Uzalendo na Utaifa tuliuuwa wenyewe CCM, tuantaka nini tena? TV hazitauokoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzalendo na Utaifa tuliuuwa wenyewe CCM, tuantaka nini tena? TV hazitauokoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jun 17, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mapema mwaka 1963 lilianzishwa Jeshi la Kujenga Taifa hapa nchini kwa lengo la kuwalea vijana kwa kuwafundisha umoja na uzalendo, kuwafundisha mbinu za uzalishaji mali na mafunzo ya ulinzi. Source: Jeshi la Kujenga Taifa

  Mmeiua JKT ili iweje? Kuimarisha au kulegeza umoja wetu na umakini katika uongozi na nidhamu ya utawala na katika kuzalisha mali? Lengo ni nini? Ni kubana matumizi au Ili kujenga mwanya wa wajanja waendeshe mambo wanavyotaka?Maana JKT ilikuwa inaweza kuitegemea kwa asilimia kubhwa tu, ukiachilia mbali askari walimu ambao kuwepo kwao ba matumizi yao hakuathiriwi na bajeti yeyote. Na sasa wako wengi tu na shughuli yao ingekuwa hii mojawapo wakati huu ambapo hatuna shughuli za kivita. Huku ndiko kulikokuwa kunatoa wataalamu mbalimbali wakiwemo wanajeshi, watu wa usalama wa taifa n.k na ilikuwa inachuja kwa utaratibu mzuri kabisa. Sijui vijana wa TISS wanatoka wapi siku hizi? Na wajeshi? Mna mfiumo mbadala au ndio mmepata nafasi ya kuchomeka watoto wenu na wa ndugu zenu katika mifumo hii nyeti kama mnavyofanya kwenye chama chetu cha siasa?

  Mkajenga hoja mpaka mkafanikiwa. Sasa limekufa, mnahaha kujenga taifa kwa TV, na majukwaa bila utaratibu unaoeleweka wapi na wapi. Mtakula matapishi yenu. Nyenzo kama hizi zilizokuiwa zimejaa uzalendo meziteketeza sijui kama huko tuendako tutaweza kukumudu. Tena kipindi kinachorushwa TBC cha Amani yetu hakjiwafikii walengwa, maana walengwa ni vijana, walio wengi kwa idadi, na wengi kati ya watu wanaojishughulisha sana kwenye hilo mnaloliita uvunjifu wa amani. Kipindi cha kizee kama kile mnapoteza 'air time', kuweni wabunifu msiwe kama watu ambao hamkwenda mafunzo ya propaganda, najua bado mpo mliopelekwa kusomea haya. Mbinu muafaka kwa kundi muafaka kama mnataka kufikia malengo. nikimaanisha mfanye mambo kisayansi na si kiushabiki.
   
 2. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Si dhani JKT ndo suluhisho la uzalendo...Uingereza hakuna national service lakini ni wazalendo sana..Jingine hata JKT nako kuna madudu sana tu ,sema ukiripoti unatafutwa kwa sheria ya usalama wa taifa. Nilikwenda JKT Makutupola miaka ya 90 wakati kuruta wengine tukila kwa kunyakuwa watoto wa wakubwa walikuwa wanakula SGT mess..sasa usawa uko wapi hapo...Tunaendesha nchi kwa kujuana badala ya kufuata sheria,kanuni na taratibu uwanja wa kujuana hauna sheria hivyo tusilaumiane
   
Loading...