Uzalendo haijawahi kupewa kipaumbele kwa viongozi wa juu katika Utumishi wa Umma

FIKRA HAI

JF-Expert Member
May 22, 2013
231
79
Uzalendo ni hali ya kuwa tayari kufia masilahi ya wengi kuliko kutanguliza masilahi binafsi katika maisha yetu ya hapa duniani. Dhana hii inaweza kuwa na zaidi ya mtizamo wangu hasa katika maisha tunayoishi.

Nitoe mtizamo wangu mdogo katika mabadiliko ya Baraza la mawaziri lililofanyika. Nisikitike tu kusema kwamba kuwa mabadiliko haya hayajalengo kumsaidia Mwanchi wa chini zaidi Ni kujenga mtandao na undugu kwa masilahi binafsi.

Miezi michache iliyopita tuliona kuwa Kuna watu walidhoofisha kwa makusudi makubwa juhudi za kuwa na umeme wa uhakika kwenye bonde la stiglers George na badala yake wakaona Ni muhimu kulinda uhai wa wanyama kuliko binadamu wenzake.

Hili tu lilitosha kuonesha ukosefu wa Uzalendo katika kujenga taifa la wazalendo. Uzalendo umekosekana kwakuwa tumeonesha kuwajali wanyama kuliko binadamu ambao ndio msingi mkubwa wa madaraka.

Dhana ya Uzalendo haijawahi kupewa kipau mbele kwa viongozi wengi wa juu Katika utumishi wa umma, hiyo ubinafsi usio na kipimo ndo unajengwa kwa Kasi ya ajau mno.

January makamba aliondolewa na Mtangulizi wako baada ya kupinga juhudi za kuwa na umeme wa uhakika huko mbeleni badala yake akaweka masilahi ya Wamarekani ili waendelee kutuuzia umeme kwa Bei ya juu zaidi.

Bunge lelimehja vijana wengi wasomi na wenye uweledi, ulipaswa kuwapa nafasi kuliko kurudia makapi kwa msingi wa huo tuamini kuwa Serikali yako haijli kilio cha wananchi ndio maana kwa Sasa wasaidizi wako wanashinda Dare sasalaama kulipana perdiem huku mkiongeza tozo za kuwaumiza wananchi wa kawaida wakati makao makuu ya nchi ni Dodoma na kila Jambo lingefanyika Dodoma.

Uzalendo ninaouzungumza Ni kuimarisha shule zetu na kuhakikisha kila kiongozi wa Serikali kuanzia Rais wabunge, wakuu wa Wilaya watoto wao kusoma shule za kataka Kama wengine. Haya yaliwezekana kwa mzalendo pekee wa nchi hii Mwalimu Julius Kambarage Nyerer tu.

Chuki inayojengeka kwa Kasi dhidi ya wananchi Ni mbaya sanaa na sio dalali nzuri katika nchi tunayohubiri amani. Mapinduzi yanayotokea katika nchi za Africa Ni kikomo Cha juu zaidi Cha uvumilivu wa viongozi hasa wanasiasa wannaotanguliza undugu katika teuzi, urafiki, ukabila na udiniambao ulipigwa Vita na muasisi wa taifa hili.

Huwezi ukawa unanisisitiza Uzalendo wakati wewe umeshindwa kuuoneaha Uzalendo huo. Kifo kinasubiri tu hata Kama utalala juu ya hela nyumbani kwako, hela hazizui uhai wako, kuwa mzalendo mjali Mwanchi wako ulipo nsio kwa nguvu zako Ni mapenzi ya Mungu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom