Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Mkuu bila shaka ulisoma Law of Tort, na unakumbuka hii principle "Res ipsa loquitur". Kwa kupitia utawala wa sheria na democrasia, wananchi wamesha-surrender powers zao kwa hao wanaoitwa madikteta. Ni wajibu wa hao "madikteta" kukanusha kwa niaba ya wananchi-watanzania kuwa wao siyo ma-Dictators...na huo ndo Uzalendo. Bila shaka wasingekuwa "madikteta" wangelisha-kanusha zamani sana.

Mkuu, kama hutojali jaribu kupitia comment yangu ile ya hivi karibuni..
@Pascal Mayalla
 
Sijaisoma yote hii habari lakini,najibu kutokana na kichwa cha habari kinavyoleza.,
ningeenda kukujibu kuwa uzalendo unakuja kutokana na raia kuona anapendwa na nchi yake..

Raia anapoona nchi yake inamlinda na mkumpenda,raia anakuwa anajivunia nchi yake,majivuno ya nchi yako ndio uzalendo wa nchi yako...

Serikali ya Tanzania,raia wake ndio maadui zake,...sifikirii kama kutakuwa na mtanzania atakae kuwa na majivuno na Tanzania...Uzalendo haupo Tanzania,period
 
Pascal Mayalla uzalendo wa WaTz upo mioyoni mwao lakini ipo siku ya moyoni yatageuka vitendo.
Kwani wewe ulikuwa unashauri tufanye nini!
Kuna moshi unafuka mahala mahala ujue kuna moto utakaounguza msitu
Nikushauri ongeeni na huyo anaitwa dikteta anatukanwa ajirekebishe
Mwambieni Tz ni yetu sote sio ya chama kimoja
Aache vitisho bali awe mnyenyekevu na msikivu
Amtoe mvuruga amani bashite
Asikilize vilio vya wananchi
Arudishe amani yetu upendo wetu na usalama wetu
Hatatukanwa vinginevyo ataendelea kutengwa
 
Wanabodi,

Makala za Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla.
Naendelea na Makala zangu ziitwazo Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la kila siku za Jumatatu. Hizi Makala zitafuatiwa na Kipindi cha TV chenye jina hilo hilo ambacho kitaanza kutoka kwenye vituo kadhaa vya TV hivi karibuni baada ya taratibu za udhamini kukamilika, vikiangazia hoja mbalimbali muhimu kwa maslahi ya taifa letu la Tanzania.

Hoja ya Udikiteta Tanzania.
Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikijadili hoja ya Udikiteta Tanzania. mada ya leo ni kuhusu uzalendo wa ajabu wa Watanzania kuunyamazia uongo unaoenezwa kimataifa kuhusu huu udikiteta Tanzania. Jee Sisi Watanzania, Tuna Uzalendo Gani Kunyamazia Huu Uongo Unaonezwa Kimataifa Kuwa Rais wa Tanzania ni Dikiteta na Tunatawaliwa Kidikiteta?. Au Kwa Kunyamaza Huku Ndio Kukubali Kwenyewe Kuwa ni Kweli Taifa Letu Tanzania Tuko Kwenye Udikiteta?.

Angalizo Kuhusu Uzalendo.
Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, na sisi wananchi wote, haijalishi umri, rais ni kama baba yetu, sisi ni kama watoto, hata kama kuna waliomzidi umri. Inapotokea baba anakosea, mfano baba ni mlevi, na akilewa huwa anampiga mama huku sisi Watoto tunaona, tunaweza kumzuia, kumkosoa na hata kumtukana, baba acha ulevi, na isiwe a big deal!, lakini inapofikia baba yako ananyooshewa vidole na majirani au mitaani kuwa Fulani ni mlevi, au watu baki wanamtukana baba yako, huwezi kufurahi wala kushangilia!, haiwezekani kuona baba yako anatukanwa na wewe ukakaa kimya, vivyo hivyo kwa rais Magufuli, pamoja na madhaifu yake yote ya kibinaadamu, Watanzania wazalendo, hawawezi kuona rais wao akitukanwa na kusingiziwa uongo, huku tumekaa kimya. Ukiona rais wako anatukanwa na kudhalilishwa kwa vitu vingine vya uongo na uzushi na wewe ukawa unajua ni uongo, lakini bado ukakubali na kukaa kimya au hata kushangilia, ujijue una matatizo!, ukimuimagine rais Magufuli kama ni baba yako, hutakubali atukanwe, adhalilishwe, na asingiziwe uongo, ila kama yote yanayosemwa ni ni kweli, then, its ok japo hupendi, lakini hakuna jinsi, acha tuu aambiwe, hata kama ukweli huo ni mchungu vipi, au unauma vipi!, itakubidi tuu ukae kimya na kunyong'onyea.

Uzalendo wa Tanzania ni Uzalendo Gani?
Leo tuuzungumzie uzalendo wa Watanzania, ni uzalendo wa aina gani ambapo Taifa lako linatukanwa kuwa linatawaliwa kidikiteta, umenyamaza, rais wako anatukanwa kuwa ni dikiteta, umenyamaza, jee haya yote yanayosemwa kuhusu Tanzania ni kweli?, kama swii kweli, kwa nini hakuna yoyote anayejitokeza kuukanusha uongo huu?. Huu uzalendo wa Watanzani tunaojivunia, ni uzalendo gani huu ambapo uongo, ukisemwa sana kuhusu taifa letu na rais wetu kuwa ni dikiteta, na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wa siku, sio tuu uongo huo utaonekana kama ni ukweli, bali unaweza kabisa kubadilika na kugeuka kuwa ni ukweli kwa sababu kauli huumba!.

Mazuri Anayoyafanya Rais Magufuli ni Udikiteta?.
Baada ya rais Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kushinda uchaguzi huru na wa haki, na kutangaza rasmi kuwa uchaguzi umekwisha, sasa ni wakati wa kupiga kazi ya ujenzi wa taifa kwa falsafa ya “Hapa Kazi Tuu” kuanza kuhimiza maendeleo ya taifa badala ya kukalia siasa, kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya kitaifa, na kubakiza ile ya majimbo tuu, na pia kuanza kazi ya kulinyoosha taifa hili katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa kutumia tumbua tumbua, na amsha amsha ya ziara za kushutukiza na kuviamsha vyombo vya dola kutimiza wajibu wake kikamilifu, ndipo kelele za udikiteta zilipoibuka.
Kwa Nini Wapinga Udikiteta Kila Siku Hupinga Kwa Hoja Kwa Kusemasema Tuu na Kutaka Kufanya Mikutano na Maandamano Badala ya Kuchukua Hatua Stahiki?.
Kwa nini Wapinga udikiteta kila siku huupinga huu udikiteta kwa kauli tuu na kutaka kufanya mikutano na maandamano? badala ya kuchukua hatua stahiki?. Hili nimewahi kulizungumza humu, kuwa kama Tanzania Tanzania kuna udikiteta, hao wapinga udikiteta kwa nini hawachukui hatua stahiki za kuupinga huu udikiteta?.
Udikiteta Tanzania: Je, Rais Magufuli kweli ni dikiteta au wanamsingizia tu? Msikie Mwalimu Nyerere kuhusu udikiteta!
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".
https://www.jamiiforums.com/threads...ata-atakayeleta-fyoko-ataisoma-namba.1009702/
Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!

Wanaolalamikiwa Kwa Hoja za Udikiteta, Kwa Nini Hawajibu Hoja na Kushia Kupiga Tuu Marufuku Maandamano na Kuzuia Mikutano?.
Kila yanapotangazwa maandamano au mikutano ya kupinga udikiteta, siku zote kwenye kauli zao, huweka hoja maridhawa kuhusu udikiteta na kwa nini wanataka kuandamana, Kwa nini siku zote, wajibu hoja ambao ni serikali, hakuna hata mara moja huzijibu hoja kuhusu udikiteta, wao kazi yao ni kutumia tuu nguvu kubwa kuzuia mikutano na kupinga maandamano, lakini hakuna juhudi zozote kujibu hoja kuhusu huo udikiteta, matokeo yake, siku zote hufanikiwa kuzuia mikutano maandamano, lakini hoja za maandamano hayo kuhusu udikiteta huwa hazijibiwi na hubaki pale pale. Hii maana yake ni nini?. Mtu anaposema nitaandamana kwa sababu rais Magufuli ni Dikiteta amefanya hili na hili na hili, wewe serikali unasema hakuna kuandamana, atakaeandamana atakiona na vitisho vingi, lakini hujibu hoja yoyote ya sababu za maandamano, hii maana yake ni nini?.

Jee Maadamano ya Tarehe 26/4/2018 Yapo au Ni Maandamano Hewa?. Hoja za Maandamano Hayo nazo ni Hoja Hewa?.
Nawaomba sana mnisamehe kuyaita haya maandamano ya tarehe 26/04/2018 yanayopigiwa upatu kwenye mitandao ya kijamii, kuwa ni maandamano hewa!.
Watu wote wenye akili timamu, wanajua kabisa kuwa kiukweli tarehe 26/04/2018, hakuna maandamano yoyote ya kweli ndani ya JMT na mahali pengine popote, hivyo hakuna sababu kabisa za serikali yetu kutishika hadi viongozi wetu hadi wakuu kuweweseka na maandamano hewa hadi kutoa kauli za vitisho kuyapinga maandamano hayo, badala yake wajikite kutoa majibu ya hoja za maandamano hayo.

Serikali, Viongozi Msijikite Sana Kupinga Maandamano, Jibuni Hoja Za Maandamano Husika!.
Natoa wito kwa serikali yetu, viongozi wetu, wasijikite sana kuyapinga tuu maandamano hewa, bali walizijibu hoja kuhusu sababu za maandamano hayo, kwa sababu ni hizo hoja ndizo zinatumiwa kulichafua taifa letu na kumchafua rais wetu.

Kama ni hoja kuhusu udikiteta na yanayosemwa ni uongo kuwa Tanzania hakuna udikiteta, wahusika wajitokeze hadharani kuzipinga hoja hizo za uongo kwa hoja mbadala za ukweli. Ndio maana nikasema namtafuta waziri wetu wa sheria, Prof. Kabudi kujibu hoja.

Jee Tabia ya Kudharau Kujibu Hoja za Udikiteta, Ni Kwa Sababu Zinatolewa na Wapinzani na Media Uchwara?
Kuna hii tabia ya viongozi wa serikali kudharau kujibu hoja zozote zinazotolewa kuhusu huu udikiteta, kwa kuzihesabu ni hoja za uongo, labda kwa vile wapiga kelele wakuu kuhusu huu udikiteta ni wapinzani, wenye majibu ya ukweli kuhusu uongo huu wa udikiteta, ni waserikali, na majibu ya kweli wanayo, lakini wameamua kukaa nayo kimya kwa kutokusema chochote, na badala yake ni kuwapuuza tuu watoa hoja ambao very unfortunately sio wote ni wapinzani. Wapuuza hao, wanapuuza hizi kele za udikiteta kwa hoja ni kelele tuu za chura kisimani, ni kelele za mlango, au ni kelele za wapangaji, haziwezi kumkosesha mwenye nyumba usingizi, hivyo kujiona wako very right kuzipuuzia kelele hizi.

Huwezi Kupuuza Uongo Unaosemwa na BBC, DW Radio, VOA, SABC, The Economist na Vyombo vya Habari vya Kimataifa.
Lakini kelele hizi zinapofikia hatua ya kuungwa mkono na vyombo vya habari vya kimataifa, BBC, DW, SABC, Jarida la The Economist, etc, kama ni uongo, sii za kupuuziwa hata kidogo. Redio mestini (redio za jeshini JKT), redio mbao (uvumi wa mitaani) zikitunga uongo na kueneza uongo kuhusu udikiteta, unaweza kuzipuuzia, kwani zinasikilizwa na nani?, lakini inapofikia BBC, DW Radio, VOA, SABC wakaudaka uongo huu na kuuvumisha, hili sii jambo la kupuuzia hata kidogo!.

Au Gazeti za Tanzania Daima, Raia Mwema, au gazeti lolote la Tanzania, likisema rais Magufuli ni dikiteta kwa kumnukuu Mbowe au Lissu, mnaweza kupuuza, kwani magazeti haya yanasomwa na nani?, si ni magazeti ya kufungia tuu samaki, maandazi na chapati, lakini udikiteta unaposemwa na majarida ya kimataifa, The Economist, The Financial Times, The Newsweek, etc, hivi sio vyombo vya kupuuzwa hata kidogo!. Unaweza kulipuuza Tanzania Daima na Raia Mwema, lakini huwezi kulipuuza The Financial Times na The Economist!.

Jarida la Economist Lilianza Zamani na Nilieleza Humu.
‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
nilisema baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni. Tulikaa kimya bila yoyote kukanusha popote!.

Kuhusu Udikiteta Tanzania, SABC Wakafuatia
Mimi kama mwandishi, kazi yangu ni kusema na kuandika tuu. Baada ya Taarifa hiyo ya SABC nilisema kitu humu Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta!
Nikasisitiza Uzalendo wa kweli ni kutokubali na kutonyamaza kimya wakati rais wako anaposemwa vibaya kwa hoja za uongo na media za nchi nyingine, bali ni kwa viongozi wetu kujitokeza kwenye media zetu kuukanusha huo uongo kuhusu udikiteta kwa kuusema ukweli na ikibidi serikali yetu sio tuu ikanushe bali pia ihitaji kuombwa radhi na ikibidi hata tudai fidia!. Hata Kikwete aliposingiziwa kuhongwa suti na Marekani, nilitoa hoja hii Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!, na Ikulu yetu iliingilia kati.

Jee Rais Magufuli ni Malaika Mtakatifu, Yuko Perfect. Hakosei?
Pamoja na matatizo yake yote na mapungufu ya kibiinadamu ya rais wetu Magufuli, kwa sababu na yeye ni binadamu kama sisi na sio malaika, hivyo anaweza kukosea. Pale rais wetu anapokosea na kusemwa vibaya kwa ukweli kuhusu makosa yake, itabidi tukubali tuu na tuwe wadogo tuu. lakini Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi yetu, kamwe tusikubali rais wetu kudhalilishwa kwa kusemwa vibaya, kwa kusingiziwa vitu vya uongo na media za nje bila ya media za ndani na viongozi wetu, kukanusha na kumtetea, au kuunyamazia udhalilishaji kama huu ni sawa na kushangilia rais wetu kudhalilishwa. kitendo cha kuuacha uongo kama huu kuendelea, ndiko kunakopelekea uongo huu sasa kuanza kugeuka kama ukweli, na mwisho wa siku kugeuka ukweli.

Jarida la Africa Confidential Likaita Serikali yetu "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Jarida la Africa Confidential toleo la 58, story number 20 lililochapishwa Oktoba 6, 2017,
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Haya sio maneno mazuri kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ushindi halali katika sanduku la kura, kupitia uchaguzi ulioendeshwa na "Tume huru ya Uchaguzi", hivyo uchaguzi ulikuwa ni "huru na wa haki", hivyo matokeo ni halali, na nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata misingi ya katiba, na kuheshimu utawala wa sheria.

Kwa Nini Serikali Inakemea Uongo wa Media za Ndani na Kufungia lakini Media za Nje iko Bubu?.
Ikulu yetu, Waziri Mwakyembe na Idara yetu ya Habari, tusikalie kuyafungia tuu magazeti ya ndani kwa kutoa habari za uongo, au nyingine ni za kweli msiopendezwa nazo, huku tukikaa kimya wakati habari za uongo kuhusu nchi yetu zikienezwa na media za nje!, zinazowafikia mamilioni?. Habari yoyote ambayo sii ya kweli, kuihusu Tanzania na rais wetu, ikitolewa media yoyote, tusikae kimya, ikanushwe!, vinginevyo itaonekana ni kweli!.

Jarida la Economist Laishukia Tena Tanzania!, Laitukana Nchi Yetu, Lamtukana Rais Wetu.
Ni muda sasa jarida la The Economist limekuwa likiisema vibaya nchi yetu, na kumsema vibaya rais wetu, ikiwemo kumuita majina ya ajabu ajabu, mimi nikiwa ni mwandishi wa habari, kanuni kuu nambari moja kwa mwandishi wa habari, ni kusema ukweli daima, hivyo sina tatizo kabisa na chochote kitakachoandikwa kwenye gazeti, kuihusu nchi yetu Tanzania, au rais wetu Magufuli, kama kitu hicho ni cha kweli, lakini natatizwa sana na uongo wowote unaoandikwa kwenye magazeti na majarida ya kimataifa, likiwemo jarida hili la The Economist, kwa lengo la kuhadaa ulimwengu kwa kutoa story za uongo kuhusu Tanzania na rais wetu, na kuzieneza kimataifa zisambae dunia mzima, wanaoujua ukweli kuhusu haya yanayosemwa ni sisi Watanzania, nchi yetu inatungiwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anatungiwa na kusingiziwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anapachikwa majina ya ajabu ajabu, dikiteta, dinasauria wa Dodoma, na sasa ameitwa rogue, tumenyamaza!, rais anadhalilishwa na kutukanwa huku sisi tumenyamaza!, huu ni uzalendo gani?!.

Kuna wanaoamini kila kinachosemwa na media za nje kuhusu Tanzania ni kweli, na kila kinachosemwa kumhusu rais Magufuli ni kweli, huo ni mtazamo wao kutegemea na uwezo wa uoni wa jicho lao, linaona vipi, kuna kitu mmoja anaweza kukiona ni sawa, na mwingine akakiona sii sawa, mimi kwa upande wangu, naona sii sawa kwa nchi yetu kusemwa vibaya na rais wetu kuzushiwa uongo na kusingiziwa uongo.

Kwa vile uongo huu unasambazwa kimataifa na huku sisi Watanzania wenyewe tumenyamaza bila kuukanusha, matokeo yake sio tuu, jamii ya kimataifa, utauamini uongo huo, bali hivyo ndivyo itakavyo tuelewa na hivyo ndivyo itakavyo muelewa rais wetu, bali uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, uongo huo hugeuka kuwa ukweli!. Hii tabia ya kusikia uongo na kuunyamazia, kunaweza kabisa kupelekea haya ya uongo yanayosemwa sasa, kuja kuwa ya ni ya ukweli na yatakuja kutokea Tanzania kwa siku za usoni!, ni mpaka pale yatakapokuja kutokea, ndipo watu watalia na kusaga meno!, tena wakati huo ukifiki, it might be too little too late.

The Economist walianzia hapa ‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
Tukanyamaza, sasa wameibuka tena na uongo mwingine
Tanzania's rogue president - Democracy under assault - The Economist

Katika report hiyo, wamemtukana rais wetu kuwa Rogue President. Kwa vile mimi sijui Kiingereza, ilinibidi nikatafute kwanza kamusi kuangalia neno rogue maana yake ni nini, mtu anaeitwa rogue ni mtu wa namna gani, na taifa likiitwa rogue state ni taifa la namna gani, naomba kwa heshima ya rais wetu, nisitoe tafsiri ya neno hilo, ila kwa kifupi ni kuwa, rais wetu ametukanwa!.

Kwenye report yao, japo kuna mambo machache ya kweli kuhusu Tanzania, lakini pia wamechomekea mambo mengine mengi ya uongo kumhusu rais wetu na hoja za udikiteta ambazo inabidi zikanushwe.

Hii ni Makala toka jarida la The Economist, linamsakama sana Rais Magufuli, katika Makala hii, linahamasisha rais Magufuli adhibitiwe kwa kuwekewa vikwazo vikali kabisa kiuchumi.
How to save Tanzania
hawa watu wanamuita rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kuwa ni an authoritarian and erratic president who is transforming a stable, if flawed, democracy into a brutal dictatorship.

Ni haki kweli kumuita rais wetu, an authoritarian na erratic president na kumtuhumu kuwa ana transforming a stable, democracy into a brutal dictatorship?. Kuna ukweli wowote hapa?. Hawa watu hivi ndivyo walivyoiambia dunia kuhusu Tanzania, kweli hivi ni vitu vya kunyamazia?.

Wakati haya yakisemwa, wiki hii hii, ndio hii wiki, waziri wetu wa habari, na naibu wake wako busy kumshupalia Diamond, mwanamuzi kijana mdogo anayejituma, hadi kufikia kiwango cha naibu waziri kufanya mahojiona ya kujidhalilisha, na Diamond akajibu mapigo kwa kumdhalilisha zaidi!.

Waziri Prof. Mwakiembe, Naibu, na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Dr. Abasi, fanyeni press conference mjibu hoja serious kama hizi zinazohusisha reputation ya taifa letu kimataifa na sio kujikita kwenye trivia issues za sanaa, mambo ya sanaa, waachieni Basata, nyinyi mjikite kwenye serious policy issues, inchi yetu inadhalilishwa kwa hoja za uongo kuhusu udikiteta, nyinyi mnadiscuss nyimbo za Bongo Flava, sijui wamevaaje etc, this is nonsense!.

Jee Tukidai Fidia Tutashinda Tutalipwa?
Kama tuhuma hizi ni kweli, tuendelee kukaa kimya, lakini kama ni uongo, tukanushe na tukidai fidia, tutalipwa!. Kuna wakati aliyekuwa rais wa Zanzibar, enzi hizo Komandoo Dr. Salmin Amour alisemwa vibaya na BBC Swahili, hakukubali aliwashitaki, alishinda na alilipwa fidia, kama hizi media za nje, zinasema uongo kuhusu udikiteta Tanzania, kwanza tukanushe, tudai kuombwa radhi, na ikibidi, tuwashitaki, tulipwe fidia.

Mhe. Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe, usinyamaze kimya wakati rais wetu akidhalilishwa na media za nje. Pia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, na Idara ya Habari Maelezo msinyamaze kimya, jibuni mapigo kwa kuusema ukweli kuihusu nchi yetu na kumhusu rais wetu hawezi kudhalilishwa kuhusu udikiteta, huku nyinyi mpo mmenyamaza.

Wenye Uhalali Kumsema Vyovyote Rais Wetu ni Sisi Watanzania As Long As Kinachosemwa ni Kweli!.
Watu pekee wenye uhalali wa kumsema vibaya rais Magufuli ni sisi Watanzania wenyewe ambao ndio tulimchagua rais Magufuli kuwa rais wetu. Ilitokea sisi haturidhishwi na utendaji wake, sisi Watanzania ndio wenye haki hiyo ya kumsema vibaya au vyovyote kwa sababu sisi ndio waajiri wake!, na media zenye haki hiyo ni media zetu Tanzania na sio media za jirani au media za nje.

Kama sisi wenyewe tunampenda rais wetu na kumkubali sana, kwa nini tusiwatimue nchini kote raia wote wa kigeni walio nchini ambao wanamsema vibaya rais wetu?.

Haki ya Kukosoa na Kumsema Vibaya Rais wa Nchi. Ina Mipaka!.
Wenye haki ya kumsema vibaya Trump kwenye media ni Wamarekani wenyewe, vivyo hivyo wenye haki ya kumsema vibaya rais wetu Magufuli kwenye media ni sisi Watanzania wenyewe!.

Kama ilivyo ngazi ya familia, unaweza kukaa jirani na wife battering neighbours na kila siku unasikia vilio vya mke wa jirani akichezea kichapo na asubuhi unamuona na manundu, hata kama huyo mke anayechezea kisago hajalalamika kwako, wewe kama jirani huna ruhusa ya kumtangazia vibaya jirani yako huyo kuwa ni mbaya humpiga mke!.

Kwa vile Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayoongozwa na katiba yanye kuheshimu haki na utawala wa sheria, taratibu na kanuni, kila kinachofanywa na rais wetu ni kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na hata rais wetu yuko chini ya katiba na anapaswa kufanya kila kitu kwa mujibu wa katiba kwa kufuata sheria taratibu na kanuni na ikitokea rais akafanya kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni, pia ziko sheria taratibu na kanuni za kumshughulikia rais anapokwenda kinyume cha katiba au sheria.

Kama ni Kweli Tanzania Tuna Udikiteta na Sisi Wenyewe Tumeukubali, Kwa Nini Watuingilie?.
Kama ni kweli rais wetu Magufuli anatenda kinyume cha katiba na sheria, na taratibu za kumshughulikia zipo lakini sisi Watanzania wenyewe tumeridhika naye na utendaji wake huo huo, hivyo hivyo anavyotenda iwe kwa kuvunja katiba au kinyume cha sheria, Watanzania wenyewe tumeridhika na kukubali, who the hell is jirani yasiyomhusu, anayekuja kutusemea kwenye media yao kuwa rais wetu amekosea?. Kama wenyewe tumekubali na tumeridhika, huyu jirani anamsemea nani?!. Kwa nini Watanzania tunanyamasia uongo huu?.

Wiki ijayo, nitakuja na set ya maswali kuhusu hoja za udikiteta ambayo nitayaelekeza kwa Waziri wa Sheria na Katiba. Prof. Palamagamba Kabudi.

Jumamosi Njema.

Paskali

Hebu tupe tafsiri ya neno tusi kwanza. Kwa kiwahili sio kisukuma.
 
Ndio ujuwe kuwa tumefika kubaya inamaana kwa upeo rahisi wakiusalama yani watanzania wapo tayari kuuza nchi yao ili rais wao auwawe. Kiukweli kabisa tuna hali mbaya sana kama taif nakama tusipo kitokomeza kizazi hiki cha wasio wazalendo usalama wetu upo ktk hatari. Mtu amekuwa na nafasi kubwa ya kitaifa anavujisha siri za taifa kwa kisingizio cha upinzani bado yupo mjini anavuta hewa nakupata kahawa hapana we need to act now. Inatisha ndugu zangu
Mmeona anayofanya yote yako sahihi? Mbona sijaona yeyote toka chama chake akikemea ukiukwaji mkubwa Wa katiba unaofanywa na huyu mtukufu mtakatifu mnayetaka kutuaminisha hakosei? Kiongozi Wa nchi kuigeuza nchi kama familia yako utaambulia mashambulizi tu. Kama yeye anafurahia maumivu kwa wenzake ni halali wenzake kufurahia maumivu yake pia.
 
Comment yako hii imenivuta kuchangia huu mjadala, hebu iweke vizuri na kwa uwazi tuweze kupambanua
Mimi sina tatizo na member kama wewe kwakuwa unajulikana wazi umesimama upande gani.... Lakini Paskali huwa anakuwa haeleweki kabisa... Na hili si jambo jema
Mbona Pascal anaeleweka sana au siku literature haisomwi. Refer kitabu kama animal farm au kusadikika
 
Watawala wanatuchukulia sie ni Wanyonge hivyo kutunyonga kwao wanalichukulia poa sana... ila wajue Bubu hutaka kusema mambo yanapomzidia....
 
Mbona sisi tunatukanwa kwakuitwa vilaza
Pointi ya Paskali ni kwamba muwe wavumilivu, sio tu umeambiwa ukatandike bango kwenye kitanda cha mke wako nawe unanyanyua kifua unataka kujibu.

Maadili yetu hayaruhusu kujibizana na Wakubwa.
 
Dk Abbas anapwaya sana pale habari maelezo
Ukizungumzia Mwakyembe na Shonza hawajui hata kazi yao pale wizarani wanadeal na petty issues ambazo hazina tija yoyote kwa nchi isipokuwa vinawapa media coverage tu.
Kuhusu vyombo vyetu vya habari tangu lini vikadeal na maswala nyeti kama tofauti na kupiga mbinje za kitoto tu ?
At least we have a platform to speak out JamiiForum tupaze sauti zetu pale nchi yetu inapodhalilishwa na vyombo vya habari vya nje.
Lakini na serikali ipunguze kufanya mambo yanayoidhalilisha.
 
Uzalendo ni dhana pana, nafkiri inaweza ikaamuliwa maana yake kulingana na sehemu, falsafa ya nchi n.k.
Kwangu mimi ni muumini wa State, My Faith and My Family hivi vitu vitatu come first to my priorities. Nikihisi mtu anahatarisha their survivor then come what may.
Lakini kuna mambo ya state wakati mwingine yanakupa ukakasi ktk morali haahasa yanapokuwa yanafanywa unpatriotically na mengine hayakanushwi kwa hoja stahiki.
 
Pascal unajidhalilisha sana. Labda kuwa verified kunakunyima kuwa huru. Epuka kufurahisha watu.
Ukifanya vyema unapongezwa. Ukivurunda unakosolewa na kusahihishwa. Wako watu kwa ajili ya kumtetea Rais. JF si watetezi wa Rais. Tunatetea maslahi ya nchi. Rais si nchi.
 
Back
Top Bottom