Uzalendo, ujasiri ngao zetu, tumeshinda beberu na tutashinda zaidi. Mahakama Zimeamua

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
Uzalendo kwa maana ya kulipenda na kujitoa kulitumikia na kulitetea taifa katika hali zote na kwa moyo wote, na ujasiri kwa maana ya kuwa tayari kukabiliana na nguvu iwayo yote kutoka kwa yeyote, ukitumia akili ujuzi na maarifa, ili kushinda ndiyo silaha na ngao yetu kama taifa katika kulinda na kutetea maslahi ya mama Tanzania.

Taifa linaweza kuwa na kila kitu, rasilimali, watu wenye akili na uwezo mkubwa, ujuzi na maarifa ya sayansi na teknolojia, na kila kitu ambacho taifa linahitaji kuweza kushindana na kushinda hila za adui zake wa wazi na walio sirini, lakini kama halitakuwa na raia wenye moyo wa uzalendo na wako tayari kujitoa kwa ajili ya taifa lao ni kazi bure.

Ni kama tu ilivyo Amri Kuu ya Upendo, Bwana Yesu aliwambia wafuasi wake, ijapokuwa mtu ana imani kubwa na thabiti kiasi cha kuhamisha milima kama hana upendo ni kazi bure, kwamba katika upendo ndimo kulimo chemichemi za neema na heri zote za Mwenyezi.

Amri zote na makatazo yote ya imani zote za dini, msingi wake mkuu ni upendo, kumpenda Mungu kwa akili yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa kila kitu chako chote, na pia kumpenda jirani kama unavyojipenda mwenyewe, kishayatimiza haya huwezi kuiba, kuua, kuzini, kumsengenya mwenzako, kusema uongo na uovu mwingine wowote ule, kwa kuwa msingi mkuu wa dhambi zote ni kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu au kumtendea binadamu mwenzako ndivyo sivyo. Ukiwa na upendo wa dhati kwa Mungu na kwa jirani, unaanzaje kuwatendea ndivyo sivyo?

Kadhalika, uzalendo, mapenzi ya dhati kwa nchi na taifa lako bila kujali hali iwayo yote. Ndiyo maana ilikuwa inastaajabisha sana kuona baadhi ya Watanzania wenzetu walikuwa wanafurahia kusikia ndege zetu zimekamatwa nje ya nchi kwa sababu ya ‘madeni’ ambayo tulikuwa tunaidaiwa kama taifa ama kwa haki au wakati mwingine kutokana na mipango iliyosukwa vyema na wahalifu wa kimataifa na taifa linajikuta katika madeni ambayo hayana uhalali wowote.

Tumekuwa na kesi kadhaa nje ya nchi ambazo kwa namna ya ajabu zimekuwa zikishabikiwa na baadhi ya wananci wenzetu waliotindikiwa mapenzi kwa taifa lao au kutokana na ujira wanaolipwa na wanaotaka kutuhujumu katika juhudi zetu za kupiga hatua kiuchumi na kujipambanua katika nafasi yetu kwenye uchumi wa dunia. Kesi hizi zimekuwa na washabiki ndani ya nchi kwa namna ambayo kwa hakika inashangaza, kwamba inawezekananaje mtu akashangilia kuona basikeli au hata mkokoteni kwa nyumbani kwao unatumika kusomba mazao au kuchota maji unauzwa, ni kukosa uzalendo kwa kiwango cha juu.

Kuamshwa kwa ari mpya ya uzalendo na ujasiri wa kuipenda Tanzania kulikojengwa misingi yake kwa ujasiri mkubwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Jemedari Hayati John Magufuli na msaidizi wake wa wakati huo Mama Samia Suluhu, kumeanza kuzaa matunda katika kesi tunazoshitakiwa nje ya nchi dhidi ya mali za taifa letu.

Ushindi ilioupata Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, katika uamuzi uliotolewa Aprili 19, 2021 dhidi ya kesi ya Rufaa ya familia ya Vipula D. Valambhia, iliyokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya juu ya Marekani (Supreme Court of the United States) ambayo wadai walikuwa wanaidai serikali ya Tanzania wakitaka kulipwa dola milioni 50.6 kutokana mgogoro wa mwaka 1985 wa kusafirisha vifaa vya wizara ya Ulinzi ni kielelezo cha halisi cha ujasiri na uzalendo halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mkulima wa Afrika Kusini, hawa nao walitaka wapewe kibali na mhakama kukamata mali za Tanzania, kokote kule duniani.

Ushindi huu ni hatua kubwa sana kuelekea kujitambua na kusimama kutetea hai zetu kama taifa, ilivyo sasa tofati na huko nyuma, Watanzania tumejengewa hali ya kujiamini, kujitambua na kuwa tayari kutetea nchi yetu na kwa hakika inatupasa kuona fahari kwa namna ambavyo awamu ya tano imekuwa na mambo mengi muhimu kwa taifa letu, moja muhimu zaidi kwa hakika ni hili la kutambua wajibu tuliona nao kama taifa katika kulinda, kuhifadhi na kutetea rasilimali zetu dhidi ya unyonyaji na ukwapuaji wa aina yoyote ile.

Matumiani yetu ni kwamba, chini ya uongozi wa Jemedari wetu Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, moyo huu wa uzalendo na ujasiri utaendelezwa na kuimraishwa kwa sababu hii ndiyo siri kubwa nyuma ya mafanikio ya taifa lolote lile.

Tunaweka imani yetu kwa Mama Samia, juu ya msingi kwamba, tofauti na Rais yeyote wa nchi hii, yeye anajua yote waliyoyapanga, kufanya na kutarajia kufanya na mtangulizi wake, tumtakie kila lakheri katika kuuendelea kuujenga na kuuimarisha uzalendo na ujasiri wa Watanzania, kwa sababu ni katika huo ndiyo tumeweza kuushinda ubeberu na kwa huo tutaendelea kushinda na zaidi ya kushinda.

ASANTE SAMIA
 
Shida yenu mnalazimisha UZALENDO kuwa ni Utii kwa rais na serikali yake.

Uzalendo ni kwa nchi. Hivyo utashangaa mtu anayepingana na serikali ndio anakuwa mzalendo hasa.

Tundu Lissu amepambana na ukandamizaji na uvunjifu wa haki toka enzi za Mkapa, ambapo serikali ya CCM ikishirikiana na makampuni ya uchimbaji wa madini, ambayo iliingia nayo mikataba feki, iliwanyanyasa raia wote waliokuwa wanapingana nayo, hata kuwabambikizia kesi hata za mauaji. Tundu Lissu aliwatoa magerezani zaidi ya wahanga 400, tena bila malipo yoyote. Tundu Lissu alifanya haya hata kule Nzega, ambapo mbunge Bashe alikiri hilo bungeni, akitofautiana na wenzake wa CCM.

Lissu aliendelea na harakati zake katika migodi mingine, ambapo alijikuta akipambana na serikali, hata kuwekwa ndani mara kadhaa. Kali zaidi ni pale serikali ilijitahidi kufunika tukio la wachimbaji wadogo kufukiwa huko Bulyanhulu. Baadaye Lissu alihamishia uwanja wa mapambano bungeni.

Ili "kuifuta" rekodi hiyo njema, serikali ya Magufuli ilitumia nguvu nyingi, na vyombo vyake vya propaganda, kumpaka matope Lissu kwamba "anashirikiana na mabeberu". Kazi hiyo ndiyo unaiendeleza katika huu uzi wako.

Kumpaka matope mtanzania mzalendo wa kweli, na wengine kama yeye.
 
Back
Top Bottom