Uzalendo ni Wabunge kupunguza Mishahara yenu iende majimboni miradi ya maendeleo

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Inasikitisha sana mbunge anapata mshahara wa sh.Mil.11 na kiinua mgongo cha sh.Mil.200 na hakatwi kodi na huo mshahara na kiinua mgongo ni kodi za wananchi leo anasimama mbunge na kudai wananchi wakatwe kodi ya uzalendo.

Kama ni uzalendo anzeni nyinyi wabunge wenye mishahara ya mamilioni kukatwa pesa na ziende kwenye miradi ya maendeleo majimboni kwenu huo utakuwa uzalendo.

Wananchi wanyonge na masikini mnawarundikia utitiri wa kodi nyinyi mnastarehe kwa mishahara minono na magari mazuri hebu waoneeni huruma wapiga kura.
 
Linapokuja suala la mishahara yao wabunge wote wanakuwa kitu kimoja tena wanaunda umoja wenye nguvu sana bila kujali itikadi za vyama vyao unafiki ndio unaolikwamisha taifa hili.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wabinafsi sana hao Wabunge uchwara ndani ya miaka mitano wanapata zaidi ya milioni 900 sawa na zaidi ya milioni 180 kwa mwaka na hawafanyi chochote cha maana Bungeni.
 
Back
Top Bottom