Uzalendo, tija na ufanisi: Ni kipi muhimu zaidi viongozi wetu kuzingatia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzalendo, tija na ufanisi: Ni kipi muhimu zaidi viongozi wetu kuzingatia?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mtazamaji, Apr 28, 2012.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu

  Kwa kimombo kama sijakosea maneno hayo ni Patriostism, Efficiency na effectivenss. Kwa kiongozi au mfanya maamuzi yeyote hayo ni mambo matatu muhimu ya Kuzingatia.

  Katika Kudadavua mtandao nikakutana na kipande Hiki
  Kwahiyo tunaona kumbe sio tu suala la usalama linaloamua gani litumiwe kwa viongozi au sio tu suala la utaratibu wa zabuni. Kuna uzalendo ndani yake na sometime kuna kutazama tija na ufanisi.

  Sasa Kwa kina HKigwangalla, Nape Nnauye, Zitto, John Mnyika
  • swali Kwa wana CCM na serikali yake na wabunge ni vigezo gani bado vinatumika kuendlea na mashangaigi kwa vingozi amabao hata kwa safari zao za mkoa a wanapaa kwa ndege ?
  • Swali kwa CDM CUF na NCCR, etc je wenzetu mngekuwa na serikali ni gari gani mawaziri, RC,,DC na watendaji wakuu wagetumia? Ni vigezo gani mtavitumia. zaidi magari mawaziri.wenu watastahiki kukaa kwenye nyumba za vyumba vingapi , wapi? etc....

  any way nimegusia mfano wa magari.; Lakini kwa wanajamvi tujadiliane kwa hoja zaidi ya nadharia ni maamuzi gani au taratibu gani au mambo gani yanatakiwa kutowepo au kuwepo ili utendaji uwe wa tija ufanisi na wakti huohuo wakiweka maslahi ya taifa?

  Yaani wewe mwana JF ungekuwa waziri au chochote cha kimaamuzi nimambo gani kwako ungeyapa kipaumbelele kwenye majukumu na wajibu wako na ungeyafanikisha vipi, bora zaidi kuliko inavyofanyika sasa ?

  NB
  In this case tuna-assume tanayo katiba mpya tayari tena safi kabisa. so sitegemei response ya tunahitaji katiba mpya.


  Tuendelee
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  If I were in the position to make political decisions, the first thing I will do is to tell the nation that it should live within it means, and the best way is to cut spending. I would rather have fewer government schools that offer decent education than a flood of schools that offer nothing.

  I will negotiate with the public and parliament to make sure that people that are elected to serve the public in various positions receive salaries and other benefits that are proportion to their services. For example, if you are a member of parliament don't expect to pay off you luxury car loan in one year, even in America public officials don't shop cars the way our senior public officials do.

  Now with regard to Patriostism, Efficiency na effectivenss (PEE), they don't come easy in a country which experience a very low public morale. In a public endeavors, Tanzanians have very low expectations because many things have been promised, but the end results have been poor. ​
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Zakumi nakubalinana wewe hapo wenye Bold. Inawezekana Salaries eesa na benefits wanzopta MP ni "kidogo".

  Lakini kinachoshangza
  • wapo wanasiasa wanasahau kuwa hicho kidogo kina apply to everyone working in every position kwenye public sector. Kasi yareform marupupu na mishara sihara ya wanasiaa (egwabunge ) ina priority kuliko
  • Hivi sasa "Protocol ya maslahi" inamuweka mbunge wa jimbo kuwa bora zaid kimaslahi kuliko afisa elimu, maji, afya, mifugo au hata RPC wa wilaya au mkoa. Je accroding to your view proportio na and imporatance ya service ya mbunge ni kubwa kuiko ya RPC au afsa Elimu wa mkoa ?


  Kwa uchokozi kwako na kwa member unaweza kutoa mchanganuo linganifu. unadhani Mbunge alitakiwa/anatakiwa kupata zaidi au pungufufu kiasi gani kuliko. Afisa Elimu,Maji, Afya.Mifugo . Assuming all other factor are constants na umezingatia PEE vizuri kabisa


  Naweza kuonekana kituko lakini binafsi nachojiuliza ni wabunge wangapi wanashangazwa wao kuwazidi mishahara watendaji hasa ambao ndio wanaotakiwa kuwa mstari wambele kuleta maendeleo huko mikoani/wilayini kupitia elimu,afya, Kiimo ulinzi. So naona kuna ka uzalendo kananazidi kukosekana na kupotea
   
 4. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  vyote ni muhimu
   
 5. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  UZALENDO ndio baba wa Ufanisi na Tija! Wapo wataalamu wetu kibao nje ya nchi, ufanisi wao unaleta tija ugenini, lakini uwapi uzalendo wao? Uzalendo ni pamoja na ufanisi na tija, lakini tija na ufanisi tu, haviwezi kuwa uzalendo, hadi pale mazingira yanaporuhusu!

  Kwa kiongozi yeyote madarakani, kuwajenga wananchi wako katika hali ya kujua ushiriki wao katika kuleta maendeleo na kutekeleza, ni silaha kubwa kwa uongozi, kwa sababu wao ndio watekelezaji wewe ni kusimamia tu. Lazima ujenge imani yao kwako kama kiongozi wao, kama unahubiri uzalendo, na uwe wa kwanza kuutekeleza! Sera na falsafa zikiukazo misingi ya imani zao, ni hatari...si rahisi kupokewa. Ipo misingi mikuu ya imani zao, pitia huko. Pia "UONGOZI NI UBUNIFU" usipokuwa nao, umeumia.

  Mungu wetu anaita!
   
 6. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #6
  May 18, 2013
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Kuna heshima ambayo taifa lolote lazima lazima iifikie, heshima hiyo imelala katika mafanikio yake.
  Mafanikio hayo hayotopatikana pasipo utayari wa raia kuyafuata, Pasipo kufanya jitihada za kuyakaribia, pasipo kufanya jitihada za kuyashika, kwa juhudi zisizofifia.

  Inaweza kuwa safari ndefu, Inaweza kuchukua vizazi vingi, lakini ni lazima tuanze safari hii.

  Hata kama soli za viatu vyetu zikiisha kwaajili ya safari hii, sisi kama taifa ni lazima tujue…safari yetu ni moja..tuna hii ndoto kubwa, tuna jukumu la kufanikisha..

  Dhamira yetu ni lazima iwe kama kiu jangwani, kwa umoja na wajibu tunaweza kuwa nguvu isiyozuilika. Tunaweza kuwa mafuriko.

  Sisi watanzania tuna nguvu hii. Nguvu hii iko mikononi mwetu. Ni nguvu ya umoja na imani isiyotetereka ya kuona taifa hili likinyanyuka.

  Ni ukweli, watu imara hujenga mataifa imara na watu dhaifu hujenga mataifa dhaifu.
  Huu ni wito wa uzalendo maana halisi ya kuliweka taifa pamoja. Tutalisongesha taifa hili ikiwa tu, tutakuwa wamoja na wazalendo.


  Lakini bila serikali imara na shupavu, bila serikali yenye malengo na nidhamu, hatutafanikiwa.
  Ni ukweli usiopingika nguvu hii iko mikononi mwetu, Nguvu ya kubadilisha hili taifa imelala kwenye mikono yetu. Ni wakati wetu kuamua mwelekeo wetu kama taifa.

  Kitabu kiu ya UZALENDO. KITAWAJIA HIVI KARIBUNI MTAANI. MOJA YA KURASA ZAKE.
   
Loading...