , aya ya kwanza. Nguvu kubwa ya ''kuetetea maslahi ya Taifa'' ina sehemu mbili.

Kwanza, wanaoujua mfumo na udhaifu na kufanya kinachosema 'wanapulizia ubani''.
Waswahili husema mtumikie kafiri upate maradi wako

Kundi la Pili, wanaolinda ugali.Ndilo linashawishi umma kuhusu uzalendo
Kundi hili halina simile, linatumia maguvu ukienda kinyume ni mbaya wao, si mzalendo

Umma wa siku za nyuma si huu. Hiki ni kizazi cha kuhoji, kufikiri na kutathmini kwa mantiki

Uzalendo ni kitu 'intrinsic' yaani natural, haushawishiwi , hauuzwi wala hauna bei.
Kwanini siku hizi kuna ushawishi!

Kukosekana kwa mfumo wa checks and balances ni tatizo, ndio umetufikisha hapa tulipo
Nguvu ya kujitawala haitoki kwa wananchi, inatoka kwa wateule na kwenda kwa wananchi

Neno 'uzalendo' linatumika kama 'silaha' , kinyume, awaye ni mhalifu
 
Rev. Kishoka, kuna neno la Kiswahili linaitwa sarabi linalotumika kuelezea hali ya kusadikika ambayo Watanzania kwa sasa tunapitia. Kama taifa tuko jangwani lakini kwa mbali tunaona sarabi na watawala kiujanjaujanja wanajitahidi kutuaminisha kuwa hiyo sarabi ni halisi na si ndoto.

Wanafanya hivi wakijua wanatudanganya na kwa sababu tuna kiu ni rahisi kudanganyika na kweli wengi wetu wanadanganyika wakiona sarabi inavyovutia. Lakini kwa kuwa si rahisi watu wote kudanganywa wakati wote, nguvu ya ziada ya itikadi inabidi itumike kwa wenye imani thabiti.

Lakini kwa wale ambao wamezinduka na kuanza kuhoji kulikoni kuna njia moja tu ya kuwashughulikia wasilete kash kash nayo ni kuwanyamazisha. Hivyo silaha pekee iliyobaki kwa hawa wanaoitwa wakorofi, wasaliti n.k. ni historia na historia haijawahi kuwaangusha wapenda uhuru na haki.

Kubadilisha mfumo ulioneemesha sehemu ya jamii si kitu rahisi na wengine tulionya na kupigia kelele dhana potofu kwamba kubadilisha mtu pekee yake kutafanikisha mabadiliko. Hapa tena mwamuzi mzuri ni historia; historia inakataa na iko siku somo hili litaeleweka hata kwa wenye mioyo migumu.
 
Mada nzuri sana hii.

Nakubaliana na hoja za waliotangulia. Na hasa hii hoja ya kuwa na checks & balances ni muhimu sana.

Mpaka sasa majukumu ya kuiongoza na kuiletea nchi maendeleo yamekuwa ni ya raisi pekee. Hii ni kwa sababu raisi ana madaraka makubwa sana chini ya katiba yetu ya sasa. Kwa hiyo raisi anakuwa ni defacto dictator hata kama yumo katika mfumo wa kidemokrasia.

Kwa hiyo ni muhimu katiba yetu ikarekebishwa ili iweke institutional structures zitakazohakikisha hizi checks & balances zipo.

Zaidi ya haya pia tunapaswa kuwa na kanuni za leadership (kumbuka Azimio la Arusha?) zitakazowadhibiti viongozi kutoingia vishawishi vya kujitaajirisha at the expense ya wananchi.

Hii nchi kuanzia tupate uhuru imetekwa taratibu (State Capture) sana na wafanya biashara wa nje na wa ndani kwa kutembeza utaajiri wao kuwanunua wanasiasa na viongozi wa ngazi zote za serikali. Kwa kupitia njia hii ya rushwa imefikia mahala kila mtumishi wa umma (kuanzia Raisi mpaka mesenja) alijitahidi kujipatia kipato cha ziada imma kwa kupokea rushwa au kujilipa kwa ziada akitumia mfumo wa serikali (misapropriation of public funds).

Magufuli ameonesha kuwa unaweza kudhibiti vitendo hivi lakini wasiwasi ni kuwa je kuna wengine anaowaonea aibu? Hapa ndipo tunapohitaji hizi institutional structures ambazo zitahakikisha watumishi wa umma wanadhibitiwa regardless ya nani ni Raisi.
 
Majibu yenu yote yananirudisha hapa: Tanzania hatujasheheni na kujenga mfumo imara wa accountability, checks and balances, governance, transparency na independent oversight.

Iwe ni sheria, sera, kanuni, katiba, utendaji, ufuatiliaji, upangaji na utitiri mwinginewe.

Mfano mzuri kabisa ni kikao hiki cha bunge, jinsi mipango na sera inavyokosa upembuzi yakinifu na bajeti kupitishwa kichwakichwa wala si kinyemela tena kwa kuona aibu.
 
Zamani sana hapa JF, nadhani mwaka 2007, tuliwahi kujadiliana kwa kirefu sana kuhusu mfumo wa serikali yetu na mojawapo ya maoni yangu yalikuwa ni kupunguza madaraka ya raisi kusudi asiwe na absolute power. Leo hii hata Jaji Mkuu, Spika wa Bunge, IGP, Mkurugenzi wa TAKUKURU wote wanamwogopa rais kwa sababu ana absolute power ya kuwaondoa madarakani wakati wowote bila kuulizwa na yeyote. Kwa hiyo, mtu ambaye anakuwa karibu na rais anakuwa untouchable!!
 
Zamani sana hapa JF, nadhani mwaka 2007, tuliwahi kujadiliana kwa kirefu sana kuhusu mfumo wa serikali yetu na mojawapo ya maoni yangu yalikuwa ni kupunguza madaraka ya raisi kusudi asiwe na absolute power. Leo hii hata Jaji Mkuu, Spika wa Bunge, IGP, Mkurugenzi wa TAKUKURU wote wanamwogopa rais kwa sababu ana absolute power ya kuwaondoa madarakani wakati wowote bila kuulizwa na yeyote. Kwa hiyo, mtu ambaye anakuwa karibu na rais anakuwa untouchable!!
Mkuu miaka mingi suala hili linajirudia na tunatoa maoni sana.

Ukitazama rasimu ya Warioba, ilijaribu kutoa majibu kwa kupunguza madaraka ya Rais

Wengi wanadhani kumpunguzi Rais madaraka ni kumnyima nguvu.
Ironically, ni kumpa uwezo wa kufuatilia kwa ukaribu.

Tazama suala la madini, laiti Rais asingekuwa na absolute power lingeweza kuzuiliwa mapema sana.

Pamoja na hayo, ''kutajwa tajwa'' kwao ni kwasababu ya absoluet power waliokuwa nayo
Hivyo walihitaji checks and balances

Hilo wanalitambua, hawalitaki, kulikubali ni kuziba njia za kuendelea kutawala

Ndio maana walipinga rasimu, kisha wakatangaza hiyo si agenda ya CCM, mwisho na kifo

Hii absolute power inawanyima watendaji nafasi.

Kwa mfano uliotoa, CJ, Spika, IGP, DCI, DPP, Dir PCCB wote wanategemea fadhila za uteuzi na kuendelea madarakani kwa kuwa 'loyal'

Kila wanalofanya ni woga umewajaa, hawana nafasi ya kutenda tofauti

Hili limetenegeneza tabaka untouchable. Sakata la yule RC wahusika wanapita pembeni!!!!
Nani atakayemgusa bila kugusa kitumbua chake.
 
Back
Top Bottom