Uyoga uliwaponza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uyoga uliwaponza

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by mahiya, Jun 4, 2009.

 1. m

  mahiya Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa na mkewe walikuwa wakitokea shamba. Wakiwa njiani waliona uyoga pori, wakaamua kuung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwamba ule uyoga pori unaweza kuwa na sumu. Basi wakaamua wapike kiasi kidogo kwanza wampe mbwa wao ale, ili asipokufa mbwa nao wapike ule uliobaki ili waule. Wakakaa siku ya kwanza na siku ya pili, mbwa hakufa. Wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.

  Walipomaliza kula tu, mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shuleni, akawaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa barabarani. Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi tena mwisho wa maisha yao ndio umefika, wakaanza kujuta kwamba muda wowote watakufa tu kwa kuwa wamekula uyoga wenye sumu kama mbwa alivyokula na sasa mbwa amekufa kwa kula uyoga huo!

  Basi yule baba akaamua kumwomba mkewe amruhusu atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinawajia wakati wowote na akifa kabla ya kutubu dhambi zake ataingia motoni. Mke alipotoa ruhusa jamaa akaanza kumwambia na kumuangukia mkewe amsamehe kwamba amefanya maovu mengi. Kwanza alikiri kuwa ujauzito wa msichana wa kazi waliyemfukuza ulikuwa wake. Pili mdogo wa kike wa mkewe anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi ila mapenzi yao huyafanya kwa kificho. Tatu ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake hivyo anaomba sana chonde chonde mke wake amsamehe kwa dhati ili mungu naye amsamehe.

  Alipomaliza mume, Mama akasema anashukuru kwa hayo yote na ameshamsamehe. Basi naye akaomba atubu kwa mume wake madhambi yake. Akaanza kwa kusema kuwa mtoto wa kiume mdogo si wa mumewe bali alizaa na Shamba boy wao. Pili ujauzito aliokuwanao wakati ule ulikuwa wa mpangaji wao humo ndani. Jamaa kusikia hayo hakusubiri amalizie! akapandwa na jazba zenye hasira kali ukawa ugomvi mkubwa mle ndani.

  Wakati wakiendelea kugombana, mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani na kukuta wakigombana. Akawauliza, Baba na Mama mnagombania nini? Hivi mnafahamu kuwa mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule nje? Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari wakabaki vinywa wazi wakitazamana wakiwa wamepigwa bumbu wazi. Baada ya majuma mawili ya kuishi kwa kununiana, ndoa ilivunjika!

  WANA JF mwasemaje Mnaona wanaume wasivyo wavumilivu?
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka zamani niliwahi kuona Filam katika luninga (Comedy) kuhusiana na kisa kama hiki... Sikumbuki ni channel gani ila ni kule Zambia.
   
 3. S

  Simoni Member

  #3
  Jun 6, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hello Xpaster waliicheza akina Maximo, Zulu na Goliath wa Zambia National Service miaka ya 1987 au 1988 kama sikosei.Mbwa alikanyagwa na Caterpillar ya Mazembe.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Yeeeeh, there you are...! ekizaktiri...

  Ahsante mkuu kwa kumbu kumbu.
   
Loading...