Uzalendo unahitajika kulinda maliasili za Taifa


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225
[h=2]15 NOVEMBER 2012[/h]
Na Agnes mwaijega

UTEKELEZAJI wa sera zinazotungwa katika nchi yoyote ulimwenguni yanategemea usimamizi wa serikali unaozingatia sera na sheria.


Ni wazi kwamba kama serikali haizingatii sera na sheria katika utekelezaji wa majukumu yake ni wazi kwamba mafanikio hayawezi kapatikana.


Yapo masuala mbalimbali ambayo yameshindwa kuleta manufaa kwa taifa na wananchi kwa ujumla kutokana sera na sheria zilizowekwa kutozingatiwa.


Suala la ugawaji ovyo wa ardhi kwa wageni au kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ni miongoni mwa masuala ambayo ni matokeo ya sera na sheria zilizowekwa kusimamia ardhi kupuuzwa.


Suala hili limekuwa likizua mijadala mizito mara kwa mara kutokana na ukweli kwamba ardhi ni rasilimali muhimu.


Suala hilo pia limekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi ambayo imekithiri katika maeneo mengi nchini kutokana na wananchi kutokubaliana nalo.


Kwa upande mwingine limewafanya watanzania wengi kutokuwa na imani na viongozi wa serikali kwa sababu wameshindwa kujali maslahi ya nchi na kulinda rasilimali za taifa.


Suala hili halijaanza kupigiwa kelele leo na wananchi wameendelea kutaabika na kuhamishwa katika maeneo yao bila kutaka.


Hata hivyo wenye uchungu na suala hilo ni wachache ndiyo maana hata utekelezaji wake ni mdogo kwa sababu katika hili umoja na nguvu ya pamoja inatajika.


Kwa mfano imekuwa ni jambo la kawaida kwa wakulima kuondolewa maeneo yao ili kuwapisha wawekezaji wa madini na nje ya nchi ili waweze kuendesha shughuli zao ambazo hazina manufaa kwa wananchi hao.


Kutokana na hilo hali ya umaskini imezidi kuongezeka badala ya kupungua kwa sababu maeneo mengi yaliyochukuliwa na wageni hao hayaendelezwi na hayatumiki kwa manufaa ya wananchi.


Pamoja na hilo inaeleweka wazi kwamba ugawaji wa ardhi kwa wageni siyo uzalendo na inazidi kudumaza maisha ya watanzania na kudidimiza uchumi wa nchi.


Suala hilo limeibuka tena katika kikao cha bunge ambapo Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee aliwasilisha hoja binafsi ya kutaka mchakato wa ugawaji wa ardhi usitishwe ili tathimini ya kina ifanyike kujua kiasi cha ardhi ambayo iko mikononi mwa wawekezaji.


Namuunga mkono Mdee na kupongeza kwa kuliibua tena suala hilo ambalo kwa kweli kila kiongozi anapaswa kulichukulia uzito na kuona kwamba linatakiwa kuafanyiwa kazi haraka.


Mdee alijitahidi kutoa orodha ya maeneo ambayo yamechukuliwa na wageni na ambapo mengine yako katika hali mbaya kwa sababu yameachwa bila kuendelezwa.


Unajua ni jambo la kusikitisha kwamba inafikia hatua uagawaji wa ardhi unakuwa wa ovyo kiasi kwamba hata kiasi cha ardhi walichopewa wawekezaji kinakuwa hakijulikani.


Hii inaonesha jinsi viongozi wetu wanavyojali maslahi ya wawekezaji, wasivyo na uzalendo na uchungu na mali za nchi na kuthamini uwekezaji usio na tija.


Suala aliloliwasilisha mbunge huyo mbele ya wabunge hao ni la muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.


Kama litaoonekana kwamba halina maana kwa sasa ni wazi kuwa taifa la kesho litaishi katika mazingira magumu na uchumi kuendelea kudidimia.


Lazima suala hilo litazamwe kwa umakini mkubwa na ifike mahali viongozi wa serikali waone uchungu na mali za nchi ambazo zimepotea bure na kuliacha taifa likiendelea kuwa maskini.


Tanzania ni nchi huru kwa hiyo ni wazi kwamba hata mali zetu zinapaswa kulindwa na kusimamiwa na kuwanufaisha kwanza watanzania wenyewe.


Ili hilo liweze kuwa na mafanikio uzalendo kwanza ndiyo unaohitajika, kwa sababu bila hivyo itakuwa sawa na kutwanga maji kwenye kinu.


Tunaomba kila aliyepewa dhamana na mamlaka ya kusimamia masuala ya ardhi aone umuhimu wa kuweka maslahi ya taifa mbele ili ugawaji ovyo wa ardhi na migogoro hiyo iweze kumalizika nchini.


0717157514 

Forum statistics

Threads 1,294,741
Members 498,025
Posts 31,186,757
Top