Uyui, Tabora: Atuhumiwa kumuua aliyemuoa mkewe

Nuraty J

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,729
3,829
By Mwandishi Wetu

Tabora.
Mkazi wa Kijiji Cha Nyangahe, kitongoji cha Lungu ,wilayani Uyui, Mhonyiwa Mwanagwalila. anatuhumiwa kumuua Mgogo Gwahendwa ambaye alimuoa mke aliyemuacha.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatano Agosti 11, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Safia Jongo,amesema tukio hilo limetokea jana katika katika kata ya Bukumbi wilayani Uyui.

Amesema marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine hali iliyomfanya mtuhumiwa apate wivu na hivyo kuamua kumvizia mwanaume aliyemuoa mkewe akiwa njiani na kumuua.

Kamanda Jongo amesema mtuhumiwa alikuwa na wenzake ambao baada ya kufanya mauaji hayo hawakuchukua chochote licha ya marehemu kuwa na Sh 200,000 na baiskeli.

Kwa mujibu wa kamanda Jongo, mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kufanya mauaji, akidai kulipiza kisasi kwa kumuua aliyemuoa aliyekuwa mkewe.

Diwani wa kata ya Bukumbi, James January, amesema marehemu aliwahi kufumaniwa mara mbili na mtuhumiwa na baadae aliamua kumuoa mwanamke huyo baada ya kuachwa.

Mkoa wa Tabora unakabiliwa na matukio ya mauaji yanayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo wivu wa kimapenzi,imani za kishirikina na ulipaji visasi.

Chanzo: Mwananchi
 
KABLA HUJAMLAUMU MTUUMIWA NAOMBA UELEWE KUWA:

Marehemu amewahi fumaniwa mara mbili akitembea na mke wa muuaji.

Mara ya kwanza, muuaji alimsamehe mke wake akaendelea na maisha yake...

Mara ya pili akawafuma, jamaa akaamua kumuacha mke wake kwa sababu ya uzinzi..

Baada ya kuachana, marehemu akaamua kumuoa mwanamke ambaye amewahi kukamatwa akizini nae.

Mtuhumiwa kakosea...ingefaa kama angewaua wote wawili.
 
Ila marehemu alikuwa na moyo mzuri. Kanuni ya uanaume ukiwa na mke wa mtu akiachwa na mumewe nawe unamuacha. Maana atafanya yale mliyofanya nae kipindi hajawa wako.

Sasa ye hii kanuni ameshindwaje kuitumia?
 
Back
Top Bottom