Uzalendo ni tatizo kubwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzalendo ni tatizo kubwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Midavudavu, Apr 24, 2012.

 1. M

  Midavudavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Temetoka mbali sana. Misingi mingi ya uzalendo iliyojengeka miaka mingi ya nyuma sasa imeanza kupotea. Suala la kutunza na kuheshimu mali za Umma siku hizi ni jambo ambalo masikio kwa watu wengi hivi sasa halina mvuto. Hivi sasa watanzania walio wengi ni wabinafsi wanajipenda wenyewe kuliko Nchi yetu.

  Kila mmoja wetu anaona mwenzie anakosea lakini ni suala la muda tu na yeye akipata nafasi kama hiyo anafanya vibaya zaidi kuliko hata yule wa awali aliyekuwa analalamikiwa. Tunahitaji kurudi na kukaa chini na kutafakari wapi tumekosea kunakopelekea idadi kubwa ya watu kukosa uzalendo. Viashiria vya kuonyesha watanzania wanapungukiwa na moyo wa uzalendo na utu ni vingi sana naomba nikupe mifano halisi ambayo imetokea;

  1. Ajari ya gari iliwahi kutokea katika kitongoji kimoja katika wilaya ya Masasi ambapo wananchi wa eneo hilo badala ya kusadia majeruhi ili wawahishwe hospitali waliwaibia mizigo yao, fedha mifukoni na simu (Ina maana kuwa idadi kubwa ya wana kitongoji hiki ni wakatili)

  2. Lipo tukio moja la jambazi mmoja mjini Dar es salaam aliyekuwa anafukuzwa na polisi pamoja na wananchi baada ya kufanya uhalifu. Jambazi hilo lilirusha baadhi ya noti za fedha hewani na hapo ikawa mwisho wa zoezi la wananchi kumfukuza huyo jambazi kila mmoja alijipa kazi mpya ya kuokota zile noti na kutia mfukuoni mwake(Wanachukia majambazi lakini wanajipatia mapato ya jambazi).

  3. Wapo wananchi ambao walijaribu kuiba mafuta baada ya gari ya mafuta kupata ajari badala ya kufasnya uungwana kuwasaidia wahanga wa ajari hiyo. Gari hilo lilishika moto hatimae na watu kadhaa walifariki na wengine kupata majeraha makubwa ya moto.

  4. watu kuhongwa fedha na vitu ili kuwapigia kura wagombea wa nafasi mbalimbali za kisiasa. Ni wachache wanaokataa zawadi hizo na matokeo yake baadhi ya nafasi za uongozi zimeshikwa na watu wasio waadilifu huku wananchi wakilalamika bila ya kujua hicho kinacho lalamikiwa ni matokeo ya kazi za mikono yao wenyewe.
   
Loading...